Uongo wa wazee wa zamani wa Tanzania kuhusu mpira

Gunner Shooter

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
4,972
8,334
Hivi nyie wazee huwa mnatuchukuliaje vijana utakuta mzee anasifia wachezaji wa zamani unaweza kusema hao wachezaji waliipa Tanzania ubingwa wa dunia yaani katika vitu vinanikera mizee kusifia magarasa ya zamani eti zamani kulikuwa na mpira sio Sasa.

Hiyo zamani yenyewe waulize hata kombe la takataka kama afcon washawahi kuvuka hata makundi jibu ooh kulikuwa hakuna pesa. Sasa pesa na uwanjani wanaume 22 wapi na wapi, wazee acheni uongo bhana hamna mpira wowote mlikuwa mnakimbizana tu kama mnafukuza nguruwe tafuteni uongo mwingine huu tumewastukia na hakuna laana mtayotupa sababu mnasema uongo halafu mwisho kwanini Kila mzee nikimuuliza alikua anakua wa ngapi shuleni anasema alikua wa kwanza mpaka anamaliza Sasa wamwisho alikua nani .
 
Hivi nyie wazee hua mnatuchukuliaje vijana utakuta mzee anasifia wachezaji wa zamani unaweza kusema hao wachezaji waliipa tanzania ubingwa wa dunia yaani katika vitu vinanikera mizee kusifia magarasa ya zamani eti zamani kulikua na mpira sio Sasa hiyo zamani yenyewe waulize hata kombe la takataka kama afcon washawahi kuvuka hata makundi jibu ooh kulikua hakuna pesa Sasa pesa na uwanjani wanaume 22 wapi na wapi wazee acheni uongo bhana hamna mpira wowote mlikua mnakimbizana tu kama mnafukuza nguruwe tafteni uongo mwingine huu tumewastukia na hakuna laana mtayotupa sababu mnasema uongo
Wazee wa zamani huwa wanapenda kuongeza chumvi kwenye story zozote zile, waelewe tu.
 
Hiyo zamani yenyewe waulize hata kombe la takataka kama afcon washawahi kuvuka hata makundi jibu ooh kulikuwa hakuna pesa. Sasa pesa na uwanjani wanaume 22 wapi na wapi, wazee acheni uongo bhana

Kama mpaka leo hujui pesa ina nguvu kiasi gani kwenye mchezo wa mpira wa miguu basi hujui mpira.
 
Zamani mbungi ilikuwa inavutia kutazama si Tanzania tu, hata huko duniani, si mpira kwa ujumla bali wachezaji wenye kutegemea vipaji asili na si kutengenezwa "maabara za mpira"...

Lakini inapotajwa zamani si zamani mpira ukiwa unaanza bali kipindi ni miaka ya 70 mwishoni, 80 hadi 90 hapo...

Mfano kwa bongo kuna familia kama ya Manara ambayo wote walikipiga ughaibuni...
 
Back
Top Bottom