Una mapenzi ya kweli ila kukosa pesa ndio kunafanya uonekane msumbufu 😔

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Feb 4, 2024
308
822
KUKOSA PESA KUNAWEZA FANYA UONEKANE MSUMBUFU KWENYE MAHUSIANO 😔

Maskini unaweza kuwa na upendo tu wa dhati na uaminifu mkubwa ila kukosa kwako tu pesa ukaonekana MSUMBUFU kwenye mahusiano.

Kumpigia simu za kumjali na salamu za hapa na pale ni msingi mzuri wa mahusiano ila kwa sababu tu huna pesa ukifanya hayo utaonekana MSUMBUFU uliyekosa cha kufanya 😔

Kukosa pesa kunaweza fanya uombe msahamaha hata kama kosa sio lako, tena usipodhibiti vizuri hisia za Kukosa pesa utajikuta kwenye mtego wa kutumikishwa kwenye mahusiano.

Hata kwenye ndoa usishangae ukiomba unyumba unaambiwa " YAANI AKILI YAKO INAWAZA HAYO TU HUFIKIRII KUHUSU PESA 😔

MWISHO WA SIKU DUNIA ITAHITAJI UWE NA PESA LA SIVYO UTAONA INAKULEMEA KWA KILA KITU IKIWEMO MAHUSIANO.

Ukianza kuona unalemewa na kila kashikashi ya Dunia kuna uwezekano mkubwa ukawa huna pesa.

Dunia ina kashikashi zake ila amini kuwa maskini ndio walengwa namba moja wa hizo kashikashi.

Jambo la kuamka nalo kila siku ni kutafuta tu pesa kwa uhalali la sivyo UZITO WOTE WA DUNIA UTAKUWA JUU YAKO.

Mwanasayansi Saul kalivubha.
#fikia ndoto zako.
 
Ni kweli kukosa pesa na muda wa kutafuta pesa mtu unakua msumbufu mnoo.

Unapiga simu mara nne haipokelewi unatuma mimeseji mambo nakusalimia bado haujajibiwa ushapiga.....haya umepokelewa nlikua nakujulia hali haya poa poa....ukikata meseji hiloooo nambie mama, mama kivipi jombaaaa.

Acha usumbufu tafuta ramani upate hela.
 
HHahaha nimewahi kuwa hivi sehemu hakika niliteseka

Mapenzi ya wanafunzi hayo.

How comes unataka muda wote sijui tuchart, usiku mzima muongee kwenye simu, mkiwa wote apechealolo hamtachokana ila kama mmoja anajiweza hilo penzi litakufa.
 
Nimelia sana, lakini sasa cha ajabu ni hiki, ukiwa na pesa bado wasio na pesa wanakulia mkeo/mpenzi wako kwa sababu ya hizo hizo meseji na calls ndo pale wazungu wanasema the world is not fair
 
Hata kama atakuthamini kwa namna gani, pesa lazima zihusike, anaweza yeye akawa upande wako, je, utaweza kuhimili kebehi kutoka kwa ndugu zake?
Hili nalo ni tatizo,. Anaweza akampata mtu wakapendana na akamthamini lakini kwenye suala la kuoa na kushirikisha ndugu hata ningekua ni mimi siwezi kuvumilia,.

Waweke tu mikakati ya namna gani wanatakiwa waongeze kipato kabla hawajafikia hatua hizo za ndoa,..

Lakini haya mambo yanaogopesha sana
 
We acha tu, kuna dhihaka na masimango ya kila namna, unakuta kuna muda naye mke kauvumilivu kanamshinda kah! usiombe sijui kuna kimchango cha ndugu kinatakiwa aaagry , the world is not fair
 
Mapenzi ya wanafunzi hayo.

How comes unataka muda wote sijui tuchart, usiku mzima muongee kwenye simu, mkiwa wote apechealolo hamtachokana ila kama mmoja anajiweza hilo penzi litakufa.
Umeshawah kupitia hali ya upweke mkuu, ambao unahitaji mpenzi wako aonyeshe ushirikiano? pesa huna, ukute hata salio umekopa, halafu unampigia mtu simu hapokei, au akipokea ulikuwa unasemaje, anakukata nyongo, maini na utumbo kwa pamoja. Nimelia sana
 
We acha tu, kuna dhihaka na masimango ya kila namna, unakuta kuna muda naye mke kauvumilivu kanamshinda kah! usiombe sijui kuna kimchango cha ndugu kinatakiwa aaagry , the world is not fair
Kungekua na sheria yw kudhibiti watu kwenye mahusiano ya watu labda ingekua afadhali kidogo😃😬

Maana sometimes unaweza kuta wahusika wanaelewana vizuri tu na kupendana lakini maneno ya watu ndio yanawatoa kwenye Reli
 
Back
Top Bottom