Ukweli ni tiba; Chadema mna kumbukumbu fupi sana, CCM wana Chuki za kudumu.

Mkuu kiukweli kuna kipindi Chadema wanapungukiwa Busara kujidai kuungana na hawa watu kwa kisingizio cha maslahi ya taifa.....

Hivi Imagine mtu kama Makonda anawaunganisha vipi? na kwa lipi? kama sio kuupandisha unafiki wao lifti

Tatizo wanasahau haraka sana
Wanaungana kwenye mambo ya hovyo
yasiyo na faida kwa watanzania
 
CHADEMA niliwadharau pale walipompokea Lowasa na kumfanya awe mgombea tena bila utaratibu maalumu,hakika nawaambia hii dhambi itatutafuna sana,dhambi ya kutudanganya watanzania itaitafuna CHADEMA milele,halafu wanawakaririsha wanachama wafuata mikumbo kwamba in politics there's no permanent enemy or friend..
Walituimbisha wimbo wa lowasa kwa takribani miaka nane..dah..niliwaamini hadi nikiona mbunge au Kiongozi wa chadema anaongea nasisimka mwili mzima..badae wanatuambia wamebadili bia angani na mwenye ushahidi aende mahakamani..hii sinema iliyochezwa kwa miaka nane sitakuja kuisahau hata kufa.
 
Nawashangaa wanaoona kwamba ule uchaguzi wa wawakilishi wetu nje ya nchi kwenye bunge la Afrika Mashariki, eti Chadema imekomolewa. Binafsi naona ni hasara kwa nchi na kama ni kukomolewa basi nchi ndio imekomolewa. Kwani tulikuwa tunawachagua kwenda kuwakilisha Chama cha siasa au nchi?
 
sheiza: Kama nyie mnasimamia haki mbona mnabagua wenye vyeti feki? Wengine mnawafukuza kazi ila wengine mnawapa ukuu wa mkoa?
 
Back
Top Bottom