Uliumbwa kwa mavumbi na mavumbini utarudi

Hapa ndio penye siri ya dhana ya kifo kwenye mwili uharibikao.

Kwa imani za Mungu mmoja, binadamu aliumbwa toka mavumbini...aliumbwa kinyago mpaka pale alipopuliziwa pumzi ya uhai/kuwekewa roho.

Mungu aliposema natuumbe mtu kwa mfano wetu dhana kuu ilikuwa kwenye ile pumzi ya uhai pumzi ya uzima, uzima wa milele.

Pumzi inayozungumziwa hapa ni ile pumzi ya kimungu ambayo IPO ilikuwepo na itakuwepo milele..haifi wala kuharibika ni pumzi roho isiyokufa.

Ndio maana baadhi ya imani hutumia maneno haya uliumbwa kwa mavumbini na mavumbini utarejea kamwe pumzi yako iliyokutoka haitajwi kwakuwa haijafa bali imerudi panapostahili ama la kwenda pengine popote.

Mungu sio mwili bali ni roho na pumzi ya uzima wa milele ukienda paradiso huendi mwili unaenda roho isiyokufa ukienda jehanam huendi mwili bali unaenda roho iliyobeba ufahamu.

Unapojitahidi sana kuugharamia huu mwili uharibikao kwa nguo na vipodozi vya gharama na karamu za kidunia huku roho ikiwa chafu ni sawa na kujipaka manukato ya bei ghali kwenye mwili mchafu.
Umenena vyema mkuu.
God isn't a physical being
 
Ila kuna watu wanadanganywa kuwa wakifa wanaenda mbinguni
Mara sijui ulale mahali pema peponi
 
Me nakataaa sikubaliani na wewe.... Hakuna binadamu aloumbwa kwa mavumbi tusidanganyane.....

mavumbi ni uchafu mwepec unaokaa kwenye masofa yetu na kuyakung'uta au yanaingia kwenye nywele zote mavumbi hayo hata ukayamata ukayafinyanga uwez kuumba mwasesele a.k.a mdoli.......

binadamu ameumbwa kwa udongo hata ww ukifanya jarbio ukachukua udongo ukafinyanga waweza mtengeneza mtu kitachokushinda ni kuweka roho....

na kugeuza kuwa nyama na ukawa na mambo yote kama binadamu ikwemo moyo figo ini n.k

hapo mwenyezi mungu alivyonesha nguvu yake.

Kwa kutumia udongo bado hata mwanadamu ameweza utumia kufinyanga vitu mbalimbali.

Binadamu kaumbwa na udongo hakuumbwa kwa mavumbi

Tuwekane sawa..kuna kaul zngne watu fulan wamezoea kutamka lkn sio sahihi kuhusu vumbi jamn........

natumai tumelewana..........

siku njema
 
Kinachofanya binadamu aogope kifo ni kuipenda dunia...lakini mwisho wa siku lazima roho iache mwili..
 
Makala yako ina jumla ya Paragraph 7.
Ningekua editor ningefuta paragraph 6 za juu nikabakiza ile ya 7 tuu.
Maana ndio imebeba ujumbe wote.

Qul nafsi will taqrib mauti
 
Makala yako ina jumla ya Paragraph 7.
Ningekua editor ningefuta paragraph 6 za juu nikabakiza ile ya 7 tuu.
Maana ndio imebeba ujumbe wote.

Qul nafsi will taqrib mauti
Hivi kwenye gari unaweza kuondoa kila kitu ukabaki na engine na chassis tu?
 
Back
Top Bottom