Ulishawahi kukosea muamala wa kiasi gani kwenye simu yako?

Dexta

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
1,942
4,806
Habari za jioni wana JF..

Bila kupoteza muda tujikite kwenye mada, ulishawahi kukosea kufanya muamala wa shilingi ngapi kwenye simu yako? Na je, ulifanikiwa kuipata hela au ndio ilipotea mazima.?

Kwa upande wangu, nilishawahi kukosea kutuma kiasi cha elfu themanini ila kwa bahati nzuri ile pesa ilienda kwa mzee mmoja hivi sikumbuki alikuwa mkoa gani.

Ila baada yakuongea nae akaniambia hata hajui kama kuna hela imeingia so akaniambia nisubiri mpaka kijana wake aje maana yeye ndio huwa anamsaidia kusoma meseji, alikuwa amemuagiza sehemu.
Yule kijana alivyorudi kweli wakanipigia simu na wakanirudishia ile hela, ikanibidi niwatumie elfu 20 kama shukrani.

WAAMINIFU BADO WAPO.

Vipi kwako mdau ulishawahi kukosea muamala wa shilingi ngapi na ulifanikiwa kuipata hela au ndio ilipotea jumla..?
images (4).jpeg
images (5).jpeg
 
Kwenye mfuko kulikuwa na elfu 10 na 2000.
Wakati wa KUTOA sadaka nikakunja ngumu langu nikajua nimetoa 2000.
Natoka kwenye Ibada jikaagiza ugali samaki 4500 Ili nikirudi getto nianze kazi za usafi.

Nimeshiba natoa hela ni buku mbili... Hahahaha waaminifu Bado wapo. Nilimwambia yule mama chukua hii 2000 hela ingine nitakupitishia wiki ijayo.

Akaniambia msema kweli mpenzi wa Mungu kama huna sawa utaleta.

Wiki iliyofuata nikapitisha hela yao. Waaminifu na wenye Imani wapo
 
Elf 95 tu nilikosea kwenye lipa namba ikaenda kusikojulikana. Nikapiga simu vodacom chap, wakazuia. Nikaambiwa next time niwe makini. Na niko makini kweli kweli
 
Ehee nishawahi kukosea kutuma elf 30 kwa mlengwa 😁😁. Lengo nimtumie second born. Pale kwenye Fav contacts nikaclick namba ya third born pasipo kujua afu kibaya zaidi 2nd born alitumia NIDA yake kumsajilia 3rd born laini, so niliona jina nika confirm muamala.

Nilikuja kushtuka baada ya kuona sms ya 3rd born kanasema huna baya tajeerr na makopa mengi ndo kushtuka 😁 nikavunga sikumwambia km nmekosea, nisishushe brand dada mkubwa nikamwambia boom likitoka unarudisha
 
Back
Top Bottom