Unalalaje lodge ya 80,000 na bado hujajipata

ukweli ni kuwa wengi wetu ni masikini. kuna wachache wana unafuu wa maisha na hata wao ukichunguza unakuta wana boost ya pesa za watangulizi wao (urithi) sasa wewe mwenzangu namimi soma hizi comments humu hlf ujichanganye.

kiukweli wengi wetu tunatoka familia masikini tena zingine ni umasikini uliopindukia na apo unakuta hata wewe apo kwenye utu uzima wako bado unajitafuta.

silaha ya kuiondoa jamii yako kwenye lindi la umasikini ni kuwaendeleza warithi wako, kuwa na rasilimali zingine kama nyumba, vibunda benki nk.

haya yote kama unafanya kazi serikalini hauwezi kuyafanikisha hasa kama unaendekeza sana hayo mambo ya starehe kama izo hotel za kulala bei za juu labda uwe mkwavi wa pesa za watu au uwe na sponsa maana ukiondoa mshahara ela pekee nyingi unayoweza kuipata kwa mara moja ni hiyo ya safari. ayo matumizi ya malaki kwa usiku mmoja wa kulala hotelini labda uwe uko sekta binafsi wanakolipa madolali.

msione haya majumba mkafikiri yanafanyika tu. hapana! kuna watu wametoa jasho na damu kufika apo. hlf kwa bahati mbaya sana hawa wanaojibana utakuta mwisho wa siku wanakuja kuitwa mafisadi kwa sababu ya rasilimali wanazomiliki bila kujua jasho na dam lililowatoka wahusika.
 
Mtoa mada ameeleza uhalisia wa maisha ulivyo hasa kwa watumishi wanapokuwa na safari za kikazi na kile wanacholipwa kwa siku.

Lakini jambo la kushangaza wachangiaji wengi wameamua kumuona huyu jamaa ni maskini na ana mawazo ya ki-umaskini kitu ambacho sio KWELI.

Tatizo la JF humu kila mmoja anataka kujionyesha ana uwezo mzuri wa kimaisha au ni tajiri kitu ambacho sio KWELI kabisa.
Acheni kujifanya mna uwezo ili hali mna maisha magumu.

Kuwa na kibanda cha kuishi, na kuwa na kagari ka kutembelea haimaanishi kuwa wewe una uwezo au kujiona tajiri.

Endelea kujitafuta kwa kufanya saving ili uweze kufikia hatua ya maisha Bora na sio bora maisha.

Acheni dharau za reja reja na majibu ya kandia
 
Uchawi huwa unaanzaga hivihivi.
Tabia za kimasikini huwa zipo kichwani na hazitoki
 
Wakati mimi naingia hali ilikua nzuri , safari zilikua nyingi , hivyo ukiachana na per diem mshahara hugusi unafanyia mambo mengine. Hakuna mwezi nilikua nakosa safari.

Ukiachana na hayo nilibahatika kutembelea maeneo mengi sana hapa nchini almost mikoa yote nimeimaliza na baadhi nimewekeza huko in terms of real estate.
 
Unalala ya bei rahisi, usiku karandinga la polisi linakuja kuwakamata kwamba unajihusisha kununua/kujiuza dada poa.

Baada ya hapo sijui utajitetea vipi jamii ikuelewe!
 
Kwani hujui kuwa JF asilimia kubwa wanajibu kufuata mkumbo?
 
Wengine tunaogopa kuoga kwenye mabafu ya ajabu ajabu kwahiyo tuvumiliane, anything for my sleep, kula nitaenda hata kwa mama ntilie. Ila sio kulala.

Nioge asubuhi halafu siku nzima niwe na mawazo juu ya sehemu niliyooga, kila nikitaka kula nikumbuke bafu /choo, nope 👎
 
Jf ina maajabu sana. Unaweza kukuta mtu anasema ivi kumbe kwao amekuzwa maisha ya choo cha shimo cha kulenga vile vyoo paspoti saizi
 
Jf ina maajabu sana. Unaweza kukuta mtu anasema ivi kumbe kwao amekuzwa maisha ya choo cha shimo cha kulenga vile vyoo paspoti saizi
Yes ni kweli, tena nimekulia Bush... hiyo haimaanishi siruhusiwi kubadilika na kufanya machaguo, Halafu kile choo cha shimo kwetu huwa nakisafisha mwenyewe, namwaga majivu na zile dawa tunapewa dispensary. Na tunatumia wana familia, huwezi onea kinyaa wana familia. Je una wasiwasi mwingine?

I'm sorry kama umekuwa offended, its not my fault.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…