Unakumbuka nini ukiwa 1st year kwa wiki ya kuripoti chuoni?

Yaan sitakaa nisahau pale SAUT, malimbe. Nilikosa room hostel, foleni ya usajili nayo ikawa haiishi dah. Muda huo naishi guest, dah...kitaa napo room zikawa hazieleweki. Baada km ya siku tatu hv kuna jamaa mmoja alikuwa mmoja wa serikali ya wanafunzi basi akanionea huruma akaenda kunipa chumba kitaa.
 
kuna jamaa mmoja pale kwenye zile form za usajili pameandikwa school, jamaa akajua shule aliyetoka advance akajaza ndanda, badala ya kujaza school of business
 
I was eagle to make new friends and some of them now have become part of my family as a God mother to their children.
 
hahah nilipochaguliwa udsm nikaambiwa ukitaka kwenda ktk lecture room lazima nipitie pale utawala.basi nilikuwa napiga ruti ndefu sanaaa natoka coet naenda utawala ndio naenda theate 1 hahaha
 
hahah nilipochaguliwa udsm nikaambiwa ukitaka kwenda ktk lecture room lazima nipitie pale utawala.basi nilikuwa napiga ruti ndefu sanaaa natoka coet naenda utawala ndio naenda theate 1 hahaha
Hahahahahaha mkuuu imepenyaaa hii
 
Daaaa nakumbuka wiki ile ya kwanza nilivyokuwa natembea na begi langu lenye kompyuta mahala popote pale nilipokuwa naenda, hata kama naenda uwanjani.

Hii ni kutokana na maneno niliyoambiwa wakati natoka nyumban kuwa chuoni kuna wezi balaa, hivyo niwe makini kupita maelezo na Mali zangu.
 
Aiseee! First week ni hectic kwakweli!! Mie ilinishangaza ratiba, ina vipindi nonstop hadi usiku,nikawaza, 'inamaana hakuna kupumzika hata kidogo' nikachoka, kumbe unaangalia vinavyokuhusu tu.

Yote tisa, kumi lecture rooms zilikuwa kimbembe, unaisaka hadi unahisi kuzimia, kuna siku katika kuisaka seminar room na rafiki yangu tukakutana na lecturer nae anatafuta room, akatuuliza hiyo room ilipo tukamjibu hata sisi hatujui ndio tunaitafuta, sijui kama aliipata maana sisi tulichoka tukaingia chumba kimoja tukatulia na walikuwa wanasoma hesabu.

Lile jengo hadi kulizoea ilinichukua muda sana.
Chuo ghan
 
Nakumbuka nilitembea chuo kizima simjui ata mtu mmoja..upweke na kila kitu nikaona sbr nisafiri kurudi home kwanza adi wengine wafungue ndio ntarudi...
 
Back
Top Bottom