Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 2,798
- 3,843
Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.
Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).
Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe
Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.
“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”
Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”
Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).
Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)
Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.
Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)
So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.