Uongozi wa Wilaya ya Kigamboni wawavua ukuu wa Shule walimu shule zilizoshika mkia NECTA

View attachment 466096 [HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]:Uongozi wa WILAYA ya Kigamboni umetangaza kuwavua nafasi za ukuu wa shule wakuu wa shule za Kidete na Somangila Day baada ya shule hizo kufanya vibaya zaidi katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2016

Chanzo:ITV
Walimu wakuu peke yake sio sababu ya watoto kufeli jamii tunazo ishi zikoje mazingira ya shule yakoje uelewa wa walimu ukoje
 
bc36ee589e789ea1463056b2a6469bfa.jpg


Source: ITV (Breaking news)
 
Kuna waalimu wamestaafu, wameacha, wamefariki, wamefukuzwa lakini hatujaajiri leo mwaka wa pili, hapo hapo wanafunzi wanaongezeka. Jamani
 
Nchi imevamiwa anayekupa ukuu ni mwingine,anayekuvua ukuu ni mtu mwingine ambaye hata ukuu ulioupata hakukupa yeye.
 
Wazazi, wanafunzi, waalimu na wadau wote wa sekta nzima ya elimu wahusishwe katika kutafuta suluhu ya hili tatizo.
 
yamekuwa hayotena, nilijua tuu kwa matokeo haya kwa dsm baadhi ya walimu lazima wawajibike like you see
 
Kama kawaida, maamuzi ya kukurupuka na zimamoto.. Nilidhani wangeitisha kikao cha wadau na wanaohusika na hizo shule, ikiwa ni pamoja na wanafunzi ili wajue sababu zilizopelekea shule hizo kufanya vibaya..

Jana nimesikia habari Radio One, walimu wanafundisha kwa uzoefu kwa sababu vitabu vya kufundishia bado havijafika toka huko vinakochapwa.. Maajabu haya..
 
Hilo siyo suluhisho la kudumu mazingira bora ya Mwalimu na Motisha kwa Walimu miundominu na mazingira ya shule mazuri ndio vitakavyoinua elimu yetu in short kabla awajawatumbua walimu wakuu waende FEZA kuangalia mazingira yao ya utoaji elimu kabla awajawatumbua.
 
Back
Top Bottom