Upendeleo wa kijinsia ni chanzo cha ukatili wa kijinsia, wanaharakati liangalieni

DON YRN

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
475
999
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania!... na kazi iendelee.

Nilikuwa napitia habari na majalada mbalimbali humu mitandaoni kuhusu ukatili wa kijinsia hasa kwa wanandoa, aisee hali inatisha mno hasa kwenye huu uchumi wa kati.

Kuna nyakati inabidi kukaa chini km Taifa hasa taasisi zinazohusika na masuala ya jinsia kuangalia ni wapi shida ilipo hasa ktk sheria na sera zetu?. Ni kweli matukio ya ukatili kijinsia yapo miaka na miaka lkn cha kujiuliza ni kwa yanaongezeka kila mwaka badala ya kupungua?.

Kama ni kuelekea kwenye 50/50 kwenye kila idara tunaelekea, lkn kwa nn vitu hivi vinaongezeka?, mlishwahi kujiuliza shida nn?

Sawa, basi tuseme ni ugumu wa maisha km wengi wetu tunavyojiaminisha ila amini hili siyo kweli!. Wengine wako vizuri mno kiuchumi!

Tuambiane ukweli na bila kufichana; uwepo wa taasi na sera nyingi zinazompendelea mwanamke zaidi kuliko mwanaume ni CHANZO!

Kiwango au speed ya hizi sera za kumuinua mwanamke ni kubwa mno na sisi wanaume hatujaandaliwa KISAIKOLOJIA kuweza KUUKABILI huu ukweli!. Kuna sera nyingi za kumkandamiza mwanaume pengine zinaenda mbali zaidi kuvuka ile hatua ya usawa wa kijinsia hatimaye kupuuzwa na wanaozisimamia!.

Leo hii kukitokea ugomvi nyumbani hasa ule wa makelele kwa mme na mke hata km chanzo ni mwanamke, askari anapofika mtu wa kwanza kukamatwa ni mwanaume tena kwa makofi na mateke(maaskari wa kibongo nazungumzia).

Ni vitu vidogo lkn hebu fikiria ni nn kinatengenezwa kwenye kichwa cha mwanaume?; ni hasira na kisasi.

Kwa sasa sheria za kijinsia zilizopo zipo kumuharibu mwanaume KISAIKOLOJIA wala siyo kumsaidia, ni chache, nyingi zipo kumkandamiza mwanaume tu.

Fikiria wanafunzi wanapopeana ujauzito, mtuhumiwa wa kwanza ni mwanaume na kifungo ni miaka 30 huku mwanamke akirudi shule baada ya kujifungua badala ya kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.

Hii haingalii chanzo ni kipi zaidi ya kuamini mwanamke kurubuniwa. Huwa najiuliza swali; Km mwanamke anarubuniwa, inakuwaje tunawapa taasisi mnaongoza, hamtarubuniwa mtuuze kweli ninyi wanawake?!(natania)

Leo hii kuna matamasha na sherehe za kila aina zinazoratibiwa na Serikali na kufanyika Kitaifa km Siku ya Wanawake, Siku ya Mama, n.k lkn hakuna siku inayoratibiwa Kitaifa kuhusu siku ya Wanaume, Siku ya baba, n.k japo hata kiunafiki zaidi ya siku ya tohara kwa mwanaume tu!.

Yote kwa yote nini kinachojengeka kwenye kichwa cha mwanaume japo wengi wanaweza kupuuza?!, mwanaume anajihisi hathaminiwi kwenye nchi yake!

Leo hii kwenye halmashauri zetu kuna mikopo ya wanawake, vijana na wazee lkn hakuna sehemu inayotaja mikopo ya wanaume kwa maana hiyo wanaume siyo kundi maalum?

Wanaume wengi kwa sasa wanapigwa au kupitia ukatili kwa wake zao, hakuna sehemu ya kwenda kusema na hata ukishaenda kwenye vyombo vya sheria utaishia kukandamizwa na kuambiwa mwanaume hutakiwi kulialia, jikaze mtoto wa kiume, n.k na mwanaume akijikaza cycle inarudi tena kumkandamiza.

Vitendo vya ukatili kwa wanawake husababisha madhara kimwili, kisaikolojia, kiafya na kiuchumi ambayo kusababisha mwanamke kushindwa kushiriki kwenye shughuli za kilimo .

Mwishowe kalipua mtu naye kajilipua na hapo ndo utasikia oooh wanaume mtatumaliza na maneno kibao ya wanaharakati!

Km ni kutozingatiwa kwa usawa wa kijinsia kulifanywa kwenye hizo karne za tangu enzi za akina Yesu na akina Mtume huko, kwa nn hizi lawama zinatumika kumkandamiza na kumbebesha mwanaume wa karne hii ya 21?

Kwa sasa tuzingatiane kwa usawa kweli pasipo na upendeleo wowote kwa maana tunajitengenezea matabaka ambayo yataathiri mienendo ya usawa kwa miaka ijayo na kufanya kundi la wanawake lionekane lina thamani kuliko wanaume.

Wako ktk ujenzi wa Taifa
DON YRN.
 
Umenena vyema Mkuu, ukiangalia hata idadi ya vijana wanaofika vyuo vikuu wengi ni wa Jinsi ya kike. Hii ni matokeo ya mifumo kandamizi ya kielimu iliyoundwa hapo nyuma ambayo ilimbeba mtoto wa kike na kumpuuza mtoto wa kiume.

Kama mtakumbuka miaka ya nyuma (Nina imani hata sasa bado iko hivyo) alama za ufaulu kwa mtoto wa kiume zilikuwa juu sana na wakati huo alama za kufaulu kwa mtoto wa kike zilikuwa chini.

Hii ilichagiza watoto wa kike wengi kuendelea na elimu wakati huo vijana wa kiume wengi waliishia mtaani.

Hili kundi la vijana wengi wa bodaboda na vibarua wa ujenzi na ajira zisizo rasmi ni wahanga wa mifumo hii mibovu iliyopendekezwa huko nyuma.
 
Umeongea kitu cha msingi sana, mtu anapokosa watetezi atajitetea mwenyewe, akijitetea makelele huanza
 
Umenena vyema Mkuu, ukiangalia hata idadi ya vijana wanaofika vyuo vikuu wengi ni wa Jinsi ya kike. Hii ni matokeo ya mifumo kandamizi ya kielimu iliyoundwa hapo nyuma ambayo ilimbeba mtoto wa kike na kumpuuza mtoto wa kiume. Kama mtakumbuka miaka ya nyuma (Nina imani hata sasa bado iko hivyo) alama za ufaulu kwa mtoto wa kiume zilikuwa juu sana na wakati huo alama za kufaulu kwa mtoto wa kike zilikuwa chini. Hii ilichagiza watoto wa kike wengi kuendelea na elimu wakati huo vijana wa kiume wengi waliishia mtaani. Hili kundi la vijana wengi wa bodaboda na vibarua wa ujenzi na ajira zisizo rasmi ni wahanga wa mifumo hii mibovu iliyopendekezwa huko nyuma.
Hiyo ya upendeleo mashuleni hadi vyuoni ipo sana tu, sera na mifumo mibovu mno kuwahi kuanyika kwenye nchi hii.
 
Umenena vyema Mkuu, ukiangalia hata idadi ya vijana wanaofika vyuo vikuu wengi ni wa Jinsi ya kike. Hii ni matokeo ya mifumo kandamizi ya kielimu iliyoundwa hapo nyuma ambayo ilimbeba mtoto wa kike na kumpuuza mtoto wa kiume. Kama mtakumbuka miaka ya nyuma (Nina imani hata sasa bado iko hivyo) alama za ufaulu kwa mtoto wa kiume zilikuwa juu sana na wakati huo alama za kufaulu kwa mtoto wa kike zilikuwa chini. Hii ilichagiza watoto wa kike wengi kuendelea na elimu wakati huo vijana wa kiume wengi waliishia mtaani. Hili kundi la vijana wengi wa bodaboda na vibarua wa ujenzi na ajira zisizo rasmi ni wahanga wa mifumo hii mibovu iliyopendekezwa huko nyuma.
Lkn cha kushangaza walitufikisha apa tulipo ni wanaume wenzetu,
Najarbu kuwaza sijui ilikuaje.

Sasa hivi kwenye jamii tuna watu wa jinsia moja, yaan wanaume pekee, wenye utofauti wa jinsia. Yaan mwanamke anataman na kuingilia majukumu ya mwanaume.

Na hii hupelekea familia nyingi kuwa na migogoro, maana unataka kijinsia ni wa kike lkn anataka afanane na mwanaume kwa kila kitu,

Kuna mdada mmoja kanizingua akiingia kumi na nane atakachokutana nacho wenzake watasimulia huku nyuma

Kuku hawa
 
Mim mbona sijapata logic hata moja hapa. Kuna mtu kakunja kona Kwa kuutaja MFUMO Lakin nae kakosea mtaa Kwa kuzungunza nje ya kinachotakiwa kujadiliwa hapa.
 
Back
Top Bottom