Unaweza pata mafanikio kwa kumfukuza mtu kazi?

Roho ya Mwanadamu inajenga mazoea, ukiwakuta wezi ukaanza kuiba ndo umeshakuwa mwizi, kutoka hapo ni neema ya Mungu. Pia mtu safi akiona nguvu ya usafi wake haithaminiwi ana amua naye kuwa mbaya, hivyo kuwakukuza watu kwa sababu ya uovu wao bila kuwaonea, nimoja ya njia ya kuongeza uwajibikaji kwa wanao baki.

Na akiiendelea hivyohivyo kutakuawa na matokeo mazuri sana. nchi zote zenye maendeleo kuna displinekali kaizini, ukifanya kosa ni adhabu hapo hapo hata kifo, angalia China, Rwanda, nk. ukokosea tu hapohapo.

Taasisi kama jeshi pia displine ni kubwa kwa sababu hiyo afanyakazi wake ni mguu pande au sawa na si zaidi ya hapo. usalama wa taifa ukimess tu wakati mwingine hata kifo.

Hivyo bila kuwatimua hutuwezi kujenga displine.
 
Sangala watafukuzwa lini maana ameanza na dagaa, kafuata vibua NA sasa amefukuza kambale. Nangoja akifukuza sangala, akaenda baharini akatimua papa na kisha nyangumi ndio nitaamini kuwa Magufuli kaamua kazi. Japo akifukuza nyangumi wawili tu nchi itamegeka vipande, pia ngalawa yake inaweza kuzama.

Natania tu jamani nisije kumbwa NA cyber crime bure.
 
Nawaskia watu wengi kwa maelfu wakubwa kwa wadogo wakisifia timuatimua ya Magufuli na wenzie. Hivi jamani ni nani kawadanganya kuwa kufukuza mtu kazi ni mafanikio?

Hivi unaweza pata mafanikio kwa kumfukuza mtu kazi? Mimi nadhani tungesubiri tuone matokeo kwani timua timua ndio ilikuwa fasheni ya Mwakyembe na Sitta walipofanya kazi kunako wizara ya uchukuzi hata hivyo tumeshuhudia maovu ya kutisha.

Je, ile fukuza fukuza ililenga nini? Ni kwa hoja hii nashauri tusubiri tuone ikiwa Magufuli ataweza kuleta mfumo madhubuti utakaodhibiti kabisa wizi na upotevu wa mapato hapo bandarini na kwingneko na si kushabikia tu.

kama mtu anaharibu kazi unategemea anaweza kuchangia kuleta mafanikio?the best solution ni kumbadili hili halihitaji hata kwenda shule kulielewa labda kama umeamua kuendekeza "politiki"
 
- Ni kawaida sana kwa nchi zilizondelea Utawala mpya unapoingia utawala wa zamani unaondoka na wote, so ni kawaida it does not matter about anything ila mabadiliko ni mabadiliko wa zamani wote wanaondoka wanakuja wapya.

le Mutuz

Kwa hiyo hata wale wa TPA ni suala la kuondoa wa zamani?
 
Mwizi na mzembe hawezi kuvumiliwa aendelee kuitia nchi hasara eti kwa sababu kufukuza hakuna tija.arguments za namna hii ni ujuha na upumbavu mkubwa
 
Ila kuna watu wanaandika vitu inaweza sema ata darasa la saba hajapita.....we ungetaka afanye nn km viongoz wa hzo secta wamefanya ujinga miaka yote hyo
 
Nawaskia watu wengi kwa maelfu wakubwa kwa wadogo wakisifia timuatimua ya Magufuli na wenzie. Hivi jamani ni nani kawadanganya kuwa kufukuza mtu kazi ni mafanikio?

Hivi unaweza pata mafanikio kwa kumfukuza mtu kazi? Mimi nadhani tungesubiri tuone matokeo kwani timua timua ndio ilikuwa fasheni ya Mwakyembe na Sitta walipofanya kazi kunako wizara ya uchukuzi hata hivyo tumeshuhudia maovu ya kutisha.

Je, ile fukuza fukuza ililenga nini? Ni kwa hoja hii nashauri tusubiri tuone ikiwa Magufuli ataweza kuleta mfumo madhubuti utakaodhibiti kabisa wizi na upotevu wa mapato hapo bandarini na kwingneko na si kushabikia tu.

Mnaisoma namba. Mlisema CCM inalea mafisadi. Magufuli kaanza kutimua watu (na kila anayetimuliwa atafikishwa Mahakama ya Ufisadi) mnaanza kuhoji kuhusu mnachoita 'timua timua.'

And by the way hujalazimishwa kushabikia. Afterall, si rahisi kwa jipu kushabikia utumbuaji majipu.
 
Kuna mazingira suala la kufukuza mtu kazi haliepukiki.Huwezi kuendelea na mtu mwizi au goigoi.Na tena aongeze spidi ya kutimua kwani taasisi/mashirika/ idara nyingi zimeoza kiutendaji.Na kama ningekua mimi wakuu wa TTCL,TBS,ATC,TCAA na TBC wangekwishatimuliwa kazi.
 
Back
Top Bottom