Updates kampeni za uchaguzi Arumeru East CCM v/s Chadema

bernoul.gif

halafu mimi huwa nakukubali sana kwa mambo ya picha mkuu! Hebu angusha kingine mwanangu ni-enjoy
 
Huyu mleta thred nazani kama ni mwanamke hajapata wa kumkole....au kama ni mwanaume basi aende mombasa maana hii nchi siyo yake maana angeionea hata huruma kwa jinsi ilivyo sasa
 
Katika wiki ya pili ya kampeni uchaguzi mdogo wa jimbo la arumeru East vyama vya siasa vimeendelea kuwanadi wagombea wao kwa wapiga kura wa jimbo hilo. Hadi kufikia sasa CCM ndiyo chama pekee ambacho kimejihakikishia kushinda uchaguzi huo kupitia mgombea wake Sioi Sumari.

Chama cha democrasia na maendeleo (Chadema) kinaomba huruma ya wananchi wa jimbo hilo angalau kipate japo kura 3500 ili kujenga imani kwa wafadhili wao wa nje ambao kwasasa wameanza kukipa mkono wa kwa heri baada ya kugundua chama hicho hakina uwezo wa kuongoza dola ya Tanzania.

Kutokana na Chadema kukosa mvuto na uungwaji mkono mashabiki na wapenzi wake wameanza kukosa updates za uhakika kutoka arumeru east kutokana na kushuku ama kupoteza umaarufu wa mgombea wao Mr Nassary kila kukicha. Chanzo kikubwa cha kudorora kwa kampeni hizo ni ukata unachokikabili chama cha Chadema na ufisadi wa ruzuku unaofanywa na viongozi wakuu wa chama hicho.

Kwapamoja tuiunge mkono CCM kuendelea kutawala nchi hii kwa maendeleo ya Watanzania na tuepukana na vibaraka wa ukoloni Chadema ambao wanafanya siasa kwa maslahi yao binafsi.

Kwa mwaka 2012 Wanaarumeru watakuwa wakwanza kuwakataa chadema na ukoloni mambo leo wao

Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake

ukoloni mambo leo up kwan hadi sasa tunao na chanzo ni ccm.we kwel mnafiki unaposema maslahi binafis wakati sumari kachaguliwa kupunguza machungu ya babake.kwa hili jajipange upya umechemka
 
Ninavyoichukia CCM ni kama mtu atayechukua mke wangu!!!! Nashukuru watu waneshashitukia CCM na kujua ndiyo mchawi namba moja.
 
Huyu pimbi vp,nadhani millya huyo maana lowassa kamwambia sioi asiposhinda basi asimkaribie.usidanganye umma mwenyewe hapa nipo shangarai meru
 
Wana-Arumeru wamesema "hawata kuchagua wahuni", wanaohamasisha maandamano
 
huyu naisi ni Ephraim Kibonde ha ha ha ha ha ha , KWANA KABISA HAKUNA UPDATE yoyote iliyopo hapo aidi ya Bla bla tu, alafu upuui kama huu, ni sasa na kujifunika uso ukadhani unajificha usionekane, we nadhani una mtindio wa ubongo, may be ubongo wako unakanusha, kila unachoiona unaona UPSIDE-DOWN
 
Wakuu, niko Arumeru kikazi tangu kampeni zianze!

Tukiacha siasa uchwara CCM inahitaji nguvu za giza kushinda uchaguzi huu! Sina haja ya kuwaficha hii ndio hali halisi Jana nilipata taarifa za mkutano wa kampeni wa CCM uliokuwa ufanyike eneo moja maarufu kama barabara nne (4 ways) kata ya Nkoanrua, nilienda nikakuta watu watatu tu, baadae kidogo wakaongezeka na kufika saba, ilibidi mkutano uahirishwe! Nimeshuhudia sijaambiwa!

Juzi kulikuwa na mkutano wa CCM kata hiyo hiyo maeneo ya moivaro (sikuweza kufika) niliambiwa walifika watu wasiozidi 30, nikatajiwa kwa majina huku vijana wakiwa 12! Mkutano huo ulitanguliwa na matangazo kama kawaida yakitolewa kwagari moja dogo likiwa limetanguliwa na pikipiki wakaenda eneo la soko la ndizi ulikofanyikia mkutano wa CDM jumapili iliopita. Walipofika tu, majira ya saa nne hivi, akina mama wafanyabiashara wa mbogamboga sokoni wakapiga ukunga wa wezi haoooo! mara ikaja gari ya polisi wakawahoji wakasema CCM wanakuja kutufanyia fujo sokoni na kutunyang'anya pesa zetu, tumewachoka hatuwataki. polisi waliishia kumchukua mama mmoja akatoe maelezo na kisha kurejea baada ya mda mfupi!

Hiyo ndio hali halisi! wadau msitegemee TBC1 na gazeti la uhuru kusoma upepo!

Pia mods naomba uwaelekeze kwa upendo madogo wanao-derive formula humu, bila shaka sio jukwaa lao. Si unajua tena madogo wako likizo! Aah shule nazo zifungue waishie zao!

Naomba kuwasilisha!
Kwa mtu anayefuatilia hotuba za hao wapiga debe wa CCM, hawezi kuhitaji huu ushahidi. Nafikiri hata wao CCM wanajua kuwa wameshashindwa, ndio maana wanishia kuporomosha matus.i majukwaani badala hata ya kumnadi mgombea wao. Chukulia mfano mzee Wasira ametumia zaidi ya siku tatu kujadili Upadri wa Dr. Slaa.
 
Wakuu, niko Arumeru kikazi tangu kampeni zianze!

Tukiacha siasa uchwara CCM inahitaji nguvu za giza kushinda uchaguzi huu! Sina haja ya kuwaficha hii ndio hali halisi Jana nilipata taarifa za mkutano wa kampeni wa CCM uliokuwa ufanyike eneo moja maarufu kama barabara nne (4 ways) kata ya Nkoanrua, nilienda nikakuta watu watatu tu, baadae kidogo wakaongezeka na kufika saba, ilibidi mkutano uahirishwe! Nimeshuhudia sijaambiwa!

Juzi kulikuwa na mkutano wa CCM kata hiyo hiyo maeneo ya moivaro (sikuweza kufika) niliambiwa walifika watu wasiozidi 30, nikatajiwa kwa majina huku vijana wakiwa 12! Mkutano huo ulitanguliwa na matangazo kama kawaida yakitolewa kwagari moja dogo likiwa limetanguliwa na pikipiki wakaenda eneo la soko la ndizi ulikofanyikia mkutano wa CDM jumapili iliopita. Walipofika tu, majira ya saa nne hivi, akina mama wafanyabiashara wa mbogamboga sokoni wakapiga ukunga wa wezi haoooo! mara ikaja gari ya polisi wakawahoji wakasema CCM wanakuja kutufanyia fujo sokoni na kutunyang'anya pesa zetu, tumewachoka hatuwataki. polisi waliishia kumchukua mama mmoja akatoe maelezo na kisha kurejea baada ya mda mfupi!

Hiyo ndio hali halisi! wadau msitegemee TBC1 na gazeti la uhuru kusoma upepo!

Pia mods naomba uwaelekeze kwa upendo madogo wanao-derive formula humu, bila shaka sio jukwaa lao. Si unajua tena madogo wako likizo! Aah shule nazo zifungue wai

Tunakuomba uendelee kutuapdate, na je vijana watapiga kura?wasiwasi wetu ndo huo tuu,wazee vijijini je nanasomeka?
 
Back
Top Bottom