Ukweli mtupu: Abdalah Bulembo na Anthony Diallo wajiandae kuula, waandae sherehe!

Hata ningekuwa mimi ningeteua watu wangu...cha msingi wawe na sifa tu. Tunaongea hapa as if angeingia Lowassa angefanya tofauti kwenye teuzi...wakati Lowassa akiwa mbunge wa Monduli...alishinikiza ndani ya chama mkwe wake agombee ubunge Arumeru wakati ni ukweli kuwa alikuwa hana sifa kabisa. Hakuna mlipa fadhira mzuri kama Lowassa na nawashukuru Watanzania kumkataa....Ikiwa Magufuli angekuwa na sifa ya kulipa fadhira...basi angeanza na Ridhiwani.
 
Halafu kusema Magufuli anahusika na mtoto wa Bulembo kuwa mbunge ni upuuzi na inaonyesha watu hamjui taratibu za viti maalum zinakuwaje. Aibu hii!
 
Haaaah jamani sasa hiyo ni fadhila au mtoto wa watu kapambana mwenyewe kwa uwezo wake mpaka akashinda, au hatujui maana halisi ya fadhila nini?
Watu hawajui nini maana ya viti maalum ndani ya CCM. Badala wahoji kile ambacho CHADEMA ilifanya...kwanza cha kutaka kumpa mama Lowassa ubunge...pili cha kumpa Lowassa nafasi kibao eti za yeye kufanya watu wabunge...zee lilivyokuwa alijitambui limechukua hadi baadhi ya wana CCM na kuwafanya wabunge wakati Wapemba kibao wamekaa kihasara tu!
 
Unaeza kuichukulia kama kulipa fadhila lkni hata ww ungepewa ofisi lazma sekta nyingine ungeweka watu unaowaamini
 
jpm hajawahi kua hawa kada nyumbu wa ccm. wengi wamemfuata edo cdm. fahamu jpm kiitikadi ni ccm asilia...mjamaa mzalendo mwadilifu. tusubiri time will prove me right.



Too good.

They wont understand you.
 
Lowasa angeshinda Sugu angepewa wizara ya Nape, kwa hiyo siyo ajabu tulieni, uchaguzi umeisha.
 
Nitamtafuta hata kuona picha yake, otheryz mwanangu mkubwa wa kiume bado kuOA anaweza kumfaa endapo akimuona alivyo.
Na mwanae naye ni zawadi kwa Wabunge wakware maana nasikia yuko sio haba!
 
Kutokana na hulka aliyoionyesha rais Magufuli (simuungi mkono na sotothubutu kufanya hivyo) basi hawa watu waliokuwa na Magufuli kwenye kampeni kwa hali na mali kwa hakika hatawaangusha! Magufuli ni mlipaji mzuri wa fadhila kuliko kiongozi yeyote yule aliyemtangulia!

Amedhihirisha hilo na kwa hakika hatanii! Wito wangu kwa hawa watu ni kuwa waandae mkao wa kula! Wataula kwelikweli!

Magufuli hajawaangusha washirika wake! Amewabeba kweli kweli! Waliompigania kwenye kampeni wamepewa madonge manonomanono! Wameula baada ya jasho!

Ila wale wa upande wa pili waendelee kusaga meno! Watarajie maumivu makubwa zaidi ya haya!
Kwa hiyo wewe kwa akili zako ulifikiri hatawakumbuka hata wachache? Akili za kitoto zonakusumbua na wivu. Ukikua utaacha.
 
Na hata hao unao amini hawana udhaifu wamelelewa na Ccm .

Sasa sijui kama unaelewa kuwa unacho amini c kila mmja Anakiamini!

Kubali kukubaliana na uwe mzalendo. Mabadiliko yana anza na WEWE

Sijasema wengine hawana Udhaifu au mapungufu hilo la kwanza. Mapungufu ya wengine sio kigezo cha kufanya CCM iendeleze Udhaifu wake na hata wananchi waipe utawala milele. Hata kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu kila mtu ana udhaifu wake na udhaifu wa mtu mmoja una tofautiana na mwingine ndio maana Watu mnaweza kuishi kwenye eneo moja, kazi moja mkatofautiana nguvu za kiuchumi na akili.

Kuhusu Umri au kulelewa na CCM ni mawazo mgando yanayowaumiza wananchi wengi sana. Kwamba ccm imetulea, ccm imetuletea uhuru. Kuwa na mawazo kama hayo ni upuuzi na ufinyu wa mawazo ya hali ya juu. Nitakupa mfano wazazi wako waliokulea utaishi nao na kuwategemea miaka yako yote ukiishi kwao? Unaweza ukalelewa na mzazi wako lakini akakulea vibaya, kuna watoto wamelelwa na wazazi wao vibaya hawakusomeshwa, hawakuvalishwa ipasavyo mwisho wa siku wamejitegemea kwa kuhangaika wenyewe na wamekuwa na maisha mazuri kushinda wazazi wao.
By the way CCM sio mzazi wala mlezi wangu. Ukisema CCM imenilea mimi hao akina JPM,JK,MKP, Rizi 1, Bulembo, Nape,EL na watoto wao watasemaje?
Kuwa na ADABU CCM haijawai kunilea na haitakuja kunilea. Siishi kwa kuitegemea ccm hata siku moja zaidi ni ccm ndio imeni cost vya kutosha kutofikia malengo yangu.
 
Nahisi Diallo hatalipa kodi kwa miaka 10 ya Magufuli... pia anaweza ambiwa asajili kampuni ya UJENZI HARAKA SANA, ATAPEWA TENDA KUBWA ZA UJENZI WA BARABARA YA MABILIONI NA MABILIONI... huyo ni Diallo..

Pia Bulembo huenda akawa Mnikulu... subirieni muone...!! Wakati Bulembo ni std 7...
Mwanae kibinti kidogo 20 yrs kashapewa ubunge... hata shule hakumaliza...

Hii ndio Tanzania....
 
Ni ujinga kuacha watu wenye sifa na badala yake ukateua watu eti kisa walinisaidia ktk propaganda wkt wa kampeni. Ifike mahali kiwepo chombo cha kuthibitisha teuzi zinazofanywa na mkuu wa nchi ili ku
Hapa dawa ni KATIBA YA WANANCHI tu, na sio chombo wala tume.
 
Tangu FISADI Wenu apigwe chini MMEKUWA MNAWAYAWAYA SANA Mpaka HURUMA.............................
 
Back
Top Bottom