Ukweli ni kwamba watu wengi wa Dar es Salaam wamezidiwa kipato na watu wa mikoani

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
15,290
44,534
Kijana wa Dar akinunua sabufa, sofa la watu 2, kitanda cha chuma na godoro, akipanga chumba kimoja, choo cha jumuia hapo katoboa maisha.

Wapo vijana waliofanikiwa wakajenga, kununua usafiri na wengine kumiliki biashara lakini wastani wa vijana wanaoishi kwenye chumba kimoja na vikorokoro vyao pamoja ni wengi sana.

Tanzania ilivyokuwa na ardhi kubwa mpaka nyingine imekuwa kama haina mwenyewe lakini kuna kijana hana hata umiliki wa square meter nne za mraba katika nchi hii, kazi kutunza ndevu na nywele tu.

Vijana wengi wa mikoani wana nyumba na mashamba ambayo yanaweza kuwasaidia uzeeni hata kama kwa kiasi kidogo.
 
Kijana wa Dar akinunua sabufa, sofa la watu 2, kitanda cha chuma na godoro, akipanga chumba kimoja, choo cha jumuia hapo katoboa maisha.
Kuishi DSM peke Yake ni Mafanikio sio kila Mtu anaweza kuishi dsm na akaweza hata kupata milo mitatu.

So Mkuu hili jiji sio kila mtu anaweza kulimudu akaingia na akatoka salama hapa DSM ni world cup.
 
Upo sahihi , kadri mji unapokuwa unaongezeka na population inaongezeka , hali ya wengi inakuwa mbaya huishia kuwa servant wa wengine na nguvu kubwa inakuwa inatumika kupigania chakula na malazi , hivyo sio ajabu dar kuwa hivo, ila ni kwa nchi zetu maskini
Kijana wa Dar akinunua sabufa, sofa la watu 2, kitanda cha chuma na godoro, akipanga chumba kimoja, choo cha jumuia hapo katoboa maisha...
 
" Najua hapa utakuwa umefanya reference ya zile takwimu za BOT"

Ni kwel kwamba kwa calculation ndogo tu watu wa dar wanaonekana wana GDP per Capital kubwa kuliko wa mikoani hii nikutokana tu na GDP ya dar kuwa kubwa halaf kibaya zaid imeshikiliwa na watu wachache.

Sasa ikichukuliwa (GDP÷Population)=GDP per Capital kubwa.

So wale wachache matajiri wamebeba wale wengi maskin wasio na hela.
 
Ndizi moja Dar inauzwa 300 wakati huko vijijini unapata sita au tatu.

Means kwa matumizi ya Dar ya mlo mmoja, mtu wa kijijini amekula milo mitatu.

Means hela ya matumizi ya mwezi mmoja, kwa mtu wa kijijini katumia kwa miezi mitatu.

Kuishi DAR ni mafanikio tosha.
 
1. Kibarua wa mkoani na Dar nani analipwa vizuri?
2. Kodi ya chumba cha Dar na mkoani kili ni gharama?
3. Dar na mkoani wapi kuna Fursa nyingi?
4. Dar na Mkoani wapi wakazi wake wanavaa vizuri?
5. Dar na Mkoani wapi kuna huduma za kijamii nyingi?
6. Dar na Mkoani wapi kuna vyakula vingi? sio vyakula vya msimu.

7. Dar na mkoani wapi serikali inakusanya kodi nyingi?
8. Dar na Mkoani wapi kuna TASAF?
9. Dar na Mkoani wapi kuna Upatikanaji wa fedha za kigeni kama Dollar, Euro nk.?
10. Dar na Mkoani wapi vijana wake wamefunga na kuchoshwa na Maisha?
 
Watu Wengi WA mkoan sio kwamba wanaviwanja hapana ,wanakaa Kwao ,uwanja wa nyumbani kapewa kidogo na baba au Bibi au Babu ,acha kusema wanaviwanja ,Mara nyingi wanakuwa hawana hata mamraka navyo wanapewa wajenge waoe hapo hapo ...

Watu Wengi WA mkoani Ni masikini WA kutupwa ,Kwanza wanalima na jembe la mkono ,Hakuna kilimo cha kisasa ,wala mbegu Bora ,Ni wachache Sana wanaolima hata hekari 5 Kwa mwaka ....

Wengi ukichukua mazao waliyolima ( mahindi ,maharage ,viazi ,mihogo ,mbaazi n.k ) hata wakiuza wanaishia kupata Laki 9 ,imagine MTU analima mwaka mzima kutafuta Laki 8 ,,,na hapo Ni calculation za juu wengi wanapata Laki 5 ,then wanarudi shamban Tena kupanda ,jembe la mkono sio mchezo wewe ....

Watu Wengi WA vijijin kilimo Chao Ni small scale ,pesa wanazopata Ni za kuolea ,Kula na kusomesha watoto ,akipata Kingi Ni kuoa mke WA Pili ,hawana exposer na biashara kabisa ,ndio maana hata wakienda sokoni bei iko chini wanauza hivo hivo ....

Wengi mashamba yao Ni ya kupewa na familia ,hivyo basi unakuta hayazidi hata ekari 3 ,....

N.b katika vijiji 5 utakuta watu 4 tu ndio wanauwezo WA kulima Kwa trekita na kilimo cha kisasa ,na MTU Huyo anakuwa kashakaa kwenye kilimo Kwa muda mrefu kanufaika kashajitanua kibiashara ...wengine Ni kilimo local tu hata Laki 4 kuipata Ni miujiza ....kama unabisha nenda kijijini kipindi cha kupanda uone walivo na Hali mbaya ,
 
1. Kibarua wa mkoani na Dar nani analipwa vizuri?
2. Kodi ya chumba cha Dar na mkoani kili ni gharama?
3. Dar na mkoani wapi kuna Fursa nyingi?
4. Dar na Mkoani wapi wakazi wake wanavaa vizuri?
5. Dar na Mkoani wapi kuna huduma za kijamii nyingi?
6. Dar na Mkoani wapi kuna vyakula vingi? sio vyakula vya msimu.

7. Dar na mkoani wapi serikali inakusanya kodi nyingi?
8. Dar na Mkoani wapi kuna TASAF?
9. Dar na Mkoani wapi kuna Upatikanaji wa fedha za kigeni kama Dollar, Euro nk.?
10. Dar na Mkoani wapi vijana wake wamefunga na kuchoshwa na Maisha?
Inategemea unazungumzia mkoani wapi km unazungumzia lindi sawa! Ila mikoa km mwanza arusha hta dodoma tofauti yake na dar sio kubwa sana kulinganisha na mikoa mingine.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mimi hapa asubuhi breakfast nimetumia 1200 mtu mmoja, ningekua bush hii hela ningekula breakfast nzito, mchana ugali na sato mkubwa usiku wali maharage ya kumwaga. Wqtu wa dar tuna mioyo Migumu.
 
Back
Top Bottom