Lissu wazungu walishamtia najisi siwezi kumuamini tena. Tayari Lissu yuko compromised.

Hivi Lissu akishinda Urais si wabeligiji watajitwalia ziwa Nyanza liwe lao?
Lissu na genge lake wakipata madaraka kwenye nchi hii, taifa litalia na kusaga meno.
 
magafulists wanateseka sana wanaokoteza vitu vya kufurahisha masikio yao wanasaau mungu wao kafa.
 


Alafu kuna wajinga watatu Assad. Lema na Lisu wanatokwa povu kutuaminisha kwamba Magufuli alikuwa zero tu.

Haya sasa hata mabeberu yanayowalea Ulaya yamewakana sasa, yamesema rais Magufuli alikuwa kiongozi mwenye maono na mwenye mapenzi ya kweli na nchi yake.

Mkuu hii ndio Tabia ya mabeberu ...yananusa hata madume yaliyohasiwa!
 
_118084313_ea6748e7-c97b-463a-b9e1-79715247324b.jpg

"Tanzania imefanikiwa kufikia nchi ya watu wenye kipato cha kati miaka minne kabla ya kufikia 2025,..' alisema Katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres


Baadhi ya viongozi katika kikao cha 75 cha mkutano wa 59 wa Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika siku ya Ijumaa Aprili tarehe 16, 2021 wametambua alama za uongozi za za aliyekuwa rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli.
Viongozi hao wameahidi kuendelea kushirikiana na rais wa sasa wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan .
Kikao hicho kiliongozwa na Volkan Bozkir Rais wa baraza kuu la UN kilikuwa na ajenda kadhaa ikiwemo ya kutambua mchango wa Magufuli aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo Machi 17, 2021.
Katibu mkuu wa umoja huo, António Guterres amesema Magufuli atakumbukwa kwa mchango wake katika kurejesha maadili ya utumishi wa umma, kupambana na rushwa, ujenzi wa miundombinu na mapinduzi ya viwanda ambayo ni msingi katika ukuaji uchumi.
"Tanzania imefanikiwa kufikia nchi ya watu wenye kipato cha kati miaka minne kabla ya kufikia 2025, alifanikiwa kuwezesha mfumo wa elimu bila malipo iliyowezesha watoto wengi kuongezeka shuleni, pia alifanikiwa kupeleka huduma za umeme vijijini kwa jitihada za kufikia wananchi wengi."



_118084314_401dceb4-53f4-40de-8aa5-31ca37af37f9.jpg

Balozi Profesa Kennedy Gastorn, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Kwenye Umoja wa Mataifa akihutubia wakati wa kikao rasmi cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa cha kumuenzi na kumkumbuka hayati Rais John Magufuli

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa amesema awamu ya 5 ikitamatika tarehe 17 mwezi Machi mwaka huu wa 2021, ukurasa mpya ulifunguliwa wa awamu ya 6 tarehe 19 Machi 2021 kwa kuapishwa kwa Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama.
"Tunajivunia kama taifa na tunashukuru kwamba katika hatamu za uongozi, kwa mara ya kwanza tuna Mwanamke ambaye ni Mkuu, ikiwa ni historia. Rais Samia ni mzalendo na mwanasiasa anayezingatia misingi, ana maono na muumini na muungaji mkono wa ushirikiano wa kimataifa," amesema Profesa Gastorn.
Chini ya uongozi wake, Tanzania itaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Umoja wa Mataifa na misingi yake ambayo ni amani na usalama duniani, haki za binadamu, maendeleo na ustawi wa binadamu, "Rais Samia tayari amechukua hatua za kiuongozi kwa unyenyekevu na ubunifu, kasi na upendo katika kufanikisha ajenda 2030 ya maendeleo endelevu."

"Kwa niaba ya umoja wa mataifa ninatoa pole kwa familia, natumia nafasi hii kuahidi umoja wa mataifa kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali iliyopo chini ya Samia Suluhu Hassan, tuko pamoja na raia wa Tanzania katika juhudi zao za kujiletea maendeleo," amesema Guterrez.
Mwakilishi kutoka Ulaya Magharibi, amesema rais Magufuli alikuwa kiongozi aliyejitoa kwa ajili ya kuwaletea Watanzania maendeleo na kwamba juhudi zake zilitambulika kwa kiwango kikubwa kupitia sekta ya elimu na miundombinu.
Kutambuliwa kwa Magufuli katika ulingo huo wa kimataifa kunajiri wakati huu ambapo pia alama zakea zinajadiliwa nchini humo ikiwemo katika bunge ambapo kunao wanaotaka yote aliyoyaanzisha yasibadilishwe ilhali wengine wana maoni tofauti kuhusu mwelekeo unaofaa kuwa wa nchi hiyo chini ya rais Samia.

Mjadala wa Alama za Magufuli bungeni​

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akitoa maoni yake kuhusu mjadala huo siku ya ijumaa alisema alama aliyoacha ya kiongozi haitetewi, bali inajitetea yenyewe.
Alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameanza vizuri na kwamba yeye kama awamu nyingine za uongozi, "aachwe aandike kitabu chake cha awamu ya sita".
Nape alisema kama ilivyokuwa kwa awamu nyingine zilivyofanya maboresho katika maeneo mbalimbali, naye kama atahitaji kufanya hivyo asaidiwe ili kazi ifanyike.
Aliwaomba viongozi, wabunge na Watanzania kwa ujumla wampe ushirikiano Rais Samia ili aweze kuyafanye hayo. Chanzo. Umoja wa Mataifa wakumbuka mchango wa Magufuli kwa Tanzania. - BBC News Swahili
 
Lissu na genge lake wakipata madaraka kwenye nchi hii, taifa litalia na kusaga meno.

Labda kama taifa ni kina bashiri, pole pole, katelefoni, mataga, bila kumsahau yule kibaka wa mbeya na wale wahitimu maarufu wa darasa la 7.

Hiiiiii bagosha!
 
Salama Wana Mapinduzi wa JF?

Ndugu zangu huko Duniani kwa sasa ni Viongozi wa Dunia wanavyomuenzi Mpendwa Wetu Hayati John Pombe Joseph Magufuli kwa kuelezea Uimara na Misimamo Yake thabiti katika Kuunganisha Taifa Letu na Mapinduzi Makubwa ya kiuchumi.

Link hii hapa chini karibu tufatilie uchambuzi yakinifu unaofanywa kumhusu Mpendwa Wetu JPM.




Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa maarufu kama Baraza la 75 kukamilisha mkutano wake maalum uliolenga kumkumbuka na kumuenzi Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 na kuzikwa Machi 26.

Baraza hilo limechukua hatua hiyo kutambua mchango wa Dkt. Magufuli aliyekuwa kiongozi wa nchi mwanachama miongoni mwa nchi 193 wanachama wa Baraza hilo la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Baraza, Katibu mkuu na wenyeviti wa makundi matano yanayounda Baraza ambayo ni Afrika, Asia na Pasific, Ulaya Mashariki, Ulaya Mshariki, Amerika ya Kusini na Karibea kushiriki mkutano huo akiwemo mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN) Balozi Prof. Kennedy Gastorn jijini New York, Marekani.

Akihutubia mkutano katika kumuenzi Hayati Magufuli, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres amesema, katika kumkumbuka kiongozi, UN itaenzi jitihada zake za kusimamia upatikanaji wa huduma za kijamii na mapambano dhidi ya rushwa.

Ameongeza kuwa aliyekuwa rais hayati Magufuli alijijengea umaarufu katika maendeleo ya miundombinu na viwanda ambayo ni dhana muhimu katika kukuza uchumi sambamba na kufanikisha nchi yake kuingia kwenye nchi zenye uchumi wa kati kabla ya kipindi cha makisio cha mwaka 2025.

Aidha akiendelea kutoa sifa za kiongozi huyo aliyedumu kwa miaka mitano na miezi michache madarakani, Guterres amesema, hayati Magufuli aliwezesha kuongeza idadi ya wanafunzi wapya kujiunga na shule za sekondari sambamba na kuboresha uwezo wa upatikanaji wa nishati ya umeme nchi nzima.

"Kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, kwa mara nyingine tena ninapenda kutoa pole kwa familia ya Rais, Serikali na Watanzania kwa jumla. Tunatambua historia ya ushirikiano uliotolewa kimataifa na kikanda, na ninachukua nafasi hii kusisitiza na kurudia tena kusema Umoja wa Mataifa tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan na tunasimama na wananchi wa Tanzania katika kuendeleza na kusaidia mafanikio ya kimaendeleo kwa Watanzania wote.

Hi mbona ni Tribute kwa rais wa nchi mwanachama anayefariki? Ni utaratibu wa kawaida kwa mkuu wa nchi yeyote.

Ila kwa waliozoea kulishwa propaganda, hapo wanaona ujiko wa pekee.

Lakini....hivi hao si ndio mabeberu? Sasa iweje mabeberu wakiongea kidiplomasia, tunajaa shangwe? Ilhali sisi tunawatukana kila uchao? Hatujiulizi mbona wao wanaongea kistaarabu sana kwa mtu kama Magu ambaye alitumia kila fursa kuwakejeli? Eti yuko kwenye vita ya uchumi. Na nani? Mabeberu hawa hawa? Mambo ya ajabu kabisa
 
Cardinal alisali nae...
Akaanzisha nyimbo... na kuongoza ibada ya kawaida before kufa..

Ndugu wa marehemu said all that.

Sasa hukumu zenu wajukuu wa ibilisi mbaki nazo wenyewe
Hao ndugu wa marehem wenyewe wamekuta mzoga, sasa sijui wamesimulia ndoto?
Meko alikufa kibudu, sahivi huko jehanamu amegeuka makaa
 
Unajua unagombana na kivuli chake JPM?
He is gone bro

Makonda alitusaidia sana kupunguza drugs
Eti kapokelewa na yesu, wasenge nyie kweli. Drugs mnavuta nyie ambao mnaamini hajafa na kila siku mnamuwaza eti shujaa wa afrika ..mnamuwaza kuliko wake zenu mbwa nyie
 
MWEZI MMOJA BILA MWAMBA;BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA LAMUENZI HAYATI DAKTARI JOHN POMBE MAGUFULI.

Leo 10:40hrs 18/04/2021

Ni heshima kubwa sana kiitifaki katika Baraza kuu la Umoja wa mataifa kumuenzi Rais wa nchi aliyefanya mambo makubwa kwa nchi yake lakini akatutoka akiwa Madarakani,kikao cha kumuenzi Hayati Rais John Pombe Magufuli kiliandaliwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kikiudhuriwa na Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Viongozi wa kikanda wa Umoja wa Mataifa,ni heshima kubwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupewa heshima hiyo kubwa na Umoja wa Mataifa.

Heshima ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli imetolewa mwezi mmoja tangu kufariki kwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 17/03/2021,Umoja wa Mataifa ilishusha bendera nusu mlingoti wakati wa maziko ya Hayati Daktari John Pombe Magufuli na Jana tarehe 17/04/2021 imeendelea kumuenzi Daktari John Pombe Magufuli kwa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kukutana na kuenzi maisha ya Hayati Daktari John Pombe Magufuli hapa duniani na mambo mema aliyoyafanya Daktari John Pombe Magufuli kwa dunia,bara la Afrika akiwa Mwenyekiti wa SADC na kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utumishi wake kwa nchi ya Tanzania.

Umoja wa Mataifa umeutangazia Ulimwengu kuwa hapakuwahi kuwepo Rais katika Afrika tangu kuondoka kwa uzao wa akina Kwame Nkrumah,Nelson Mandela na Julius Nyerere mwenye kariba,maono,uhodari na Uzalendo kwa nchi yake kama Hayati Rais John Pombe Magufuli,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitaja moja ya Jambo la kukumbukwa alilofanya Hayati Rais John Pombe Magufuli ni kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati miaka 4 kabla ya muda uliotarajiwa yaani 2025,pia alisema katika awamu ya Rais John Pombe Magufuli mchango wa kulinda amani la jeshi la Wananchi wa Tanzania uliongezeka mara dufu katika Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika salamu zake kumkumbuka Rais John Pombe Magufuli alisema wanatambua utumishi uliotukuka wa Rais John Pombe Magufuli,alisema Hayati Rais Magufuli alipambana kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana na kukabiliana na vitendo vya rushwa ambavyo vilikuwa vimeshindikana,Katibu Mkuu huyo alisema Rais John Magufuli alipata umashuhuri kwa maendeleo ya miundo mbinu ambayo ni zana muhimu katika maendeleo ya kiuchumi kufikia uchumi wa juu, Tanzania ilifika azma yake ya kuwa nchi ya kipato cha kati miaka minne kabla ya lengo lake la 2025,

Thamani ya miundo mbinu tunayoiona,thamani ya miradi mikubwa tunayoiona Bwawa la Umeme,Ununuzi wa ndege,ufufuaji wa atcl na ttcl,Ujenzi wa barabara nane,Ujenzi wa Daraja la Tanzanite na Daraja la Busisi,Ujenzi wa meli kubwa tisa,pato la taifa la trillioni 1.8 kwa mwezi alilokuwa akikusanya Rais John Magufuli,thamani ya huduma za jamii alizozianzisha Ujenzi wa Zahanati 400 nchi nzima,Ujenzi wa masoko mapya katika mikoa yote 30,Ujenzi wa vituo vipya vya mabasi katika mikoa yote ya Tanzania,ukijumlisha thamani ya hayo yote ukagawanya na idadi ya Watanzania Milioni 60 utapata kipato cha dola 2300 ambacho kimetuingiza Watanzania katika uchumi wa kati.

Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Hayayi Rais Daktari John Pombe Magufuli wa Tanzania ilitekeleza miradi mikubwa ya kimkakati iliyobuni ajira kwa Watanzania wengi kama mradi wa SGR kutoka Dar hadi Morogoro na kutoka Morogoro hadi Dodoma na tayari mradi mpya umeanza kutoka Tabora hadi Mwanza,mradi mwingine ulioajiri Watanzania wengi ni mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere ambalo likikamilika litatoa fursa ya kilimo cha umwagiliaji cha mpunga kitachozalisha zaidi ya tani laki mbili na kuuza duniani kote,ni kati ya vitu ambavyo viliivutia Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kama taifa lenye kipato cha kati,

Mbali na uongozi thabiti wa Rais John Pombe Magufuli katika kudhibiti matumizi ya fedha ya umma pamoja na kupambana na wale wanaotaka kufuja fedha ya umma, taifa la Tanzania limeimarika kiviwanda, Serikali ya CCM ya awamu ya tano imefanikiwa kuanzisha zaidi ya viwanda elfu nane katika kipindi cha miaka mitano,Benki ya Dunia, WB, tarehe 1 Julai 2020 ikaiorodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa kipato cha kati, Shukrani kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli na hivi leo tunamuenzi kwa mema yake aliyoyafanya enzi za uhai wake hapa duniani.

Luka 19:40

Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.

Nami nasema Huyu mwamba Daktari John Pombe Magufuli amefanya yaliyoshindikana,Ushindi wa ccm kuanzia serikali za mitaa vijiji na vitongoji,udiwani kata zote bara na visiwani,ubunge,hii alama ni ngumu kufutika,ninukuu ilani ya CCM 2020-2025.

"Ni ukweli usio na shaka kuwa, ili CCM iendelee kukubalika na kuaminiwa na wananchi na kupewa ridhaa ya kuongoza nchi yetu, upo muhimu mkubwa kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, kuwa karibu na wananchi kwa kuwatembelea, kusikiliza kero zao na kushirikiana nao katika kuzipatia majawabu. Ni muhimu pia kwa CCM wakati wote kuwa kimbilio, msemaji na mtetezi wa wananchi wote na hasa wanyonge. Hii ni muhimu kwa kuwa, kwa asili yake, CCM ni Chama cha wakulima na wafanyakazi kinachowatetea wale ambao sauti zao sio rahisi kusikika."
ILANI YA CCM YA MWAKA 2020: 2025


Ndugu zangu ukwel ni mmoja tu ili CCM iendeleee kuaminiwa na pengine kuongeza Wanachama njia ni moja tu Serikali Kuu kutekeleza ilani ya CCM kama ilivyoandikwa na kunadiwa Tanzania nzima na Hayati Daktari John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan na utekelezaji wa miradi yote ambayo imeanzishwa na Hayati Rais John Magufuli ikiwa sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa Watanzania,miradi hiyo isimamiwe kwa bidii na iishe vinginevyo 2025 tutapigwa usoni na Watanzania kwa kutumia Ilani yetu tunayoishika mkononi bila kuitekeleza.

Alale pema peponi Rais John Pombe Magufuli,Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki Rais wetu mpya,Mama Samia Suluhu Hassan.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom