Ukuta wakatisha uhai wa watoto wawili wa familia moja

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,173
1611679659420.png

Watoto wawili wa familia moja wamefariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba chanzo kikitajwa kuwa ni mvua inayoambatana na upepo iliyonyesha wilayani Geita juzi Jumapili Januari 24, 2021.

Waliofariki ni Asheri Malima(4) na Laurencia Malima (2) waliokuwa wakiishi kijiji cha Kasesa kata ya Kaseme.

Akizungumza leo Jumanne Januari 26, 2021 baba wa watoto hao, Malima Kengere amesema aliwaacha wanae tisa nyumbani na kwenda kuuza mahindi ya kuchoma lakini mmoja wa watoto wake alimfuata na kumueleza kuwa nyumba yao imeanguka.

Amesema wakati ukuta ukianguka watoto hao walikuwa wenyewe nyumbani.

“Walipoona ukuta unaanguka walikimbia lakini hawa wawili walikuwa wadogo hawakuweza, walifukiwa na kifusi,” amesema akibainisha kuwa siku hiyo mvua ilinyesha kuanzia saa nane mchana hadi saa 10 jioni.

Mmoja wa watoto walionusurika, Leokadia Malima amesema akiwa sebuleni alisikia kishindo cha jiwe alikimbia na aliwaona wadogo zake lakini baada ya ukuta kuanguka alibaini kuwa wapo waliokuwa wamebaki ndani.

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Hendry Mwaibabe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wazazi kuwa waangalifu hasa nyakati za mvua ili kuepuka majanga yanayoweza kuzuilika.
1611679534673.png
 
Duh mzee malima hatari watoto tisaaaaaa. Mama yao hajatajwa popote pale alikua wapi?

Anyway Rest In Peace little Angels
 
Pumziko La Amani wapate Watoto.

Watoto tisa Mzee anauza mahindi ya kuchoma,Raisi Obama ana Watoto wawili tu....sijui anaogopa nini?
 
Back
Top Bottom