Unatumia njia gani kulinda data/taarifa zako binafsi kwenye simu yako?

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
368
461
Taarifa binafsi ni taarifa ambayo inaweza kukutambulisha wewe, mf. Picha, jina, kitambulisho, kadi ya benki, nk. Mfano, unaponda kujindikisha kwa mlinzi ili kuaingia kwenye ofisi fulani ukaacha jina lako, namba ya simu, pamoja na email, hizi ni taarifa zako binafsi, mtu zimefungamanishwa na wewe na zinaweza kutoa utambulisho na pengine kuwa njia ya kupata taarifa nyingine zaidi kuhusu wewe.

Taarifa zako zinaweza kutumiwa vipi vibaya? Angalia mfano huu:

Wewe ni mwanafuni wa kidato cha sita kutota shule X, mara baada tu ya mahafali unaanza kupokea jumbe za matangazo kuhusu vyuo mbalimbali, wakitaja jina lako pamoja kozi unazoweza kusoma kwenye vyuo vyao! Kwa wale ambao wazazi hawajawanunulia simu jumbe hizi zinatumwa kwa mzazi. Unashangaa wamepata wapi taarifa hizi mpaka wanataja jina lako? Hii ni kwasababu kuna mtu ameuza taarifa hii na katika mfano huo ni shule. Shule hizo zinakuwa zinafaidika kwa njia ya fedha sababu taarifa hizo hazitolewi bure zinanunuliwa.

Mfano wa pili, wewe hujui kubeti na wala hujawahi kufikiria kubeti lakini huishi kupokea ujumbe kutoka kampuni za kubeti, je wamepataje namba yako na hujawapa? Ukiwauliza watakwambia tumenda kwenye kampuni Y wametuuzia!

Sasa fikiria ikiwa umefanya uzembe mtu akapata zaidi ya namba ya simu, mtu akapata password yako ya MPesa au Tigo Pesa na unampunga wa kodi kwa mfano, madhara yake yatakuwa makubwa si ndio, ukizingatia usawa huu. Au vipi umezembea mtu akapata picha yako halafu ukajikuta kwenye mstimu sehemu jamaa huyu ni tapeli anatafutwa na polisi? Au umegombana na mtu anachukua namba yako anaenda kuweka kwenye tangazo la mganga au wanaojiunga na freemason, hapo vipi?

Unaweza usiathirike kifedha lakini lazima upate usumbufu wa mpaka kubadilisha namba na hiyo ikaenda kuharibu mambo mengine hasa ikiwa namba hiyo ndio inayotumika kwenye biashara zako nk.

Maswali ya kujiuliza;

Ukiwa unaambiwa ujiandikishe taarifa zako sehemu huwa unauliza zinatumiwa kwaajili gani?

Simu yako ina password ya imara au mradi tu umetimizawajibu (kuweka password kwenye simu yako ni takwa kisheria wala sio ombi) tumia namba, herufi na alama mbalimbali kutengeneza password nzuri, Wengine hutengeneza hata sentesi nzima.

Huwa unabonyeza link ovyo mtandaoni bila kujiridhisha mradi umeona umeambiwa umeshinda iPhone bonyeza kuipata? hivyo usibonyeze zinaweza sababisha kuhakiwa na kufanya taarifa zako zikasambaa bila hidhini yako.

Password yako ya MPesa, TigoPesa ni siri yako au umeshea na mpenzi wako sabababu mapenzi ni motomoto?
Unafanya juhudi kulinda taarifa zako usihakiwe/kudukuliwa kizembe au ndio unamuachia Mungu? Na ni vyema pin zako zisiwe tarehe yako ya kuzaliwa ilikurahisha hacker kukutapeli.

Vipi kuhusu watoto wako, umewafungulia account na kushea picha zao ovyoovyo? Ikiwa mtoto ni mkubwa na anatumia mtandao, unafanya nini kumlinda?

Kwenu Wakuu
 
Back
Top Bottom