Una mapenzi ya kweli ila kukosa pesa ndio kunafanya uonekane msumbufu 😔

Umeshawah kupitia hali ya upweke mkuu, ambao unahitaji mpenzi wako aonyeshe ushirikiano? pesa huna, ukute hata salio umekopa, halafu unampigia mtu simu hapokei, au akipokea ulikuwa unasemaje, anakukata nyongo, maini na utumbo kwa pamoja. Nimelia sana
Wakati ulipokua nacho ulimjali, ulimpa muda wako?

Mapenzi ni bond, akujue na wewe umjue. Siku usipokua sawa kuna signs utaonesha na atajua la kufanya.
Kama hamna bond nzuri mtaishia kuchukiana tu.
 
Wakati ulipokua nacho ulimjali, ulimpa muda wako?

Mapenzi ni bond, akujue na wewe umjue. Siku usipokua sawa kuna signs utaonesha na atajua la kufanya.
Kama hamna bond nzuri mtaishia kuchukiana tu.
Mkuu hawa viumbe unawajua vizuri au unawasoma kwenywe gazeti mkuu, ujue practical tofauti na theory
 
KUKOSA PESA KUNAWEZA FANYA UONEKANE MSUMBUFU KWENYE MAHUSIANO 😔


Maskini unaweza kuwa na upendo tu wa dhati na uaminifu mkubwa ila kukosa kwako tu pesa ukaonekana MSUMBUFU kwenye mahusiano.

Kumpigia simu za kumjali na salamu za hapa na pale ni msingi mzuri wa mahusiano ila kwa sababu tu huna pesa ukifanya hayo utaonekana MSUMBUFU uliyekosa cha kufanya 😔

Kukosa pesa kunaweza fanya uombe msahamaha hata kama kosa sio lako, tena usipodhibiti vizuri hisia za Kukosa pesa utajikuta kwenye mtego wa kutumikishwa kwenye mahusiano.


Hata kwenye ndoa usishangae ukiomba unyumba unaambiwa " YAANI AKILI YAKO INAWAZA HAYO TU HUFIKIRII KUHUSU PESA 😔


MWISHO WA SIKU DUNIA ITAHITAJI UWE NA PESA LA SIVYO UTAONA INAKULEMEA KWA KILA KITU IKIWEMO MAHUSIANO.

Ukianza kuona unalemewa na kila kashikashi ya Dunia kuna uwezekano mkubwa ukawa huna pesa.

Dunia ina kashikashi zake ila amini kuwa maskini ndio walengwa namba moja wa hizo kashikashi.


Jambo la kuamka nalo kila siku ni kutafuta tu pesa kwa uhalali la sivyo UZITO WOTE WA DUNIA UTAKUWA JUU YAKO.

Mwanasayansi Saul kalivubha.
#fikia ndoto zako.
Hiki ndicho kinacho sababisha hata ndoa zikose maana.Kweli mahusiano mwanaume unahitaji kuwa na pesa, ila wanawake wengi hawajui kutofautisha basic needs za mwanamke na luxury needs.Wanaume wengi wanauwezo wa kuwapa wanawake zao basics needs, ila luxury needs ni wachache sana. Hapo ndipo wanawake huwapoteza watu wanao wakubali na kuwafeel kisa tu jamaa hana hela ya kumtimizia luxury needs.

Ndoa zina ups na down,inawezekana mlipo kutana mwanzoni mwamba alikuwa na mawe alikuwa anampa mpaka zile luxury needs na basics needs,ila kuna kipindi inawezekana mwana akapitia msoto wa kiuchumi, hapo ndipo mwanamke humuona mwana hana maana japo anamtimizia basic needs zake kama mwanamke.

Ndio maana mwanamme husiingie kwenye mahusiano ya ndoa, ANAYENDEKEZA fedha kuliko utu au mwanamke mwenye matarajio makubwa ya kiuchumi kupitia ndoa. Kwani nidhamu ya mwanamke kwenye fedha, inaweza ikakuambia unadate na malaya/mdangaji au mwanamke atakaye kuwa mkeo. Ndio maana kwenye ndoa viapo vyake vinabeba nyakati ngumu na nzuri, so husiingie kwenye mahusiano na mwanamke ambaye hakubali kuishi na ww kwenye nyakati ngumu na utamjua kupitia fedha na hata kama unapesa mpe pesa,ila sometimes muingizie kama huna kitu then angalia attitude yake inakuwaje, ukiona anabadilika na kukuleta dharau piga acha tafuta mwengine.
 
Ndoa ni ajira kwa mwanamke
Mwanaume anamuajiri mwanamke .

Ndio maana halisi ya ndoa sasa .
Kwanini how ukijua huna uwezo wa kumlipa mshahara mwanamke?
Ndoa ni mzigo kwa mwanamme.

Wadogo zetu wa kiume Wana msongo wa mawazo waoea nani ..
Sijui tunaelekea wapi? Dunia ya kuwa na baba bila mama..
 
Ni kweli kukosa pesa na muda wa kutafuta pesa mtu unakua msumbufu mnoo.

Unapiga simu mara nne haipokelewi unatuma mimeseji mambo nakusalimia bado haujajibiwa ushapiga.....haya umepokelewa nlikua nakujulia hali haya poa poa....ukikata meseji hiloooo nambie mama, mama kivipi jombaaaa.

Acha usumbufu tafuta ramani upate hela.
 
Back
Top Bottom