Ukraine inalipa gharama kubwa sana za vita kwa super powers, nchi imetolewa sadaka mchana kweupe

kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
2,375
4,893
Ni hatari kua adui wa Marekani, lakini ni hatari zaidi kua rafiki wa Marekani, Henry Kissinger.. je ni haki kwa Ukraine kutupwa nje kwenye meza ya mazungumzo kuangalia namna ya kuvimaliza vita? Je, miundombinu na idadi ya askari waliojeruhiwa na kufa pale ukraine si kitu kwa Dunia? kwa sasa Zelensky atakua kwenye hali gani? waliompa silaha na kumuhimiza apigane wanampangia kitu cha kukubali kwenye meza ya mazungumzo ambayo yeye hatashiriki bali ataambiwa cha kufanya!

Urusi amechukua takribani 20% ya ardhi nchini ukraine ikiwa na utajiri wa madini, gesi, bandari, ardhi yenye rutuba pamoja na kiwanda kikubwa cha nyukilia Ulaya, USA ametangaza kuyataka madini muhimu ( rare minerals) ili kufidia gharama za silaha na fedha alizopewa na mkubwa huyu, madini hayo yatachimbwa kwa mda mrefu hivyo tutarajie makampuni ya US kua kwenye ardhi ya ukraine. Russia naye ameweka ngumu kuachia majimbo aliyoyachukua kwa Ukraine, majimbo hayo yatapaswa kua ni ardhi ya Russia na Dunia itapaswa kutambua hivyo.

Ikiwa hayo yatatokea ( ni lazima itakua hivyo) maana yake Ukraine itakua imetolewa sadaka kuwabariki wakubwa wawili utajiri mkubwa sana ulipo ardhini kwao, je Zelensky hakuyajua haya? intelligence ya Ukraine haikuona haya yakija? hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii itaenda kuaje pale Ukraine?

ikumbukwe Ukraine ilipata msaada wa bilions za dollar kutoka ulaya na marekani ili kuiangusha Urusi, sio hivyo tu, Urusi ilipokea na mpaka sasa ina vikwazo vya kiuchumi kibao ambavyo dunia haijawahi kushuhudia toka imeanzishwa, wachumi na majasus wa west walikua na calculation za kuimaliza vita mapema au kuilazimisha urusi ije mezani na kukubali matakwa yao. katika hali ya kushangaza sana Urusi imeweza kuhimili vikwazo vyote, na katika vita imechukua ardhi ya ukraine ya kutosha huku ikizinyanyasa sana silaha za west kwenye uwanja wa vita.

kwa hayo yote yaliyotokea, Dunia itakua imeona mabadiliko makubwa ya utawala wa kidunia na sasa wakubwa wa kutoa order hatakua mmoja tena bali wawili au watatu (multpolar system) hata sisi wamarekani wa mbwinde, na warusi wa ubena zomozi tutakua tumejua ukweli mkuu kuhusu siasa za kidunia, pole sana ukraine, pole sana ulaya, haki ipo mbinguni tu.
 
Wa ubena zomozi hoyeee,Warusi weusi ni fire.
 
Dume la dunia ni Russia na mama ni US ulaya ni watoto sasa baba na mama watakutana saudia kutoa maelekezo.
 
Ni mhimu kujifunza kwa wenzako ama kwa hakika dunia ni uwanja wa fujo donbas imekwenda madini yamekwenda zelesky amekwenda watoto wa maskini wamekwenda nachelea kusema kwamba ukoloni mamboleo upo na hakuna rafiki wa kuleta maendeleo zaidi ya ninyi wenyewe
Umemaliza kaka
 
Trump anachofanya kwa urusi ni kama kutoa hisani na zawadi maana kama si propaganda za urusi kwenye mitandao ya kijamii Leo hii asingeupata uraisi kwenye ile tem ya Kwanzaa haikuwa direct ila indirect way kwa kutumia account fake na kuweka habari nzuri za trump so anarudisha fadhila
 
Back
Top Bottom