Unapompa Mpinzani Ukuu wa Mkoa, Sehemu Ambayo Unapingwa, Nini Tafsiri Yake?

Wote watanzania, hakuna upinzani Tanzania.

Wanatofautiana majina ya vyama tu lengo lao ni moja tu nchi ya viwanda na uchumi wa kati 2025

Sio kwa jinsi serikali hiii inavyochukulia, wao Wapinzani ni maadui na hawastahili hata kuwepo.
 
Kama naiona future ya ACT matatani
Mkuu labda tuna mawazo tofauti. Mimi naona ACT-w wameweza kupenya serikalini haya ni mafanikio ya kimkakati. Chama chochote cha siasa kina lengo la kushika dola, leo ACT-w wanashika dola ndani ya Kilimanjaro na wana Katibu mkuu serikalini. Mghwira na Mkumbo wanajulikana na viongozi wa ngazi za juu kwenye upinzani na leo wanashika dola. Haya mambo hufanywa kabla ya uteuzi. Wanakaa wanazungumza halafu wanamchukua Mweyekiti anajiunga na CCM ila bado hajahama ACT. Huku ni sawa na kuoa mapacha nyumba inakuwa na amani kwa sababu kabla ya kuwaoa wao walishaazimia lazima waolewe na mwanaume mmoja.
Kwa mtindo huu lazima Dr. Magu atawale 2 terms +.
 
Nalo neno mkuu
 
.io inaitwa devide and rule ni kuhakikisha kuwa upinzani unakosa nguvu Kwa kugawa nakujinyakulia wale wenye nguvu na kuwaweka chini yako kama mkulu anavyofanya..lengo ni moja kuuwa au kupunguza upinzani
 
Yalisemwa tangu zamani kuwa ACT ni tawi la CCM lililoanzishwa kwa lengo la kuihujumu CHDEMA,CCM walikanusha kwa mapovu mengi kama mapovu ya sabuni ya Omo,Mh Magufuli amethibitisha kwa vitendo kuwa yale yaliokuwa yanasemwa na wapinzani ni ya kweli kwa kumteua Ana kuwa Mkuu wa mkoa nafasi ambayo mpaka uteuliwa ni pale tu ambapo inakuwa imethibitika kuwa wewe ni kada muaminifu wa CCM ambaye utakuwa tayari kuipigania CCM kwa hali zote ikiwa ni pamoja na kuiwezesha CCM kushinda kwa kura za wizi.
 
Wana jamvi, leo Rais wetu, kamteua Mwenyekiti na aliyekuwa Mgombea wa urais wa ACT kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro...Tukumbuke kuwa mkoa huu ni upinzani kwa asilimia kubwa,na aliyepewa kuuongoza ni mpinzani, je kwa kufanya hivi, anategemea huyu mama yetu kuhamasisha watu wa kilimanjaro waanze kumuunga mkono? Nawakilisha.
Mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa mgumu sana na mrahisi sana kuungoza kutokana na misimamo iliyomo damuni ya wakaazi wake kwani wanaamini kupigana kila siku ili kuupata mkate wao kila siku hivyo ukipelekwa kule kama mkuu wao ukajifanya ni mjuaji na huendani na wanachokiamini hutapata ushirikiano unaostaili katka kutekeleza ya majukumu yako kama ulivyoelekezwa kny barua yako ya uteuzi hivyo inahitaji umakini sana unapodili na hii jamii.(ikumbukwe kuwa huko kaskazini kuwa wafuasi wa upinzani ni kwamba wao walishaona kuwa ccm hawakutaka kuwainua kiuchumi toka pale walikokuwa kwenda juu zaidi kimaendeleo na ndiyo maana wapinzani waliweza kuutumia huo udhaifu na kufanikiwa kuchukua majimbo mengi)
Hivyo ninaamini kabisa JPM hakukosea kabisa kumtuma huyu mama kwani ndiyo aina ya watu watakaoweza kuelewana na hiyo jamii kwani ni mtu mwerevu na asiyekurupuka wakati wa kudili na issue yoyote itakayokwenda mbele yake.pia ikumbukwe kuwa JPM aliwaahidi wana kilimanjaro kny zile sherehe za mei mosi,2017 kuwa ahadi zote alizo wa ahidi kipindi cha kampeni atazitekeleza hivyo JPM alihitaji mtu makini wa kusimamia hela zote atakazozielekeza huko kny miradi bila kufujwa kwa namna yoyote ile na mtu huyo ni huyu mama.hivyo ninaamini kwa moyo wa dhati kabisa usishangae huyu mama akawaingia mioyoni mwao hadi hata jimbo la mbowe likarudi ccm hapo baadae.
Hivyo kwa uteuzi huu namsifu sana Magufuli hapa kalamba JOKER.
 
Nikiona hizi teuzi za mkuu na nikikumbuka hotuba yake kule lazima naanza kutilia shaka consistency yake
Siasa za leo ukitafuta consistency utakwama ndugu yangu- angalia chief liar wa dunia alichohaidi wakati wa kampeni na anacho kifanya sasa huko ma mtoni.
 
Wana jamvi, leo Rais wetu, kamteua Mwenyekiti na aliyekuwa Mgombea wa urais wa ACT kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro...Tukumbuke kuwa mkoa huu ni upinzani kwa asilimia kubwa,na aliyepewa kuuongoza ni mpinzani, je kwa kufanya hivi, anategemea huyu mama yetu kuhamasisha watu wa kilimanjaro waanze kumuunga mkono? Nawakilisha.
Kwani huyo alikuwa mpinzani au ccm,B"?
 
Back
Top Bottom