Uliwezaje kufungua mnyororo wa umaskini kwenye miaka yako ya 30?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,825
6,057
Nilipokua mdogo nilisema nikiwa mkubwa nitapata pesa, nitakua nawasaidia masikini, ila mpaka sasa hivi najiona Mimi ndio maskini mwenyewe ninayepaswa kusaidiwa kabisaa, sijafika 30 lakini nina approach 30, naona kama game ni gumu sana,
Inabidi nikae chini zaidi nifanye meditation nijue nimekuja kufanya nini duniani, maana nikisema utajiri naona kama hamna kabisa😁.

Watu wazima wenye miaka 40 -70 wasiokua na pesa ni wengi tu lakini kiukweli sitaki kua Miongoni mwao, ila kuna kitu nakiona kwenye maisha ukitaka vitu vizuri lazima ufanye juhudi, pia usubirie saana (uvumilivu ndio muhimu), japo wengine wanazaliwa na bahati tu, kila akifanya kinaenda lakini wengine lazima tupiganishe saana.

Mfano, nilishawai kuuza vitunguu sokoni ilala sokoni, gunia moja lilikua linachukua week mbili haliishi mpaka vitunguu vinanyauka, lakini wengine wanauza gunia moja kwa siku,

Mifano ya kupambana ni mingi sana, ukisema uingie shambani utakuta wapo waliofanikiwa kwenye mashamba, ingiza wewe uone moto, lakini je tutaacha kufanya? Lazima tuendelee kupigana na kupambana mpaka mwisho.

Hii dunia ninavyoiona, haitaki mazoea na watu maskini kabisaa, yaani lazima utapata matokeo ya umaskini.

Tusichoke tu, tuendelee kupambana.
 
Yeah brother never give up
 
Umaskini ni nini?

Kwa mfano mvuvi anaishi Kilwa au Mafia, anavua samaki wake anauza kwenye soko lao anapata pesa ya kula na kusomesha watoto wake, anaishi nyumba ndogo inayomtosha ina umeme, hana gari na wala haliihitaji kwa shughuli zake, je huyu ni maskini?? Pengine ana shamba kijijini analima heka 3 za mazao ya chakula, anatumia simu ya kitochi. Hana mali pengine na wala haziihitaji je huyu ni maskini? Lakini ana furaha.

Umasikini ni dhana ambayo ukifuatilia sana wanaoonekana masikini mara nyingine sio bali ni mtazamo tu au "definition".

Kuna mwingine yupo dar ni muajiriwa anaishi sinza, ana gari alilokopa benki, ana smart phone, lakini pia analipa kodi ya nyumba laki 6 kwa mwezi, anapambana kukutanisha mishahara kutokana na gharama kubwa za maisha je huyu na wa kilwa yupi maskini? Ana kiwanja 20×20 mapinga anakitembelea mara kwa mara ila hajafanikiwa kujenga. Hana furaha kivile mpaka alewe anapambana na changamoto za jiji.

Yupi maskini kati ya hawa??
 
sanihihi kabisa kusema umaskini na usio umaskini unakamilshwa na mitazamo ya tunao utazama .

Ingawa ujumla wa yote umaskini ni mbaya sana , kama zipo njia mbele yako za kuukabili umaskini usiache kuiendea.
 
usipime mwanangu life 2002 napewa mchongo na r.i.p rafiki angu kuuza nguo minadani karatu jamaa alikuwa na kama mtaji wa 150...mi nikiwa na wa 25. ukapanda mpaka 40k..tulikuwa tunapanga nguo karibu jamaa alikuwa anauza mizunguko ya kutosha mimi bado hata mmoja..kumbe location ilikuwa inambeba na yeye ni mzoefu(so suala la kuuza sana komaa ipo siku yako)huwezi kuanza tu na kutusua lbda uwe na research ya mda mrefu na ubunifu kingine ni bahati...sasahivi kuna biashara naifanya vijana wangu wameondoka na kwenda kujipanga watu wanapoingilia na kuifanya mkama mimi...sasa utafanyaje?pambana hama location kuna wengine wako karibu yako wakunyweshe sumu..
 
Back
Top Bottom