Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 339
- 705
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwenye mazingira ya Jiji la New York nchini Marekani, Wanandoa Wawili (Nova na Reemo Styles) walijikuta na Wageni wachache harusini kutokana na kuweka Kiingilio cha zaidi ya Tsh. 700,000 kwa kila mwalikwa.
Uamuzi wa kuweka kiwango hicho ulitokana na wao kubaini gharama za sherehe yao ni zaidi ya Tsh. Milioni 350, pesa ambayo ilikuwa nyingi sana kwao kuitumia kwaajili ya sherehe tu.
Mwisho wa siku walipata Wageni 60 tu ambao walilipa na kujumuika nao ambapo huduma walizopata ni kutembezwa katika Jiji la New York kwa Basi la Ghorofa lenye uwazi eneo la juu pamoja na Chakula cha jioni kilichokuwa na Mapande ya Steki na Vyakula vya Bahari au Sea Food mnaita.
Baada ya Sherehe za Harusi kuisha Wanandoa hao walifanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh. Milioni 170 ambazo waliamua kuzitumia kuanzisha miradi ya familia yao.
Inaelezwa kuwa gharama za Harusi nchini Marekani tena kwa Harusi ambazo hazifanyiki ukumbuni na hazina Wageni zaidi ya Ndugu ni kati ya Tsh. Milioni 13 hadi Milioni 70. Kama utataka ifanyike katika Jiji la New York basi mfuko lazima ukutoboke, yaani hapo hamna hamna uwe na Tsh. Milioni 100
Na gharama kubwa zaidi ni Ukumbi pekee ambao huchukua takriban 37% ya pesa zote.
Kibongo bongo hapa ukiwekwa kwenye Group la Michango huwa unajisikiaje mdau?
Tema sumu kwenye comments hapo.