Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 52,334
- 70,330
Tuungane kutokomeza haya mauaji mkuu kabisa aisee...inatisha sana
Mkuu wao kazi kuwataka watu kuomba amani na kuhubiri amani amani ipi hiyo wanayohubiri bila haki?Viongozi wa uamsho wako jela labda tuwaulize maaskofu na mapadri wako wapi?
Ingekuwa kuna maaskofu wapo gerezani wangejitokeza.Unataka maaskofu watetee, lini imeripotiwa kwamba padre au askofu ameuawa? Kila nyani achunge mkia wake!
Sio kumkosoa tu.Atiii? Pengo amkosoe Magu?
Ni kutafuta mkia. wa Chura
Kanisa la leo limeacha kutetea ukweli,wao wanaangalia makusanyo yao ya sadaka,kanisa linaangalia maendeleo ya vitu,kama majumba ndege barabara za juu na maendeleo ya majengo mazuri mazuriNaandika hapa nikiwa kwenye hali ya wasiwasi mkubwa sana maana hali si nzuri hakika.
Mengi yamefanywa na watawala awamu hii hapa sitoyaorodhesha maana yanafahamika vizuri tu lakini mengi ya hayo yameumiza sana raia sababu yanaminya haki za msingi za raia.
Wapo walojaribu kuzungumza kwa kushauri watawala lakini waliishia kulala ndani ya kuta za mahabusu huko, wengine kutishiwa kuuawa nk, wanaamua heri wabaki kimya kwa uoga wa kuuawa.
Mauaji yanayoendelea huko pwani Kibiti, Mkuranga na Rufiji yatatumaliza maana takwimu zinaonesha hadi sasa raia wasio na hatia zaidi ya 30 wameshauawa kwa kupigwa risasi na kile kinachoitwa 'watu wasiojulikana' wakiwemo askari polisi 13 na nilimskia ndugu rais John Magufuli akiwa ziarani huko pwani akiwaomba hao watu wauaji 'wasiojulikana waokoke', na hatujui kwa hakika inaezekana kwao kuokoka si lazima na sio kipaumbele chao sasa si tutakwisha!
Tegemeo la raia limebaki kwa viongozi wa dini hawa ni Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania [Tanzania Episcopal Conference - TEC], Mashehe na maaskofu wa madhehebu tofauti Tanzania na wachungaji wote kupaza sauti zao katika kuwataka watawala wachukue hatua kudhibiti na kuzuia mauaji haya kuendelea tu kutokea hali ndugu na jamaa zetu wapenda wanaendelea kupoteza maisha huko Pwani.
Lakini chakuskitiza zaidi hawa viongozi wa dini wako kimya tu hata tamko na waraka hakuna kutoka kwao hivi hadi afe nani ndiyo mtatoka na kutoa waraka na matamko?
Mchungaji mwema anawachunga na kuwalinda kondoo wake na kuhakikisha wanabaki salama siku zote.
Mauaji haya yanayoendelea hao kondoo wanaezaje kuskia na kuuata mafundisho yenu ya dini hali wanasakwa na kuwindwa ili wauawe kwa kumiminiwa risasi na walengaji shabaa bila huruma na hakuna mtetezi?
Tunamkumbuka mchungaji Rev. Martin Luther King Jr. kwa kupigania amani duniani na upendo wa watu wote pasi na ubaguzi hadi alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel [Nobel piece prize] na kwa hakika dunia haitoeza kumsahau kwa mchango wake na alivyojitoa kwa watu nawaomba muige mfano wake.
Mwingine ni askofu Desmund Tutu wa Afrika ya kusini na huyu pia aliwahi kushinda tuzo ya Nobel na aliwahi kusema nanukuu '
If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor' tafsiri kama unakuwa kimya tu na hauna upande kwenye uminywaji wa haki basi wewe umeamua kuchagua upande wa yule mvunja haki.
Ni nani wa kuwatetea ndugu Watanzania hawa wanaoteseka na kuuawa kila uchao? ni nani huyo na yuko wapi?
Mungu ibariki Tanzania na wote waliouawa kwa kupigwa risasi nao wametutangulia mbele ya haki.
Mwanaharakati mie herikipaji.
Naandika hapa nikiwa kwenye hali ya wasiwasi mkubwa sana maana hali si nzuri hakika.