Unahisi ni sababu ipi zaidi inayofanya ndoa nyingi za vijana kuvunjika?

Analog

JF-Expert Member
Apr 4, 2024
291
531
Ndoa ni maridhiano baina ya mtu(mme) na mtu(mke) kisha yakaidhinishwa ama kukamilishwa kwa sheria ya dini, kiserikal ama tamaduni. Suala la kuvunjika ndoa nyingi za vijana limekuwa ni kawaida siku hzi, unahisi ni sababu gani kati ya hizi ambayo imezidi?
  • Ukosefu wa elimu ya ndoa
  • Matumizi ya simu
  • Mmong'onyoko wa maadil
  • Kukosekana uadilifu katika ndoa
  • Uzinzi
  • Kupungua uvumilivu katika ndoa
  • Tatizo la afya ya akili.
 
1. Pesa

2. Hela

3. Maokoto

4. Njoro njoro

5. Mkwanja

6. MONEY

ASILIMIA KUBWA WANAOANA KWA KUKURUPUKA AU KIJANA KUMVUTA BINTI KWA PESA ASIZOKUA NAZO,Binti anawahi ndoani akijua kijana ana pesa za kutosha hivyo atazifaidi vizuri
 
1. Watu hawa 2 wanaoingia kwenye ndoa wawe wanapendana kutoka ndani mioyoni mwao.

Tatizo kwenye ndoa za siku hizi mmoja wa wanandoa anakuwa amevutiwa na vitu, hela, status, cheo, n.k.

2. Ubinafsi. Unaona kama hii sababu ya Shusho kuvunja ndoa yake? Ni ubinafsi ulimsukuma.

Screenshot_20240410-225625.png
 
Tatizo watu hawataki kukubaliana,kwenye dunia ya utandawazi kuchapiwa ni kawaida....sasa wale wanaojiona wanaume utasikia "nilimpa kila kitu".
Btw hakuna maadili,wanandoa wanaoishi kwa kumuogopa mungu wote wawili hiyo ndoa hadi mmoja afe🥸
NB: bado sijaoa😎
 
Wengi wao wanaingia katika ndoa kuficha aibu ya kukaa mda mrefu bila kuolewa, hii ni kwa wanawake
Kupelekea kupata mtu ambae ajashibana nae na hana mapenz nae kiasi iko
Sababu kuoana watu ambao mnapendana ni muhim sababu hufanya muweze kuvumiliana au kuhurumiana katika majambo mbali mbali sabab ya ile bond ya upendo
 
Kila Ndoa inavunjika kwa sababu tofauti na nyingine hauwezi kudhani kama inaweza kuwa sababu.

Kwangu mimi naona Ndoa zinavunjika kwa kuwa wanaoana watu kwa kupendana tu bila hata kuendana na upendo ni kitu ambacho kinaisha na kikiisha mnaanza kuishi uhalisia na hapo ndio shughuli inaanza.

Utafiti unaonyesha Upendo wa wanandoa unakuwepo kwa wastani wa miaka miwili na baada ya hapo tabia za kila mmoja ndio zitafanya muendelee kuishi ikiwa tu mnaendana.

Watu wanaoendana wanaweza kuishi bila hata Ndoa kwasababu wanakua marafiki na wanaweza kuvumiliana mapungufu.
 
Back
Top Bottom