Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,409
Jumuiya ya Umoja wa Ulaya hivi leo wametoa tamko lifuatalo kwa ushirikiano na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya wenye uwakilishi Tanzania na kuungwa mkono na Mwakilishi na Mabalozi wa Norwei, Kanada na Uswisi
"Tunashuhudia kwa wasiwasi muendelezo wa matukio ya hivi karibuni yanayotishia nidhamu ya kidemokrasia na haki za Watanzania, katika nchi iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa utulivu, amani na uhuru.
"Tumesikitishwa na kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi mwisho wa juma lililopita Akwilina Akwilini Bafta, anayeombolezwa nchi nzima. Tunakaribisha wito wa Rais Magufuli wa uchunguzi wa haraka. Vilevile, tunatoa wito wa uchunguzi wa kina katika vifo vyote vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu. Tunatoa pole za dhati kwa familia zao zote.
"Tuna wasiwasi na ongezeko la ripoti za ukatili katika miezi ya hivi karibuni, kama vile: jaribio lililohatarisha maisha ya Mbunge Tundu Lissu; kupotea kwa watu kama mwandishi wa Habari Azory Gwanda; pamoja na mashambulio yaliyopoteza uhai wa viongozi wa serikali, wawakilishi wa vyombo vya usalama na wananchi yaliyotokea Mkoa wa Pwani ndani ya miaka miwili iliyopita.
"Tunaungana na watanzania katika kuziomba mamlaka husika, kutunza amani na usalama wa michakato ya kidemokrasia, nchi, watu wake na kuheshimu utawala wa sheria bila udhalimu."