Ukweli tupu; Hadi sasa sijajuta kumpa kura Lowassa

Haya ni mawazo huru! Tujifunze uungwana kwa kusikiliza watu wote hata wale ambao hatujaendananao kimtazamo, binafsi sioni sababu ya kumtukana mtoa mada! Hayo anayoyasema ni mawazo yake huru, kumuita kuwa hana hakili ni kukosa akili zaidi, je ulitaka awe na mawazo yanayofanana na yako?

Katika nchi inayoheshimu azimio la haki za binadamu ni jambo la ajabu mtu kutokuheshimu uhuru wa mtu kuzungumza!

Busara zetu na zionekane katika matendo yetu na kunena kwetu, na pale inapobidi, tupingane kwa hoja na kujenga (kushirikisha nguvu misuri ya ubongo) na si kutukana na kukashfiana.

Binafsi nimemuelewa mtoa maada! Kabainisha kuwa kuna mazuri (machache) na mabaya (mengi) katika awamu hii ya tano! Labda yuko sahihi, ila nadhani awamu hii ya tano haijatimiza hata mwaka mmoja ofisini, yawezekana ni mapema mno kutoa hukumu ya jumla.
Viwavi wanahisi wataishi milele na wasijuwe kuwa yaja kwao saa mbaya ambayo nchi nzima itageuka dodoma, WATASAKWA KILA KONA YA NCHI NA KUTAFUNWA
 
Naanza kuamini kwamba hii nchi ina vilaza na vipofu kupindukia kuamini Lowasa angeweza kuwa Rais wa nchi hii.
 
MwlvNyerere alisema "hatuwezi kama nchi kuwa na rais ambaye hujui kesho ataamka amefikiria lipi" Nadhani tumeanza kumwelewa Mwl sasa
kuna yule mhuni alienda kwa dokta mwaka na mpaka wakapiga marufuku matangazo yake lakini cha ajabu nayaona matangazo yake kwenye luninga yaani hizi mbwembwe zinachanganya kweli
 
Naanza kuamini kuwa nilikuwa sahihi zaidi kumpatia kura yangu ndugu Edward Lowassa.

Kwa hali ya sasa kule Zanzibar, mgogoro wa umeya Dar na Tanga, uamuzi wa "mr. Wakukurupuka" wa kuwatimua watumishi wa umma bila hata kuwasikiliza, uminyaji wa demokrasia na kuminya vyombo vya habari inanipa shaka sana.

Ndani ya siku 100 tu mtani wangu Ngosha kafanya makosa mengi sana, tena yasiyo ya msingi. Japo kafanya mema pia ila yamefunikwa na mabaya kwa kuwa yamekuwa kero kubwa.

Janja janja ya bongo movie ya kuongea mbele ya kamera za TBC, STAR TV, CLOUDS na mic za UHURU na TBC-TAIFA hauwezi kutufumba macho tunaotazama mwendo wa kuvizia na kutunisha misuli wa serikali.

Ndo maana hadi leo sijawahi kujuta ile october 25 kura yangu kumpa laigwanan.
Kura yako iko jalalani imeshaoza, tulia!
 
Endelea kudeki barabara anazoita pale mikocheni.
 
Politically, Lowassa is finished!

Hata wafuasi wa shetani watakuambia uamuzi wao kumfuata shetani ni bora kuliko kumfuata Mwenyezi Mungu! Hii haina maana walichokifanya kina manufaa katika maisha yao yajayo!

Ujinga ni mzigo!

Mmh! hii ni shida.
 
HUNA AKILI
mwenzio anahoja toa hoja sio mahaba sefue ana kashfa bado yupo ikulu na wanadai mwenye ushahid apeleke takukuru kuna watu wamesimamishwa kazi bila hata kushirikishwa takukuru huoni kama ni sheria inayohusu wasio na nguvu na wenye nguvu wanaendelea kupeta? kiukweli utumbuaji majipu ni wa wale wadogo bado ni mchezo tu unachezwa suala la uda hadi leo kimya na washasema kuna gari hazijalipiwa ushuru mbona tra hawajaenda kuziteka? changa la macho bado nchi inaliwa vizur na wakubwa kufukuza watu kazi sio suruhu bado mfumo umeoza!!!!??
 
Kwani kuna mtu kakuomba ujutie?
Ndugu mtoa hoja nakushauri ujipongeze kwa kufanya sherehe kabisa. Uliwaona wagombea ukawapima kwa uwezo wako na ukaibuka na Edo! Sasa ulitaka ujutie nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom