Unawezaje kubadilisha maisha yako Daima??

Staphylococcus Aureus

JF-Expert Member
Jan 18, 2024
1,744
2,652
Wakuu nina swali??

LEO KATIKA PITA PITA ZANGU
Nimekutana mtandao (Whatsapp status) na dogo mmoja tulikutana ofice moja hapa jijini wakat nasajili campuni yetu.Kwakua yeye alikua very educated kwene haya maswala niliomba namba yake awe ananisaidia maana wao ndo walikua wanamalizia usajili namm nilikua naanza.

Sasa imepita kama miez mitatu leo nimeview status yake nikakuta amepost demu wake mzuri mzuri namm na umalaya wangu nikaanza kumtania mwanangu unamademu wakali uwe unanilink aisee

Maana ana postigi watoto wakali sana tofauti tofauti. Kwa ufuska wangu nikajua anawala au ana date nao.
Cha kushangaza aliniambia

Bro mimi hawa si mademu zangu ni rafiki wa chuo wengine ndugu zangu mi nina demu mmoja tu tangu niko msingi na ndo nitakuja kumuoa”

Alimaliza kuniambia… aisee sikuamini nikajaribu kumdadisi akanijibu

“Wanawake ni wale wale ile kitu ni ile ile hamna haja ya kuhangaika na starehe ya muda mfupi maana hata kama kitu kitamu vipi kitaisha tu,,,,,,
Pia kuna hii post

“No matter how the food
might be delicious, it must be
finished and you remain with
empty and dirty plate. So, don't
allow the pleasures of this
world to consume your soul.
Everything on this world must perish


Hii imenifanya nikumbuke maisha yangu ya uasherati”
Nimetembea na mademu wengi lakini ukiniuliza faida hata moja hamna zaidi nimekua siwezi kutulia kwene mahusiano , nimepata matatzio makubwa yaliyoharibu afya yangu na makovu ya mwili

Ni mwaka 2013 nilikua nimekaa room ya watu wanne chuo ambapo nilinunua smartphone kwa mara ya kwanza.
Ilikua ni tecno nadhan ndo zilikua smarphone za kwanza kwanza kwene ulimwengu wa smartphone kwa techno kwa tz. Darasan kwetu walikua nazo watu kama kumi tu huku wengine wakisongesha na viswaswadi….
Ni katika simu hii ya smartphone nilijikuta nimekula mademu wengi mtandaoni kwani ilikua ni rahisi kumtongoza mwanamke usiyejuana nae kwa kuangalia tu location yake.
Hivo ililua inanipa urahisi wakufanya ufuska.

10 years later nimejua ni yale maamuzi ya siku moja ndio yalibadirisha maisha yangu daima hadi leo kupenda “Fast food”.. au dada poa.

Siwezi ilaumu simu ila nalaumu hiyo ideology niliyoishikiria iliyonifanya nikawa mtu wa hivo na kujikuta nataman kulala na kila mwanamke niliyeweza kumfikia.
Kwa kua sikua napenda mahusiano na usiri hivo sikua nadate au na wanawake maeneo ya chuo. Nilikua nachek mtandaoni na kuwapanga kila nilioohitaji mwisho ikawa tabia.
TOO BAD……..


KUNA JAMAA NILIMUONA BBC
Jamaa anaitwa “John Francis“ alikaa miaka 17 bila kuongea.Na sababu ilikua alijifunza watu hawataki kusikiliza wala hawatak kujua akaamua kukaa kimya .

Ukitaka hii story google ipo moja tu utamuona na kusoma zaidi.

NINI KINAFANYA WATU WACHUKUE UAMUZI HUU AU ITIKADI FULANI
kuchukua maamuzi mazito au yatayobadilisha maisha yako milele si jambo jepesi wala si jambo la kusema nimeamua.
Uamuzi huu hufikiwa kutokana na vitu kadhaa

1.Matatizo makubwa yanayokupa funzo la maisha

2.Aina fulan ya imani ya muda mrefu ya mtu

3.Sababu muhimu


NINI NAHITAJI
Nahitaji nipate mlengo fulani au falsafa ya maisha ambayo itakua ni chachu ya kubadili maisha yangu.Hapa siongelei dini za kina modi au wagalatia No

Falsafa kama za marastafarai, au itikadi fulan nzito nzito ambazo zitafanya niayaone maisha tofauti kabisa.

Itikadi zitazoniingia na kupelekea kubadili maisha mazima.
zinaweza kua kuhusu maisha, lifestyle, hela, wanawake , nk ambazo zinaleta impact kumbwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom