Unakumbuka nini kuhusu Mgomo wa Madaktari mwaka 2012?

9867_

JF-Expert Member
Jan 28, 2024
671
1,308
Wanajamvi kwema?

Bila kupoteza muda, nadhani wengi tunakumbuka kuwa mwaka 2012 kulikua na vuta ni kuvute za hapa na pale baina ya Madaktari nchini na Serikali chini ya aliyekuwa Rais wa kipindi hicho Dr. Jakaya Marisho Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (mzee wa “utapigwa tu”), issue ambayo ilipelekea chama cha madakatri kuitisha mgomo wa nchi nzima na kupelekea serikali kuagiza madaktari wa jeshi kuingia mahosipitalini kwaajili ya kutibu raia.
IMG_7680.jpeg

Binafsi nakumbuka sana tukio la Ulimboka kutekwa na kupigwa vibaya mnooo.

Anyway, tutakumbuka pia mgomo huu hatari zaidi kuwahi kutokea katika nchi yetu ulisababisha aliyekua Mwanasheria mkuu wa serikali wa kipindi hicho kupeleka maombi ya zuio la mgomo huo mahakamani ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania, Division ya kazi, Dar es Salaam chini ya Jaji Moshi ilitoa amri ya zuio ya mgomo huo kwasababu kubwa kwamba, kama mgomo huo ungeruhusiwa na amri hiyo isinge tolewa basi madhara makubwa ambayo yasingeweza kufidika yangetokea ikiwemo vifo.

Madakatri wao walikua wakidai kwamba hata walipokuwa wakitoa huduma watu walikua wakifariki kutokana na kukosa huduma stahiki na mazingira mabovu ya kazi kwaio walisema mgomo huo ulikuwa pia ukilenga kuilazimisha serikali kuchukua hatua za haraka ili kuboresha huduma za afya nchini.
IMG_7681.jpeg

Kwa upande mwingine madaktari walihitaji waongezewe posho ya kuitwa kazini kutoka 10k mpaka 25k, pia walitaka kuongezwa posho ya uchunguzi wa maiti kutoka 10k mpaka 100k na jingine ni kuwa walitaka uongozi wa juu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ubadilishwa mara moja.
IMG_7679.jpeg

Kutokana na mgomo huu, Dr. Haji Mponda aliyekua Waziri wa Afya aliondolewa madalakani yeye pamoja na aliyekua katibu mkuu wa wizara hiyo Dr Brandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali Dr Deo Mtasiwa na kisha Dr Hussein Ally Mwinyi akawa ndiye waziri wa wizara hiyo.

Licha ya mabadiliko hayo ya uongozi madaktari walidai baadhi ya ya madai yao ya msingi bado hayajafanyiwa kazi na hivyo kupelekea kutangaza mgomo mpya mnamo tarehe 21 June 2012 .

Pia tunakumbuka vyema kuwa mgomo huu ulikua ukiongozwa na Dr. Steven Ulimboka ambaye alikua ndiye mwenyekiti wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) ambapo alilipotiwa kutekwa na watu wasiojulikana siku 5 tu kutoka kutangaza mgomo huo yani tarehe 26 June 2012 maeneo ya leaders club Dar es Salaam.
IMG_7682.jpeg

Ulimboka alitekwa wakati alipokuwa katika mazungumzo juu ya mgomo huo na mtu mmoja aliyemuita na kujitambulisha kama Abed na Afisa wa serikali kutoka ikulu na kuja kuonekana kesho yake katika msitu wa Mwabepande uliopo bunju Dar Es Salaam na ndipo msamalia mmoja alimuokota na kumpeleka kituo cha polisi Mwabepande ambapo hapo Dr ulimboka alifatwa na aliyekua Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu wa wakati huo Bi. Helen Kija ambaye nae alisema kuwa licha ya jitihada zake za kupigia ambulance kutoka muhimbili kugonga mwamba na kuamua kumkimbiza Dr Ulimboka hospitalini kwa kutumia gari yake binafsi laki bado njiani hapo walikutana na vikwazo mbalimbali ikiwemo foleni na uwepo wa gari moja iliyokua ikiwazinga mbele yao ili kuwachelewesha hospitali japo baadae walipatiwa msaada wa ambulance kutoka katika shirika la afya la AAR ambapo lilimpeleka Dr Ulimboka mpaka moi ambapo alilazwa kwa muda kabla ya kwenda nchini South Africa kwa matibabu.
IMG_7685.jpeg

Hii issue ya Ulimboka iliacha mjadala mkali sana ikiwa swali kuu ni je, ni kina nani waliomteka Ulimboka??.

Gazeti la mwanahalisi liliwahi kuchapisha habari iliyosema “Aliyemteka Ulimboka huyu hapa” ‘Ni Ighondu wa usalama wa Taifa’ habari ilisema kwamba aliyemteka Dr Ulimboka ni Ramadhani Ighondu na kuwa ndiye afisa wa usalama wa Taifa aliyekua katika mzungumzo na Dr Ulimboka, dakika chache kabla ya kutekwa kwake, jambo ambalo lilisababisha serikali kulifungia gazeti hilo kwa muda usiojulikana kwa kosa la kuandika habari za upotoshaji na uchochezi.
IMG_7686.jpeg

JK yeye alitangaza kuwa serikali yake aihusiki kivyovyote na utekaji huo wa Ulimboka na wakati huohuo Waziri mkuu Pinda naye akiliambia bunge kuwa serikali aihusiki na utekaji wa Ulimboka.

Siku chache baadae kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi, Dar Es Salaam wa wakati huo Suleiman Kova alidai kuwa wamemkamata mtu mmoja aitwae Joshua Malundi (21) kutoka kenya ambaye amekiri kuhusika na kumteka na kumtesa Dr ulimboka, Kova alisema kuwa mtu huyo alienda kutubu makosa yake katika kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo kawe Dar Es Salaam hata hivyo Ngwajima ambaye ndiye kiongozi wa kanisa hilo, alikanusha kauli hiyo ambapo hata Joshua naye baadae alikanusha kauli hiyo na kisha kupewa adhabu ya kifungu cha mwezi mmoja jela pamoja na fine ya 1000 aliyolipiwa na moja ya waandish wa habari kwa kosa la kulipotosha jeshi la polisi.
IMG_7688.jpeg

Pamoja na hayo yote mpaka leo hakuna mtu yeyote aliyethibitika kama mtejaji wa Dr Ulimboka na kitu kinacho nishangaza mimi mpaka leo hii na wadau wengi waliokuwa wakifuatilia suala hili ni ukimya aliokuwa nao Dr Ulimboka kulizungumzia suala hili

Najiuliza Why aliamua kulikalia kimya kabisa suala hili licha ya kufatwa na mamia ya waandishi wa habari kutaka kumuhoji juu ya suala hili toka alipotoka nchini SA kwa matibabu, au kuna nguvu ilitumika kumkalisha kimya🤷🏽‍♂️?

Anyway, ikiwa leo ni alhamisi ya TBT, tuambie unakumbuka nini kuhusiana na mgomo huu mkubwa zaidi kuwahi kutokea hapa nchini.


View: https://youtu.be/EgU-jcaA718?si=bkF6BJqqnOBRm0LW

PIA SOMA 👇🏼​

 

Attachments

  • IMG_7683.jpeg
    IMG_7683.jpeg
    17.4 KB · Views: 3
Waziri wa afya alizungumza kumuomba Ulimboka aache ili majadiliano yaendelee watanzania wanakufa .
Ulimboka Akajibu hata kabla ya mgomo watu walikua wanakufa .
Sijaelewa, kwahiyo hili ndo lina justify alichofanyiwa?🤔​
 
Madaktari walikua wanagoma hospitali hakuna vifaa tiba, akatokea mtangazaji mmoja akawasema sana kwenye kipindi chake na alikua machachari mwenyewe.....

Na faili lake la kuchukua zile naniliu likawekwa wazi.

Bahati mbaya mtangazaji huyo huyo alikuja kuugua na kufariki kwa kukosekana dawa (kitu madaktari walichokua wanataka dawa ziwepo).....

Ndo kitu nakumbuka katika huu mgomo
 
Madaktari walikua wanagoma hospitali hakuna vifaa tiba, akatokea mwandishi mmoja akawasema sana kwenye kipindi chake na alikua machachari mwenyewe.....

Na faili lake la kuchukua zile naniliu likawekwa wazi.

Bahati mbaya mwandishi huyo huyo alikuja kuugua na kufariki kwa kukosekana dawa (kitu madaktari walichokua wanataka dawa ziwepo).....

Ndo kitu nakumbuka katika huu mgomo
tufungulie code😁
 
Back
Top Bottom