Unaenda katika nyumba za ibada ili ufaidike na nini?

Ntaganda boy

Member
Jan 16, 2016
90
59
Mara nyingi najiuliza swali juu ya faida ya kusali ni ipi na kwanini watu wanatumia muda mwingi kusali na sio kutafuta mali.

Je, kusali ni lazima iwe katika nyumba za ibada au unaweza kusalia sehemu yoyote na kama unaweza kusalia sehemu yoyote kuna faida gani kukutana katika nyumba za ibada.

Je, unapaswa uombewe au ujiombee?
 
Mkuu unajua moja ya vitu vinanirudisha nyuma juu ya hizi imani za kidini ni matabaka kwann kuna matabaka sijui Muslim mara Christian kule Budas,Paganism nani yupo sahihi???
 
Kuna maisha ya mwilini mkuu na kuna maisha ya rohoni, kila maisha yana maandalizi yake, wewe ukijikita kutafuta mali usiende kanisani kumtafuta Yesu utafanikiwa duniani lakini kwenye maisha yako baada ya kifo chako utaishia jehannum ya moto na hapo ndipo utakapokuwa milele hiyo ni kanuni!! Tunasali au kwenda kuabudu kanisani kwa sababu ni agizo la Mungu ( waebrania 10:25"

wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Ukifahamu kuwa baada ya kifo chako kuna maisha baada ya haya huwezi kuuliza hayo maswali yako mpendwa

Mara nyingi wanadamu tunaangalia sana vinavyoonekana, ndo unakuta unasoma sana muda wote kusoma, kuwa busy sana, kutafuta mali usiku na mchana, unasahau kuwa kuna maisha baada ya kifo chako,

2 korintho 4:18"
tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.

Mtu ambaye anahoji kwanini watu wanasali au kwenda makanisani huyo mtu ni kipofu na ni mpumbavu maana hajui kitu pamoja na mali zake na usomi wake lakini hana kitu ni mtupu!

Zaburi 14:1"
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

Ni vizuri kusoma sana, kutafuta mali, fedha nk lakini kumbuka ipo siku utasimama mbele za Mùngu kutoa hesabu ya mema au mabaya
Mhubiri 11:9"

Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.

Ni vizuri ukajifunza kwa hawa watu walikuwa na kila kitu Leo hawapo unapaswa kujiuliza Leo hii wapo wapi
1: magufuli
2:mengi
3: membe
4: mrema
5: kubaki
6: moi
7: mkapa
8: Queen Elizabeth
Nk
Luka 12:16
Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hiyo nawaambia, Msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini.
Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, na Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege! Na yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
Basi, ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo, kwa nini kujisumbua kwa ajili ya yale mengine?
Ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa; wala msifanye wasiwasi,

kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.
Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa.

hivyo mpendwa usione kuwa wanaosali ni wajinga hao wanajua wanachokifanya, ipo siku utayakumbuka maneno yangu lazima ujue kuwa kuna ziwa la moto na kuna ufalme wa Mungu uchaguzi wa sehemu utakapoenda ni wewe mwenyewe, unapaswa kujua kuwa pasipokumwamini YESU kristo hakuna kwenda mbinguni, usidanganywe na dini yako, Yesu ndiye njia pekee na uzima pasipo huyo Yesu utaishia motoni mpendwa
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Ufunuo 21:8

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Matendo Ya Mitume 4:12

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Yohana 14:6

Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.

Isaya 35:8

Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

Mhubiri 12:14

katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.

Warumi 2:16

Siku njema
 
Kuna faida kubwa sana mkutanapo kanisani, japo sijaenda sku nyingi mungu anisamehe. Mimi ni mtu niliekua na question sana dini ni kupinga imani za watu. Acheni huo ujinga kama unahisi dini haina maana kwako usi criticise imani za watu wengine. Dini na imani kitu personal
 
Mara nyingi najiuliza swali juu ya faida ya kusali ni ipi na kwanini watu wanatumia muda mwingi kusali na sio kutafuta mali.

Je, kusali ni lazima iwe katika nyumba za ibada au unaweza kusalia sehemu yoyote na kama unaweza kusalia sehemu yoyote kuna faida gani kukutana katika nyumba za ibada.

Je, unapaswa uombewe au ujiombee?
kwani wewe ukisali huko kazini kwako na wao wakenda kusali huko wanakoenda makanisani, kihedemswede, kihoro na kiroho papooh unakitoa wap 🐒

si usonge mbele kivyako na wao wasonge kivyao kadiri wanavyoona inafaa 🐒
 
Watu wa kidini inawezekana wakawa wanaongoza kwa tabia mbaya, mataifa ya kidini zaidi ndio yenye ufisadi, ukandamizaji na mambo ya ajabu ajabu sana ukilinganisha na yasiyo ya kidini sana.
ni muhimu zaidi wewe ukang'ang'ana na hiyo yako nzuri sana 🐒

huna haja ya kubabaika, kujaji na kuhukumu tabia ya wengine 🐒
 
Back
Top Bottom