Gill Rugo
Member
- Aug 28, 2022
- 30
- 121
Itakua 2030, Greta Thurnberg ataenda kuandamana Riksdag kupinga mabadiliko ya tabia nchi. Itafika 2050, kamati ya Nobel itampatia tuzo ya mafanikio ya maisha kwa kubakiza dunia chini ya 3.5°. Ilikua hivyo pia kwa Martin Luther King. Alikufa kwa ajili ya haki za watu weusi lakini 2020 Derek Chauvin alipiga goti kwenye koo la George Floyd. Upo wapi usawa aliopigania Mandela Afrika Kusini? Hivi kweli Afrika ilipata uhuru?
Hivyo ndivyo itakuwa baina yangu na wewe. Mimi na wewe tupo ndani ya boksi. Tumewekwa kwa sababu ya rangi, au jinsia, au imani, au hadhi. Tutapambana kwa bidii lakini mwisho wa siku tutakufa maskini, au wenye kipato cha kati. Najua unaamini wewe ni wakipekee na Mungu ana mpango nawe, lakini sote ni maalumu na Mungu ana mipango nasi.
Mara kadhaa, mmoja wetu anatoboa boksi hilo. Huyo ndiye mfumo unamtumia kutuaminisha inawezekana. Tutapigana tukiamini fungu letu laja, lakini mwisho wa siku tunaishia kuutajilisha mfumo. Ni mamilioni wanatamani kuwa kama Diamond Platinumz, kuwa Kamala Harris, au Shahruk Khan, lakini inatimia kwa wasiozidi 10.
Dunia ina fomula rahisi: Wenye pesa na nguvu watatunukiwa pesa na nguvu zaidi kwa kazi za wasio na pesa na nguvu. Ni mfumo wa kibepari ulioandikwa na watu wachache na kutiwa muhuri kama njia pekee ya maisha.
Wachache hawa walianzisha benki kubwa na makampuni ya usimamizi wa mali kisha wakanunua chapa kubwa zote unazozifahamu. Kampuni washikadau hizo ni kama Black Rock, JP Morgan, Morgan Stanley, Goldman Sachs, Vanguard, na nyingine; na wanamiliki chapa za Apple, Samsung, Adidas, Nike, Vofafone, Airtel, Pepsi, Cocacola, Facebook, Tiktok, na vyingine nyingi. Chapa pekee wasizomiliki ni ndogo- kama Jamii forums na Azam, zisizoweza kutishia ukiritimba wao. Lakini zikikufumuka watazinunua.
Mwisho wa siku wanakalia pesa na nguvu zote. Kufikia 2022, taasisi ya Thinking Ahead inadai, washikadau(makampuni) wakubwa 500 wanamiliki dola trilioni 131 za mali. Na ripoti ya Oxfam ya 2022 inasema: 1% ya matajiri zaidi duniani inamiliki karibu nusu ya utajiri wa dunia, huku nusu ya chini ikimiliki 0.75% tu ya utajiri wa dunia. Haijatokea kwa bahati mbaya. Ni kwa neema ya mfumo uliobuniwa ili watengeneze pesa kwenye pande zote za sarafu. Wanatengeneza pesa vitani na penye amani. Wanatajirika penye demokrasia na penye udikteta, kwenye uharibifu wa tabia nchi na kwenye kupigania mazingira.
Angalia Tesla, mtengenezaji wa magari ya umeme. Inamilikiwa na washikadau walewale wanaomiliki wachafuzi kama Toyota, Ford, na BP oil. Usisahau pia Tesla inatumia madini yanayochimbwa na watoto wanaolipwa chini ya dola 2 kwa siku huko Kongo huku ikihamasisha usawa nchini Marekani. Au shirika la FOX NEWS linaloeneza itikadi za kibaguzi linavyomilikiwa na walewale wanaomiliki CNN yenye msimamo mpana. Wanaomiliki programu ya IOS ndio wanamiliki Android. Washikadau wa Disney ndio wanaomiliki WB. Hapa nyumbani, kampuni mama za Tigo, Airtel na Vodacom zinamilikiwa na washikadau walewale.
Haijalishi chapa gani utachagua, wao wataingiza pesa tu. Ukisusia kampuni moja kwenda nyingine, unakua unabadili akaunti watakayopokea pesa yao. Wanaimiliki seneti ya Marekani, hakuna kitu kinatendeka Afrika kisicho kwa ajili ya matakwa yao. Haijalishi nani utampigia kura au kama itakuja katiba mpya kwa sababu unabadili kiongozi na sio mfumo. Ndio maana hakuna utawala bora wala uwajibikaji.
Mfumo huu umeandikwa kana kwamba mabadiliko huja pale mwenye nguvu ama pesa akikubali. Angalia jinsi mweusi anavyopata haki pale ambapo mweupe ataridhia. Au mwanamke anapopata usawa pale mwanaume akiridhia. Lakini mfumo haumilikiwi na weupe wote au wanaume wote. Unamilikiwa na wanaume weupe wachache sana huku ukiwapendelea watu weupe na wanaume.
Ila ipo njia, njia ya kuleta usawa, ya kumaliza pengo la mali kati ya weusi na weupe, ya kuleta usawa wa kijinsia haraka, ya kuokoa tabia ya nchi.
Kama wao, nasi tuanzishe benki au kampuni ya usimamizi wa mali. Benki itakayomilikiwa na umma, ambayo makampuni washikadau ya mfumo huu hayana hisa.
Ni rahisi sana: Greta Thurnberg au mtu yeyote tutakaye mchagua anafungua benki na kuiita Benki ya Mabadiliko. Kwa sababu hakuna pesa, sote tunachangia dola 10. Lakini kila mchango unakuwa hisa iliyonunuliwa. Hisa ambayo haiwezi kuuzwa tena. Ikiwa watu million 100 watachangia, basi bilioni hiyo itatumika kujenga miundombinu ya benki ulimwenguni. Halafu kwa pamoja tutahamisha pesa zetu kutoka benki zao(JP Morgan, BOA, CRDB) kwenda benki yetu. Hii itathibiti vipi na wapi hela yetu inawekezwa.
Kisha tutabainisha malengo na maadili yetu. Tutasimamia haki za binadamu, uhuru, usawa, haki za wafanyakazi, tutapinga ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia. Yote hayo bila kutikisika.
Lakini wanaimiliki dunia. Je, tutaichukuaje?
Tutawanyang’anya na kuwapelekesha kama wanavyotufanyia. Chukua mabilioni ya dola anayoingiza Amazon huku akiwalipa wafanyakazi wake mishahara midogo. Kama benki, tutamuomba Amazon aongeze mishahara. Ikiwa Amazon atakataa basi benki yetu itanunua hisa kwenye kampuni shindani na Amazon. Halafu wote tutaisusia Amazon na kuagiza vitu kupitia kampuni yetu. Hii itawanyima washikadau wa Amazon pesa ambazo wangetegemea kuzipata kupitia Ebay kama Amazon Ikisusiwa. Faida tutakayoipata kwenye kampuni yetu tutawekeza kununua makampuni zaidi au kuongeza mishahara ya kampuni hiyo.
Kama Tesla akikataa kuondoa utumwa kwenye uzalishaji, hatununui magari ya Ford; tunaanzisha kampuni yetu ya utengenezaji wa magari. Kama Apple akipandisha bei kisa ubepari, tunainunua Samsung na kuifanya iwe kubwa zaidi. Kama Pfizer akigoma kushusha bei za dawa, tunaanzisha kiwanda chetu cha madawa. Ikiwa Vodacom itapandisha bei za vifurushi, tutanunua Smile na kuisusa Vodacom. Aidha watafanya tunachotaka au tutaziua kampuni zao.
Nguvu yetu ni idadi. Tutaupa ulimwengu mbadala wa makampuni bepari wanayojali faida tu. Kampuni ambazo benki yetu itamiliki zitalipa mishahara ya viwango, na hazitakua na ubaguzi. Watu zaidi watakapojiunga nasi, mfumo utakosa wa kumlenga ili kutunyamazisha. Ni kawaida kwa mfumo kuua lakini sasa tutakua benki wa watu bilioni, yenye mtandao wa wanasheria ulimwenguni. Kama Barrick akitoa rushwa Tanzania na watanzania hatuwezi kumshtaki, basi wenzetu walioko Marekani watamshtaki kwenye mahakama zao na kumsusia.
Hiyo ndiyo njia pekee, la sivyo tutaendelea kuandamana kudai haki huku wao wakiwahonga viongozi wasipitishe mabadiliko. Na njia hii haiuvunji sheria wala kuleta vurugu. Tunafanya kama wanavyofanya wao. Tunatengeneza ukiritimba wetu. Wao watabaki na pesa walizokwisha pata, sisi tunachukua mstakabali. Wataendelea kuwa matajiri, lakini wasio na nguvu.