Ukweli kuhusu uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TIC

Ndugu Wanabodi,
Tangu kutenguliwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa TIC Bi Kairuki, kumekuwepo na mjadala mkubwa wenye kutoa hoja na uchambuzi wa aina mbalimbali wengine wakimtetea na wengine wakimponda,ilimradi kila mtu na fikra zake.

Katika mijadala yote, kwa bahati mbaya msingi wa maoni yaliyotolewa uliegemea kwenye taarifa za uwongo na potofu ambazo zimetolewa aidha kwa makusudi au kwa kutofahamu.

Mimi sitoingia kwenye mtego wa kuingia mjadala, bali nitakachofanya ni kuwasaidia wanaBodi kuwaelezea taarifa zipi zilizotolewa kwenye mitandao sio za kweli:

1) Sio kweli kwamba Bibi Kairuki alifuatwa na Rais Kikwete afrika ya kusini na kuombwa kurudi nchini kuja kufanya kazi TIC na akaahidiwa kiwango chochote kile cha mshahara.

Ukweli ni kwamba mwaka 2012, nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TIC ilitangazwa baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Bw Ole Naiko kumaliza kipindi chake cha Uongozi.

Awamu ya kwanza ya Usaili wa nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa TIC ilifanywa na Kampuni ya KPMG kwa niaba ya Bodi ya TIC. Na awamu ya pili ya usaili ilifanywa na Bodi yenyewe ya TIC. Bibi Kairuki alisailiwa kwenye awamu zote mbili na kushinda usaili huo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania Investment Act ya mwaka 1997 kifungu cha 10, Mkurugenzi wa TIC anateuliwa na Rais, hivyo baada ya kufaulu usaili jina la Bi Kairuki lilipelekwa kwa Rais ili amteue kama Sheria ya TIC inavyoelekeza.

Kwa mantiki hiyo taarifa zilizotolewa kwamba Bi Kairuki alitafutwa na Rais aje kusaidia TIC na kwamba alikuwa analipwa usd 18,000 na JK akamuahidi atamlipa alafu baadaye wakageuka hazina chembe hata moja ya ukweli.

Wanabodi,
Tuepuke kuendesha mijadala kwa kutumia taarifa ambazo hazijathibitishwa. Kwa wanahabari ni vema wakafanya kazi yao kwa weledi. Maadili ya fani ya Habari yanawataka kuipokea taarifa iliyotolewa na Serikali na kuitoa kwa umma kama ilivyotoka. Kitendo cha kutia chumvi na kukoleza taarifa kwa habari za uwongo sio sahihi. Kwa mtu mwenye kutaka kupata ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa, vipo vyombo vinavyohuika vinavyoweza kutoa maelezo sahihi kuhusu suala hii. Navyo ni Wizara ya Viwanda na Biashara na Bodi ya TIC.
Mkuu Namtumbo, kwanza asante kwa hii!, uwongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa, unageuka ukweli!, hivyo haya usemayo ndio ukweli wenyewe, na ushahidi ni huu hapa kutoka kwa mwajiri wake!.
Msikilize Mizengo Kayanza Peter Pinda, Anasema Nini Kumhusu Julliet Kairuki!.

Wanabodi,

Tangu huyu mama ametumbuliwa jana, kumekuwa na uwongo mwingi kwenye magazeti na mitandao ya kijamii , haswa kuhusu jinsi alivyoipata hiyo kazi ya Ukurugenzi Mkuu wa TIC!.

Naomba usikilize from the horses mouth, jinsi Julliet Kairuka alivyo patikana!, jinsi alivyofanyiwa 5 test kabla ya kupewa hiyo kazi, na jinsi mwajiri huyu alivyompongeza kwa kile alichokifanya pale TIC.



Paskali
 
taarifa rasmi ndio hii unatoa wewe au na wewe yako ni udaku. hebu tueleze kama wewe ndio mtoa taarifa rasmi, tumeambiwa alikua hapokei mshahara sasa tuseme alikua anafanya kazi bure?
Labda ni msemaji wa Boss wake Kairuki
 
Umeandika mengi ambayo msingi wake ni zile taarifa mbili. Moja ni utetezi wa Kairuki na nyingine ni iliyofichua kuwa alikuwa anajilipa posho ya 25M per month na kufanya safari kibao nje ya nchi. Hujaeleza hoja iliyopo kwenye ile barua ya kutumbuliwa kwake kwamba hakuwahi kuchukua mshahara tangu aajiriwe. Nini hasa kilimfanya asichukue mshahara huo?
mkuu kumbe kuna wakati akili zako huwa zinarudi, mi nilidhani utamtetea.
 
Back
Top Bottom