Kuelekea 2025 Ungepata nafasi ya kuuliza swali kwenye tume ya uchaguzi ungeuliza swali gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mawele

Senior Member
Jul 25, 2023
119
314
Ungepata nafasi ya kuuliza swali kwenye tume ya uchaguzi ungeuliz swali gani?

Huenda wengi tuko na maswali ambayo tungehitaji kuyauliz kwenye tume ya uchguzi ila hatujui tunayauliza wapi.

Basi ni vyema tutumie uzi huu kuyauliza hyo maswali, mimi nawaomba Mods wayakusanyanye wawape tume ya uchaguzi watuletee majibu hapa jukwaani ili kila mmoja pate jibu l swali lake. Ila kama inawezekana Tume ya uchaguzi waje hapa jukwaani wtujibu, tujadili pamoja watupe na tuwape mawzo yetu.

Kila mtu aulize maswali yake hapa, Mods tunaomba myakusanye.

1724891520086.jpeg
Pia soma:Hii ni yetu sote,ni lazima tuungane kwa maslahi ya mitaa yetu
 
1. Kwa nini Wakurugenzi wa Halmashauri wanaendelea kuwa wasimamizi wa uchaguzi na wakati Mahakama ya Afrika ilishatoa hukumu ya kuwaondoa? Maana hao ni wateule wa Mwenyekiti wa chama tawala!

2. Kwa nini matokeo ya Rais hayapingwi mahakamani?

3. Kwa nini mshindi wa kiti cha Urais asipatikane kwa ushindi wa zaidi ya 50%, ili kuondokana na huu mfumo wa sasa?

4. Viti maalum vya udiwani na vile vya ubunge vina tija gani kwenye dunia ya sasa?

5. Kwa nini baadhi ya wagombea wa nafasi ya ubunge hutangazwa kuwa washindi kupitia njia ya kupita bila kupingwa? Na kama mgombea amekosa mpinzani wa kushindana naye, kwa nini asipigiwe kura ya ndiyo au hapana?
 
Ningewaulizaa hv n kweli tokaa nchi ipate uhuru n kweli n CCM tu wanashindaga kiti Cha urais hkn chama Cha upinzan kinashinda kihalali miaka Yate ya uchaguzi!!!!

Kama taifa tunasafari ndefu sanaa
 
Nimeyapenda maswali haya, safi sana
 
Ningewaulizaa hv n kweli tokaa nchi ipate uhuru n kweli n CCM tu wanashindaga kiti Cha urais hkn chama Cha upinzan kinashinda kihalali miaka Yate ya uchaguzi!!!!

Kama taifa tunasafari ndefu sanaa
Kwa kweli wajibu hili swali, hata mimi najiuliza pia
 
Hapo hakuna swali hata moja linaweza kujibiwa na tume ya uchaguzi, maswali yako yanaihusu serikali na ndio yenye majibu.
 
Ungepata nafasi ya kuuliza swali kwenye tume ya uchaguzi ungeuliz swali gani?

Huenda wengi tuko na maswali ambayo tungehitaji kuyauliz kwenye tume ya uchguzi ila hatujui tunayauliza wapi.

Basi ni vyema tutumie uzi huu kuyauliza hyo maswali, mimi nawaomba Mods wayakusanyanye wawape tume ya uchaguzi watuletee majibu hapa jukwaani ili kila mmoja pate jibu l swali lake. Ila kama inawezekana Tume ya uchaguzi waje hapa jukwaani wtujibu, tujadili pamoja watupe na tuwape mawzo yetu.

Kila mtu aulize maswali yake hapa, Mods tunaomba myakusanye.

Hapo kabla iliitwa Tume ya uchaguzi. Kuanzia hapa karibuni inaitwa Tume huru ya uchaguzi. Wanieleze huo uhuru wao umepatikanaje? Swali langu linatokana na ukweli kwamba mwenyekiti, wajumbe na watendaji wa tume ni wateule wa mwenyekiti wa ccm.
 
Back
Top Bottom