Unabii: Nimeona Simba kutoka mbinguni akishambuliwa na nyoka watatu kutoka baharin mpaka kufa

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
18,295
27,333
Amani iwe nanyi wapendwa katika BWANA

Juzi tarehe 1 mwezi wa 10 majira ya usiku nilimuona simba mmoja wa wasitan akishuka kutoka maeneo ya angan

Kisha nikaona tena nyoka watatu nao ni wa wastan wenye ukubwa kias unene wa mipini miwili wakipanda kutoka baharin

Simba alipokaribia kutua chini kabla hajatua urefu kama ghorofa 7 kutoka juu wale nyoka watatu kutoka baharin walimfuata huko huko juu kwa juu na kuanza kumshambulia sana kwa nguvu kisha nikamuona huyo simba akijaribu kurudi juu angan zaid lakin wale nyoka walimtelemsha chini na kuanza kumshambulia zaid

Kisha nikamuona yule Simba akijaribu kuwakimbia wale nyoka watatu kwa kutimua mbio ardhini lakin mbio zake hazikuweza kufua dafu mbele ya wale nyoka

Wale nyoka watatu walimkimbiza zaid na kumpata kisha wakamshambulia zaid hata simba yule kuishiwa nguvu na kufa kabisa

Then nikashituka

Lakini ikumbukwe kwamba kabla ya tarehe 1 mwezi wa kumi siku tatu nyuma nilikuwa nipo kwenye mfungo wa mtakatifu wa BWANA Antonio wa Padua

Wajuzi karibun kwa tafasiri zaid juu ya huu unabii

Asanten sana

LONDON BOY
 
Back
Top Bottom