Umoja wa Ulaya waridhishwa na hatua za Tanzania kukuza uchumi wa kidigitali

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
572
1,348
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry William Silaa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka Umoja wa Ulaya, Hans Christian Stausboll, ambaye wamejadili naye masuala ya ushirikiano katika uchumi wa kidijitali nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Desemba 11, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine umoja huo umefurahishwa na maendeleo mbalimbali ya kidijitali nchini na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika masuala ya TEHAMA.

Tanzania imenufaika na ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya (EU), kupitia mradi wa Digital4 Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano (2021-2025), wenye thamani ya Euro milioni 35.

Screenshot 2024-12-11 190945.png
 
Back
Top Bottom