Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 2,349
- 4,615
ukweli ni kuwa wengi wetu ni masikini. kuna wachache wana unafuu wa maisha na hata wao ukichunguza unakuta wana boost ya pesa za watangulizi wao (urithi) sasa wewe mwenzangu namimi soma hizi comments humu hlf ujichanganye.Mleta mada ana hoja ila wadau wanamshambulia tu.
Ni sahihi kusema kwamba kwa perdiem ya 130,000 kutumia 80,000 kwa Lodge sio matumizi mazuri ya pesa.
Mpaka ulipwe 130,000 ina maana viwango vyako ni vya chini na unapaswa kubudget pesa kulingana na viwango vyako.
Mimi nakumbuka kuna mshkaji alijenga nyumba kwa pesa hizi hizi za safari, ndio alinipokea kazini.
Tukiwa safari ananielekeza namna ya kuishi mtu unaweza dharau hii hoja ila ina maana kubwa sana.
kiukweli wengi wetu tunatoka familia masikini tena zingine ni umasikini uliopindukia na apo unakuta hata wewe apo kwenye utu uzima wako bado unajitafuta.
silaha ya kuiondoa jamii yako kwenye lindi la umasikini ni kuwaendeleza warithi wako, kuwa na rasilimali zingine kama nyumba, vibunda benki nk.
haya yote kama unafanya kazi serikalini hauwezi kuyafanikisha hasa kama unaendekeza sana hayo mambo ya starehe kama izo hotel za kulala bei za juu labda uwe mkwavi wa pesa za watu au uwe na sponsa maana ukiondoa mshahara ela pekee nyingi unayoweza kuipata kwa mara moja ni hiyo ya safari. ayo matumizi ya malaki kwa usiku mmoja wa kulala hotelini labda uwe uko sekta binafsi wanakolipa madolali.
msione haya majumba mkafikiri yanafanyika tu. hapana! kuna watu wametoa jasho na damu kufika apo. hlf kwa bahati mbaya sana hawa wanaojibana utakuta mwisho wa siku wanakuja kuitwa mafisadi kwa sababu ya rasilimali wanazomiliki bila kujua jasho na dam lililowatoka wahusika.