Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,398
4,203
Maana ya Gen Z.
Kwa mujibu vyanzo vya mtandaoni, Gen Z ni vijana waliozaliwa kuanzia mwishoni mwa miaka 1990. Pia wanafahamika kama kizazi cha kidijitali kwa sababu walizaliwa wakati mtandao ndio umeanza kuchipukia.

Hiki ndicho kizazi kinachosadikika kukuza mtandao ndio maana kimepewa jina Gen Z ambalo lina maana ya: Gen=Generation. Z=Zoomer. Hivyo, kijana aliyezaliwa katika hicho anaweza kuwa na miaka 26-28

Gen Z ya Tanzania!

Tumeona au kusikia huko Kenya Gen Z yao imeandaa maandamano bila kujali ukabila dhidi ya mswaada wa kodi na wamefanikiwa kwa sababu rais hajasaini na ameurudisha bungeni. Gen Z ya Kenya imekuwa kitu kimoja kupigania mustakabali wao.


Pia soma: Kule Kenya Gen Z wanadili na Wakusanya Kodi wa Kenya, Tanzania tunadili na Mbowe ambaye hakusanyi kodi

Mimi nawauliza wajumbe kila mmoja atathmini kwa kurejea Gen Z ya Tanzania iliyopo mtaani na mtandaoni;

1. Je, Gen Z ya Tanzania ina uwezo wa kupigania haki zao?

2. Je, Gen Z ya Tanzania inafuatilia mambo yanayohusu nchi yao?

3. Je, Gen Z ya Tanzania inauwezo wa kujisimamia katika maisha na kufika mbali au ni mpaka wapewe mwongozo na wazazi au walezi?

4. Je, Gen Z ya Tanzania inatumia muda mwingi kufanya nini katika maisha yao ya kila siku?

5. Je, Gen Z ya Tanzania inaweza kupewa madaraka mbalimbali na wakafanya vizuri?

6.Je, Gen Z ya Tanzania ni ya moto au imepoa? Kama imepoa, ni nini kimesababisha kuwa hivi?

Ikumbukwe, Gen Z ndio baadae wanakuwa watu wazima. Je, Gen Z ya Tanzania inaandaliwaje baadae kuwa watu wazima na kuongoza nchi baada ya wale wazee wajamaa wote kuisha?
 
Gen Z ya Tanzania!
Kwa bahati mbaya baadhi ya Gen Z wa Tanzania wanaelekea kuharibiwa na profession mpya ya uchawa. Kuna siku niliona humu uzi ukisema hiyo ni kati ya profession zinazolipa vizuri kwa sasa.

Vijana wakizoea kujipendekeza na kupigia chapuo misimamo ya hovyo ambayo hata wao wenyewe hawaiamini ila wanafanya kwa sababu ya matumbo yao, maana yake kuna tatizo kubwa
 
Back
Top Bottom