Jamii isiyo na utaratibu ni sasa na kundi la nani. Binge lina utaratibu hivyo ni budi ufuatwe. Hata vikoba vina utaratibuSio tabu kijana,tunahitaji hoja mbadala.
Amani iwe kwenu.
Kwa mara ya kwanza nchi imekuwa na kambi ya upinzani iliyoshindwa kutekeleza majukumu yake sijui kwa umbumbumbu ama makusudi.
Hivi kususa kutoa mpango mbadala kunaboresha vipi upinzani? ama kunaathiri vipi serikali? Hotuba nyingi hasa zile zilizowasilishwa na Wabunge wa Chadema hazina mpango mbadala wala namba. Zimejaa vijembe na kushambulia watu. Huwezi kufanya ulinganisho wa mpango wa serikali na upinzani.
Mbunge anavunja kanuni za bunge ili kupata "attention" ya media kueleza upotoshwaji. Mfano hotuba ya Lema imeingiza mambo ya uuzwaji wa nyumba za serikali ambayo kimsingi ni wizara nyingine, Mambo ya Lugumi ambayo yanachunguzwa na kamati ya bunge hivyo kikanuni na kisheria hayapaswi kujadiliwa bungeni. Anaambiwa kuyatoa na Kamati ya Kanuni anazira kwa sababu kufanya hivyo hotuba yake itakuwa imekwisha. Hivi mpango mbadala uko wapi? Kwanini mnaruhusu upumbavu na ulofa kutamalaki hapo Chadema?
Hivi kwanini mnasusia vikao vya bunge siku wake/vimada wenu wakiwa hapo dodoma? manake Lema hakuona la maana la kuongea zaidi ya kumsifia mkewe. Aibu yenu.
Kwa vijana wadogo, Mh. Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Temeke miaka ya mwishoni 90. Aliiwajibisha serikali na mawaziri kujiuzuru bila ya Bunge kuwa "Live"... Ndio walijiuzulu... Prof.Mbilinyi (Fedha), Dr. Hans Kitime nk. Alitoa hoja ambazo hata wabunge wa CCM walimuunga mkono. Kambi rasmi ya upinzani isipobadilika mtakiona cha mtema kuni.
Kwa siasa za nyakati hizi mtapotea; kususa, matusi, selfie, bunge live havileti barabara, maji, umeme, afya nk kwa wananchi.
Nilikuwa pia napendekeza CAG atukagulie elimu za wabunge wa kambi ya upinzani hususani Lema, Msigwa, Kubenea, Sugu na Lijuakali na iwe wazi kama ya ATCL na TTCL.
Nawasilisha.
Pole kijana najua umeumizwa na ukweli hapo juu.Ungesoma niliorodhesha mawaziri wengi nikaweka nk.Inafurahisha mtu "makini" kama wewe unatoa hoja dhaifu huku unalialia.Pole sana jiwe la kizani halichagui.Kwanza mtoa mada hujui unalolisema umejawa na ushabiki ambao unaonyesha kua ni mbumbu aliyesababisha mawaziri kujiuzulu alikua mzee Mzindakaya mara nyingi najiuliza hivi kwanini mnatoa mada za uongo ni maana watu makini wanashindwa kuchangia mnaidhalilisha hii forum punguzeni ushabiki au kutumiwa
Ni moja ya mchango unaoonyesha utambuzi mdogo kabisa kufikiri.Hivi hujui pia kazi ya CAG nikukagua ubora wa "manpower"?Siku nyingine usichangie ukiwa na hasira.Najua Lema ni "role model" wako ila ukweli mchungu lazima uzungumzwe.Jikite kwenye mada.Sawa bana mchambuzi!! Ila kumbuka unavyoona kuwa Lema kachanganya mambo hana tofauti na wewe! Umesema CAG akague elimu za baadhi ya wabunge!! Hujui hata kazi za CAG, lakin pia hujui hata kigezo cha kuwa mbunge! Utajitofautishaje na Lema?! Kwangu mimi ni afadhali hata hawa wabunge wanaojaribu kuzungumza kuliko hao mabubu wa ccm walioko bungen! Wao wanajua "ndiooooooo" tu!
Tumia kichwa cha juu kufikiri, cha chini kitakupoteza kama unavyowaza kuwa upinzani unapotea!!
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Hizi akili kiwango cha Kubenea,ipo siku Mbowe atawambia mnywe mkojo mtakunywa.Enyi vijana wa bavicha ni lini mtakubali kuondoka kwenye minyororo ya utumwa?Ndo kiwango cha juu cha uwezo wao wa kufikiri, ila ndo wanaoaminika kwa hoja lumumba. Tutegemee nini kwenye bunge la Agnes?
Amani iwe kwenu.
Kwa mara ya kwanza nchi imekuwa na kambi ya upinzani iliyoshindwa kutekeleza majukumu yake sijui kwa umbumbumbu ama makusudi.
Hivi kususa kutoa mpango mbadala kunaboresha vipi upinzani? ama kunaathiri vipi serikali? Hotuba nyingi hasa zile zilizowasilishwa na Wabunge wa Chadema hazina mpango mbadala wala namba. Zimejaa vijembe na kushambulia watu. Huwezi kufanya ulinganisho wa mpango wa serikali na upinzani.
Mbunge anavunja kanuni za bunge ili kupata "attention" ya media kueleza upotoshwaji. Mfano hotuba ya Lema imeingiza mambo ya uuzwaji wa nyumba za serikali ambayo kimsingi ni wizara nyingine, Mambo ya Lugumi ambayo yanachunguzwa na kamati ya bunge hivyo kikanuni na kisheria hayapaswi kujadiliwa bungeni. Anaambiwa kuyatoa na Kamati ya Kanuni anazira kwa sababu kufanya hivyo hotuba yake itakuwa imekwisha. Hivi mpango mbadala uko wapi? Kwanini mnaruhusu upumbavu na ulofa kutamalaki hapo Chadema?
Hivi kwanini mnasusia vikao vya bunge siku wake/vimada wenu wakiwa hapo dodoma? manake Lema hakuona la maana la kuongea zaidi ya kumsifia mkewe. Aibu yenu.
Kwa vijana wadogo, Mh. Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Temeke miaka ya mwishoni 90. Aliiwajibisha serikali na mawaziri kujiuzuru bila ya Bunge kuwa "Live"... Ndio walijiuzulu... Prof.Mbilinyi (Fedha), Dr. Hans Kitime nk. Alitoa hoja ambazo hata wabunge wa CCM walimuunga mkono. Kambi rasmi ya upinzani isipobadilika mtakiona cha mtema kuni.
Kwa siasa za nyakati hizi mtapotea; kususa, matusi, selfie, bunge live havileti barabara, maji, umeme, afya nk kwa wananchi.
Nilikuwa pia napendekeza CAG atukagulie elimu za wabunge wa kambi ya upinzani hususani Lema, Msigwa, Kubenea, Sugu na Lijuakali na iwe wazi kama ya ATCL na TTCL.
Nawasilisha.
Hizi posho kufutwa zimewachanganya sana.Wabunge wengi wa upinzani wanawaza kupiga dili tu hawana mda kutumikia watu.
Kijana naandika ukweli sihitaji malipo.Mimi ni Raia mwandamizi katika nchi hii.Nilijuwa wewe sababu Lema ni "role model" wako lazima itakuuma.Pole.Pamoja na kwamba Unajitutumua kila Leo, ili uonekane kwa viongozi wako, lkn ukweli ni kwamba CCM huipendi upo huko tu kwa sababu ya njaaa zako, unatia aibu
Toka alipoondoka Slaa chadema hawana hoja
Nondo zilikua zinajadiliwa na kupitiwa halafu anapewa mtu anakwenda kushusha
Enzi za Dr Wilbroad Slaa mbunge asingeongelea shanga bungeni,au kususa kutoa mpango mbadala,jeuri ataitoa wapi?
Hii inaamanisha kuwa hata bajeti isipopita na bunge likavunjwa ,uchaguzi ukiitwa chadema wataambulia patupu kwa kuwa wananchi hawajasikia mipango mbadala yao,wameishia kususa
Nakubaliana na wewe kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ndiyo kila kitu. Mfano mdogi, majuzi hapa huko Tanga, kuna mpiganaji wa Chuo cha Kijeshi huko Tanga alijipiga Risasi, lakini msemaji wa Taarifa ya kuhusu kifo ilitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa TangaKwa taarifa yako wizara ya mambo ya ndani ndio kubwa kuliko wizara zote.maana wizara ya mambo ya ndani haina mpaka inaingia popote.usitegemee wizara ya afya waki iba madawa wizara ya mambo ya ndani ikae kimya,wizara ya ujenzi kukitokea ubadhirifu mambo ya ndani wakae kimya.ndio maana lema kagusia mambo ya mikataba tata,uzwaji wa nyumba za serikali kwa sababu majibu ya usafi na uchafu wa hayo mambo mwenye wajibu wa kuyachunguza na kushtaki ni wizara ya mambo ya ndani.sasa iki kaa kimya watu wasihoji?kumbuka penye moto pana moshi na penye moshi pana moto.hebu jaribu kutikisa ubongo wako uone.
Nawewe muombe CAG awakague,ila kwa dhumuni la mada hii nimeona nipewe CV za hao,mbona unachukia?umeumizwa na hili?
Maskini hivi ndipo ulipofika,hujui hata majukumu ya CAG?..hivi alivyoaudit viwango vya elimu vya TTCL na ATCL ilikuwaje?Hakuna anayeumizwa ila watu wanakudharau. Hata kama unashikiwa akili CAG anakagua CV? yeye anahusika vipi na sekta ya elimu? Hilo ungesema Prof Ndalichako ungeeleweka.
Vipi wapiga deki barabara na wazungurusha mikono walichagua kwa kufuata mihemko au posho?Nusu ya wananchi wa Tanzania wanachagua viongozi kwa mazoea, ujinga, rushwa na ushabiki. Asilimia karibia 70 ya wapiga kura hakuna anayeelewa sera ni nini bali wanachagua kwa vionjo vya udini, kabila, ukanda na sifa nyingine nilizotaja hapo nyuma. Kwa taarifa yako watu walikuwa wanachagua mtu na sio sera. Mfano wengi wa waliomchagua Magufuli waliendeshwa na mazoea, kabila lake nk. Na waliompa kura Lowassa hali kadhalika. Nadhani kwa wagombea wote ni asilimia chini ya tatu tu waliompa kura mgombea yoyote kwa ajili ya sera zake. Kwa hiyo kujidanganya eti cdm wataambulia patupu labda mazingira hayo hapo juu yasiwepo.
Vipi wapiga deki barabara na wazungurusha mikono walichagua kwa kufuata mihemko au posho?