CHIEF PRIEST
JF-Expert Member
- Dec 13, 2021
- 7,955
- 14,593
Mashudu tu kama ya Lucas Mwashambwa ,au ndiyo umekuja kivingine?WANACCM NDANI YA CCM
Makada wa CCM ndani ya serikali,
Kila mmoja amuwazie mwenzake mema.
Tuache kuchuliana powa.
Powa powa sio powa.
Hakika hatutampenda Mungu bila ya kuwapenda waliotuwezesha kuwa na maisha tuliyonayo.
CHARITY BEGINS AT HOME. Tuondoe umaskini kwa wanaccm kwanza ili tuwaondolee Watanzania umaskini.
Nakumbuka tarehe 23/Novemba/2021
Mbunge na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani Tanzania, Comrade Hamisi Hamza Chiro, alianza kwa kusema:
"Mabibi na Mabwana na Wanahabari,
Asalaam Aleikhum
Bwana Yesu Asifiwe,
Ninawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
Kwanza kabla ya yote, nichukuwe fursa hii nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa ametujaalia tumekutana hapa tukiwa wazima wa afya."
Mwisho wa kunukuu.
Comrade Steave Biko, mpinga maovu aliyeuliwa kikatili huko Afrika Kusini tarehe 12/Septemba/1977 katika mahabusu ya polisi ya Makaburu aliwahi kusema:
"It is better to die for an idea that will live than to die for an idea that will die."
"I am going to be me as I am. And you can beat me or jail me or even kill me but I'm not going to be what you want me to be."
Mwisho wa kunukuu.
Nakumbuka tarehe 25/Agosti/2021
Padre Dkt Faustine Kamugisha wa Parokia ya Minziro-Bukoba aliwahi kusema:
"Na mimi naongea kwa sababu nina matumaini kwamba haya yote yatawasaidia."
"Na wewe unayeyasikiliza una matumaini kwamba yatakusaidia."
Mwisho wa kunukuu.
Tukiisoma Kitabu cha Maandiko Matakatifu ya Mwenyezi Mungu kiitwacho Fadhila za A'maal, ukurasa wa 166, maandiko yanasema:
"Rasulullahi Swallallahu Alaihi Wasallam amesema: Kuweni wanyenyekevu sana na wenye heshima kwa watu ambao kutoka kwao mnapata elimu."
Mwisho wa kunukuu.
Wanaccm na Watanzania wenzangu, chama chetu CCM ngazi za shina, tawi, kata, na majimbo hali ya kimionekano sio nzuri na hii ni aibu kwa wanaccm wote bila ya kujali vyeo vyetu.
Na huu sio utu, ni kinyume na matakwa ya ilani ya CCM 2020 - 2025. Posho za baadhi ya viongozi ngazi hizo za CCM huku chini ni vichekesho.
Tubadilike kifikra.
Nakumbuka tarehe 05/Desemba/2021
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan akifungua barabara ya Morocco - Mwenge Dar alisema:
"Niwaombe sana na wananchi tubadilike kifikra, tubadilike kimatendo."
Mwisho wa kunukuu.
Ofisi za CCM ngazi za shina, tawi, kata, na jimbo hazina kumbi za mikutano, hakuna ofisi za kutosha kwa viongozi wa ngazi hizo, hakuna posho, na miradi mingi ya CCM ilianzia huku chini ila fedha nyingi inapaa juu. Mrejesho wa fedha hizo haukidhi mahitaji ya wanaccm wa huku chini.
Ukiangalia ngazi za wilaya, mkoa, na taifa hali ni nzuri sana. Tujenge daraja la kutuunganisha wote hali zetu ili tusichukuliane powa walau tujenge vyoo tu. Wanaccm wanaumia ila hawasemi. Baadaye tunawalaumu wajumbe kumbe ni sisi baadhi ya wanaccm tunawachukulia powa wenzetu kwa ukimya wao.
Nakumbuka Novemba 2020
Dkt Hassan Abbass aliyekuwa msemaji mkuu wa serikali akiwa katibu mkuu wa wizara yenye dhamana na sanaa aliwahi kusema:
"Kama wenzetu wamejengewa mradi la Rufiji kule la matrillioni, hivi na sisi kwenye sanaa huku hatuna kitu fulani hivi amazing cha billion kadhaa tukafanyiwa! Mbona wanatuchukulia powa hawa watu."
"Sasa inawezekana tulikuwa tunachukuliwa powa kwa sababu na sisi wenyewe tuko powa. Ehee, ukiwa umepowa watu wanakupoza tu, unaona bhana, inakuwa simple tu."
Mwisho wa kunukuu.
Nakumbuka tarehe 04/Novemba/2016
Hayati Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wahariri wa habari alisema:
"Tuna wajibu wa kwenda pamoja, sisi wote ni wamoja tuna haki sawa mbele ya Mwenyezi Mungu wetu."
Mwisho wa kunukuu.
Wanaccm na Watanzania wenzangu, miongoni mwetu kuna baadhi hawaamini kabisa kama na sisi wanaccm wa ngazi hizi za chini tunahitaji kutendewa haki na usawa kwenye mambo ya kimsingi ya kibinadamu.
Nakumbuka tarehe 26/Desemba/2021
Comrade Job Yustino Ndugai, Spika wa Bunge alisema:
"Ohoo unajua sisi, tunadharaulika tunafany... Usidharaulike kwa nini?! Kwani una nini cha kukufanya uheshimike? Watu wanaheshimikaga tu hivi hivi?!"
"Haiwezekani, unaheshimika kwa kazi, kwa achievable, huna cha kuonyesha huheshimiki."
"Hii maneno ya shuleni binadamu wote ni sawa ile ni theory ya kupasi mtihani, ile ni ya kufaulu mtihani wa Wizara ya Elimu."
"Binadamu ni sawa tangu mwaka gani?! Tangu lini?"
Mwisho wa kunukuu.
Tusome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ukurasa wa 20 Ibara 12 (1)(2), Ibara 13(1)(4)(5), Ibara 26(1)(2) bila kuacha Ibara 9(a)(b)(f).
Katiba ya CCM 1977 toleo 2020 ukurasa wa 01 Ibara 04 (1)(2).
Azimio la Arusha ukurasa wa 01 kifungu (a)(b).
Nakumbuka tarehe 15/Desemba/2021
Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa wadau wa kujadili hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini alisema:
"Unapovunja sheria, unajivunjia heshima, na serikali inashindwa kukuheshimu."
"Naomba tufanye kazi kwa kuheshimu sheria."
"Hakuna mbora wetu mbele ya sheria."
"Mbora wetu ni yule anayefuata sheria."
Mwisho wa kunukuu.
Nakumbuka tarehe 27/12/2021
Akihojiwa na ITV, Mheshimiwa IGP Simon Nyakoro Sirro alisema:
"Unajua Mheshimiwa Rais (Samia) akisha zungumza ni maelekezo. Na mimi nayafanyia kazi maelekezo yake, nafuatilia."
Tusome Ilani ya CCM 2020 ukurasa wa 161 - 168 bila kuacha ukurasa wa 01 Ibara 04.
Nitoe wito kwa viongozi wa CCM ngazi za juu kutuangalia sisi tulioko huku chini kwa jicho la huruma na upendo huku tukijikumbusha ya kuwa sisi ni mwili mmoja.
Tukisoma Kitabu cha Awamu ya TATU ya Mradi wa Kukiimarisha Chama ukurasa wa 05, maandiko yanasema:
"Katika kikao chake cha Desemba 1985, Halmashauri Kuu ya Taifa ilianzisha mradi wa kwanza wa kuimarisha chama baada ya kubaini kuwa chama kilikuwa kibovu hasa katika ngazi zake za mwanzo."
Mwisho wa kunukuu.
Nakumbuka tarehe 04/12/2021
Mheshimiwa Salvatory Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi alisema:
"Hakuna mwanadamu ambaye Mungu kamnyima kila kitu, wala hakuna aliyepewa kila kitu. Wote tumepewa kadri ya uwezo wetu. Na hivyo ni wajibu wetu na hasa viongozi wetu kutuunganisha sote kwa pamoja kushirikiana katika kuujenga ufalme wa Mungu."
Mwisho wa kunukuu.
Tukisoma Kitabu cha Sera ya CCM ya Kujitegemea Kimapato na Kiuchumi ukurasa wa 03, maandiko yanasema:
"Katika chama hiki tokea 2000 yamekuwepo maamuzi mbali mbali ya vikao vya juu vya chama kuanzia sekretarieti, kamati kuu, halmashauri kuu ya taifa na hata mkutano mkuu wa taifa kuhusu chama kujitegemea kimapato na kiuchumi. Changamoto kubwa imekuwa ni utekelezaji wa maamuzi hayo."
Mwisho wa kunukuu.
Ilani yetu ya CCM imetamka neno ubunifu mara nyingi ila hakuna mtu aliye tayari kusaidia kwa lolote ili kubadili mielekeo na mitazamo ya kimaskini ndani ya CCM.
Mwenye uwezo naomba anipeleke kwa Mheshimiwa Sam