Inajulikana tayari, CCM imekwapua ushindi wa CUF ili itimize lengo la kuipitisha ile Katiba ya Chenge/ Sitta. Kwa maneno ya Pro-pesa Lipumba, "Katiba ya ma-intarahamwe".Maalim alipewa nafasi ya kushiriki uchaguzi ili kuhakikisha kwamba alishinda kama alivyodai, akasusa! Maalim ni Bingwa wa kupoteza muda wa wenzake. Uchaguzi umeshakwisha. Sasa tunajenga nchi!
Lakini pia CCM kukubali kuachia madaraka Zanzibar ni kaburi la CCM kwa utawala wa CCM bara(Tanzania). Pia CCM kung'ang'ania serikali mbili 2 ndio njia inayokamilisha ule mduara ambao CCM Zanzibar inaitegemea CCM bara na CCM bara inanuafaika kutokana na kuibeba CCM Zanzibar na kuisimika madarakani.
Naomba ili kufahamu mduara (cycle)huo na mazingaombwe ya CCM na serikali mbili soma hizi mada:
Link Kura Ya Maoni Na Hatima Ya Muungano
Link2. CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano
Link3. CCM: Mwaka 1993 Tanganyika Ruksa, Mwaka 2014 Tanganyika Sio Ruksa
Link4. Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla
Link5. Tuache Kuwatisha Wazanzibari Kuhusu Udogo wa Taifa Lao na Hatima Ya Muungano
Link6. Mdahalo: Kipi Ni Sumu Ya Muungano - Je, Ni Kwa Kuikataa Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Tanganyika?
Link7. Hoja Mbadala: Katiba Ya Muungano Kuja Kabla ya Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara) ni Makosa!
Je mgogoro anaouleta Lipumba (ndani ya CUF na hatimaye UKAWA) akisaidiwa na Msajili wa vyama na mkono uliojificha una agenda kubwa na pana zaidi?