Yaa unalipa lakini mwisho wake hauwi vizuri. Nitakupa mfano kidogo, Maalim alimfanyia yule mzee unafiki na kusababisha mzee kuvuliwa nyadhifa zote akidhani atateukiwa kuwa Rais, mwisho hakuwa Rais. Chadema waliwahi kusema hawawezi kushirikiana na cuf kwa kuwa cuf ni CCM B baada ya mwafaka, baadaye wakaazima mgombea mweza wapate urais, mwisho hawakupata. Chadema waliwahi kuzunguka nchi nzima wakidai Mh.Lowassa ni fisadi na Mbowe akasema jamaa ni dhaifu sana, mwisho wakafanya unafiki wa kumsafisha nchi nzima kuwa ni safi na kumwazima agombee urais akifikiri watapata, mwisho walikosa Rais. Mifano iko mingi, Nakubaliana unafiki unalipa kwa kitambo tu, mwisho unakuwa sio.