Ukweli uliofichwa: Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa ya kulevya

Setfree

JF-Expert Member
Dec 25, 2024
2,799
3,845
Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.

Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).

Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe

Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.

“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”

Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”

Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).

Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)

Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.

Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)

So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.
 
Yesu asingeweza kutengeneza divai ya kuwafanya watu wapige yowe, wagombane na kupata majeraha.

Mithali 23:29-35
"Ni nani wapigao yowe? Ni nani wenye huzuni? Ni nani wenye ugomvi?
Ni nani walalamikao? Ni nani wenye majeraha bila sababu? Ni nani wenye macho mekundu? Ni wale ambao hawabanduki penye divai, wale wakaao chonjo kuonja divai iliyokolezwa. Usiitamani divai hata kwa wekundu wake, hata kama inametameta katika bilauri, na kushuka taratibu unapoinywa. Mwishowe huuma kama nyoka; huchoma kama nyoka mwenye sumu. Macho yako yataona mauzauza, moyo wako utatoa mambo yaliyopotoka. Utakuwa kama mtu alalaye katikati ya bahari, kama mtu alalaye juu ya mlingoti wa meli. Utasema, “Walinichapa, lakini sikuumia; walinipiga, lakini sina habari..."

Yesu asingetengeneza divai ya kuwafanya watu wapatwe na madhara hayo.
 
Kumbuka, shetani anapenda kuchanganya ukweli na uongo. Anatumia mfano wa divai ya Yesu ili kuwadanganya watu wajione wako salama katika dhambi. Huo ni mkakati wa kupotosha.

Katika Walawi 10:9 Mungu aliwaambia wana wa Haruni, wasinywe mvinyo wala kileo wanapoingia kwenye hema ya kukutania(hekaluni). Sisi pia ni hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 6:19), hatupaswi kunywa pombe.

Pombe imekuwa chanzo cha maumivu kwa familia nyingi. Imesababisha ugomvi katika ndoa, watoto kukosa malezi bora, ajali za barabarani, magonjwa kama cirrhosis ya ini, na hata vifo. Watu wanapolewa hupoteza utu wao, heshima yao, na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.

Yesu asingeweza kutengeneza divai inayoleta madhara hayo makubwa.

Kwa hiyo ndugu yangu, usikubali udanganyifu wa shetani na manabii wake wa uongo wanaosema eti "hata Yesu alitengeneza pombe." Yesu alileta uzima. Alikuja kuvunja minyororo ya ulevi na dhambi nyingine.
 
Kama umefungwa na pingu au minyororo ya ulevi, ni vigumu kujinasua kwa nguvu zako mwenyewe. Inawezekana hupendi ulevi, lakini kila ukijitahidi kuacha kunywa pombe, unashindwa. Yesu anaweza kukufungua vifungo hivyo na kukupumzisha mzigo huo wa ulevi, kama utakubali leo kuokoka. Ukiokoka, hautasikia tena hamu ya pombe.

Kama unapenda kuokoka na kuwa na nguvu ya kushinda ulevi na dhambi zote, tafadhali omba (kwa kufuatisha kwa moyo wako wa dhati) sala hii ya toba. Omba hivi:
“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi hii ya ulevi na dhambi zangu zote. Naziacha kabisa kuanzia leo. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda ulevi na dhambi zote. Niwezeshe kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na uongo wake. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Tayari umepata neema na nguvu ya kushinda ulevi na dhambi zote. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri na wokovu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea kiroho.

Please, share uzi huu kwa wengine wanaoteswa na ulevi.
 
Pombe1.jpg

Yesu asingeweza kutengeneza divai itakayowafanya wanywaji wapate madhara kama hayo
 
Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.

Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).

Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe

Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.

“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”

Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”

Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).

Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)

Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.

Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)

So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.
Ku-hamba kwingi???

Endeleeni kuedit tu for your own benefits
 
Bado Sana Kuelewa Maandiko.

Nipe Tofauti ya Divai Aliyokunywa Nuhu mara baada ya Kuokol3wa gharikani na Aliyotengeneza Masihi Yesu.

Pili Kumbukq Maandiko yote uliyoyaweka Yamezungumzia Ulevi na si Unywaji wa Divai.

Na Andiko La Harusi Mjini Kana Halitumiki Kuhalalisha Ulevi, Bali Utukufu wa Muujiza Wa Bwana Wetu Yesu Masiha.
 
Ikishaitwa divai maana yake kuna kilevi tayri...
Safi sana ndugu yangu Otorong'ong'o ,
Umeibua point inayowachanganya watu wengi.

Iko hivi: Biblia ya Kiswahili imetafsiriwa kutoka kwenye lugha za asili.

Kwa Kiswahili, neno “divai,” kwa walio wengi linamaanisha kileo. Lakini katika Biblia ya Kiebrania, neno lililotumika ni "yayin." Neno hilo linamaanisha aina tofauti za juisi ya zabibu—iwe mbichi, iliyochemshwa, au iliyochachuka. Zote zinatumia jina moja tu(yayin). Muktadha wa matumizi ya jina hilo ndio unaotofautisha aina ya juisi, sio jina lenyewe. Ndio sababu katika Yohana 2:10 yametumika maneno "divai njema" kuitofautisha divai ya Yesu na aina nyingine za divai yenye kilevi.

Katika maandiko ya mwanzo, watu waliweka juisi ya zabibu kwenye viriba na kuichemsha ili isiweze kuchacha—bado waliiita "yayin"(divai). Pia, katika baadhi ya maandiko, divai mpya (new wine) ilikuwa tu juisi ya zabibu iliyotolewa kutoka shambani. Hivyo basi, sio kila palipoandikwa “divai” panamaanisha kinywaji chenye kilevi kama unavyoelewa wewe.

Labda mfano unaokaribiana na maelezo hayo ni neno "maziwa." Maziwa yanaweza kuwa ya moto, ya baridi, yaliyochacha, ya mgando au fresh. Jina ni lile lile, lakini hali ya maziwa inategemea muktadha.

Narudia tena, Yesu hawezi kutengeneza kinywaji chenye kuwafanya watu walewe halafu aseme kwamba walevi hawataurithi ufalme wa Mungu.
1 Kor 6:9-11
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi."

Mpaka hapo hakuna point inayohalalisha unywaji wa pombe. Okay?
 
In vino veritas......hujui kwanini walatin wanakaelewa haka kadude cha zabibu
Huo msemo (In vino veritas) hauna mashiko. Pombe inapunguza udhibiti wa akili (inhibitions).
Alcohol inafanya kazi kwenye mfumo wa fahamu kwa kupooza sehemu ya ubongo inayodhibiti tabia. Hiyo inaitwa prefrontal cortex. Hiyo sehemu ndiyo inayokusaidia wewe kufikiri kabla hujasema au kufanya jambo.

Ukiwa mlevi, hiyo "kinga ya udhibiti" inazimwa—hivyo unajikuta unasema au kufanya mambo ambayo kwa kawaida unayaficha au kuyaonea aibu.

Ndiyo maana Biblia inasema:
"Mjinga hutangaza hasira yake yote, bali mwenye hekima huiweka akilini." (Methali 29:11)

Mtu akilewa anakuwa kama mjinga tu. Anaweza kufanya hata mambo ya aibu mbele ya watoto wake. Yesu hawezi kutengeneza kinywaji chenye kuharibu mfumo wa ubongo. Nope!
 
Endeleeni kuedit tu for your own benefits
Endelea tu kuukataa ukweli, to your own disadvantage.

"Kwa sababu hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote wasioamini ile kweli, bali walifurahia udhalimu." (2 Wathesalonike 2:11–12)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom