Ukorofi Usio na Sababu: Njaa Imeisha?

You can't use an anecdotal example to dismiss the claim kwamba hakuna njaa, that one person isn't a representative of a whole

Njaa ipo and it has been proven kwa kutumia tafiti, soma report ya twaweza iliyokuwa published recently
Twaweza ni wazushi tu,hawana lolote.Hakuna njaa.Njaa iko kwa waliokuwa wapiga dili na wale wavivu wasiotaka kufanya kazi lakini wanataka kula.Hapa kazi tu.
 
You can't use an anecdotal example to dismiss the claim kwamba hakuna njaa, that one person isn't a representative of a whole

Njaa ipo and it has been proven kwa kutumia tafiti, soma report ya twaweza iliyokuwa published recently
...UN, ambao shughuli zao za huduma, na misaada ya kibinadam, msingi wake ni tafiti, imetoa taarifa kwa mujibu wa tafiti zake kuwa nchi nne ulimwengu(yemen, sudan kusini, somalia, na nigeria/kaskazini mashariki), ndio nchi zinazokabiliwa na baa la njaa, na juhudi zifanyike kuzisaidia, kukabiliana na baa hilo...baadhi ya vigezo vya UN, kutangaza baa la njaa, ni pamoja na asilimia 20, ya watu ktk eneo husika wakishindwa kukabiliana na upungufu wa chakula(twaweza wanasema theluthi, i.e 33% ya watanzania wanalalia mlo mmoja kwa siku, au wanakosa kabisa),na mlipuko mkubwa wa utapiamlo kwa wtt...
....tafakari...
....upatikanaji wa chakula masokoni ktk tz ukoje?(uwezo wa kununua ni jambo lingine)
...utapiamlo ktk tz?
....mwaka jana, mvua zilikuwaje, na hali ya mavuno ilikuwaje?
.....
 
You can't use an anecdotal example to dismiss the claim kwamba hakuna njaa, that one person isn't a representative of a whole

Njaa ipo and it has been proven kwa kutumia tafiti, soma report ya twaweza iliyokuwa published recently
Kilo moja ya unga 2000
Nenda Sokoni ukaulize bei ya debe la Mahindi, Kilo ya mchele halafu ulinganishe na miaka miwili iliyopita, halafu ujiulize mtu wa kijijini hela ambavyo haipatikani anamuduje kunua hayo mahindi na kwa familia zetu tunavyojua kuzaa.

Ukishayafanya hayo, njoo tena na swali lako la njaa.
Huku njaa Ipo,debe la mahindi 25000,Hii ni Mbeya.Huwezi kuelewa lakini,UPO MAREKANI.

Hiyo ndiyo njaa kwa maoni ya baadhi ya watu mitaani na watafiti uchwara. Kabla hatujarudi studio kwa matokeo mengine zaidi kwa njia ya mtandao, naomba kutoa maoni yangu. Yaonekana bei ya mazao ya vyakula ikipanda, hiyo ni njaa. Sukari ilipopanda bei, hiyo haikuwa njaa. Kilo ya samaki ilipopanda bei kwa sababu ya rift valley fever, haikuwa njaa.

Maoni ya undani hebu tujadiliane. Mazao ya chakula kama Mpunga/mchele na mahindi hayaangaliwi sana na mpaka sasa hakuna anayeweza kunieleza bei halisi ya mazao hayo ni ipi, ili mkulima asipate hasara na mlaji asiumie. Kila mwaka wakati wa mavuno, mkulima ni kama anagawa bure mazao yake. November 2014 bei ya gunia la mahindi Sumbawanga liliuzwa TZS 8000 - 12000! Bei ya kishenzi kabisa! Walaji hawakusikiliza kilio cha mkulima, walikenua na wengine kusanga na kulisha nguruwe. Leo hii bei ya debe inapofikia 25000 watu walalama eti hiyo ndiyo njaa!

Serikali iliyopita iliwahi ruhusu uingizaji wa mchele wa nje kwa sababu tu kilo moja Dar ilifikia 2500. Mchele ukaingia na wafanyabiashara walionunua kwa mkulima na baadhi ya wakulima wakapigwa hasara.
 
Tatizo mmelishwa unga wa ndele.

Madhara ya siasa zisizo na kichwa, kwenda na upepo.
-jina la Nchemba,
-January Makamba na mzungu,
-Dangote kufunga kiwanda,
-njaa,
-Bashite etc
 
Najua watu wanataka kuona vyeti vya Makonda, na wengine wangependa aondolowe Mkoa wa Dar na aletwe mtu mwingine mwenye vyeti vinavyoweza kuthibitisha kuwa alisoma shule ya vidudu a.k.a chekechea wapi, shule ya msingi wapi (na kama hakuhama) na hata ijulikane majina yake ya utotoni au ya Kilugha. Na najua watu wengine wamekwazika na yaliyotokea kwenye Mkutano Mkuu wa CCM na wengine wanaendelea kufuatilia yanayotokea TLS na matukio mengine mengi.. habari ya Magu kufisiwa na Trump (ambayo nilisema ilipoletwa humu haina ukweli) na habari nyingine nyingi..

Ila kati ya mengi ambayo binafsi nilitaka kusikia ni kuwa suala la njaa limeishia wapi. Maana mwaka ulivyoanza tulitaka kuaminishwa kabisa kuwa kuna watu wanakufa hasa baada ya "mifugo 3000" ya watu wenye njaa ilipokufa! Nakumbuka hata Magufuli alipofika mahali fulani watu walimlilia na kusema "njaa, njaa" hadi akawajibu 'mbovu' (walikuwa wanacheka wale waliokuwa wanasema 'njaa njaa').

Mvua zimeanza kunyesha na mafuriko kila kona, na juzi nimemuona dadangu mmoja nyumbani akitembelea shamba lake la mahindi huko Songea; mahindi yakiwa ya kijani kitupu yamefika kiunoni sasa.. nikabakia kujiuliza ile njaa ilikuwa kweli njaa au vipi?

Njaa ile imeisha au ni njaa itakayokuja; ni njaa iliyokuwepo tayari au kulikuwa na tishio la njaa baadaye mwakani au mwaka huu? Ni njaa ambayo maeneo yale ambayo yalikuwa kame bado yana ukame na watu hawajaweza kupanda au sasa yamekuga ya kijani tangu mvua zianze na watu wameanza kupanda..

Kama njaa haikuwa njaa ya kutisha kama tulivyoambiwa; itakuwaje siku kama kutakuwa na tishio la njaa la kweli. Siyo kwamba ndugu zetu waliolia "njaa njaa" wakawa kama yule mtoto wa kwenye simulizi la Hisopo aliyelia "mbwa mwitu mbwa mwitu" kwa sababu tu alikuwa ameboreka wakati anachunga kumbe hakukuwa na mbwa mwitu? Siku moja mbwa mwitu kweli akatokea na alia "mbwa mwitu!" watu wakadhani "ndiyo alivyo huyo" wakapuuzia?

Najisikia kukorofisha watu tu ili wahoji mambo makubwa zaidi yanayotishia taifa letu na vijana wetu kuliko vyeti vya Paul Makonda a.k.a Bashite Original.. or they say.
Mwanakijiji wewe sio mtafiti wala mchumi, dalili moja ya bidhaa kuadimika (chakula hususani Mahindi) ni kupanda bei ya bidahaa hiyo, mfuko wa unga wa kilo 25 mwaka juzi tulikua tunanunua sh 27,000 leo 39,000. Sasa upungufu huu unasababishwa na nini? hii ni dalili ya uhaba mkubwa wa mahindi na ndio dalili za NJAA yenyewe. Miaka ya nyumba MWANAKIJIJI ulikua unaandika makala zenye msingi sana, SIJUI UMEPATWA NA NINI? au huyu siye mwanakijiji halisi huyu ni mwanakijiji bashite.
 
Najua watu wanataka kuona vyeti vya Makonda, na wengine wangependa aondolowe Mkoa wa Dar na aletwe mtu mwingine mwenye vyeti vinavyoweza kuthibitisha kuwa alisoma shule ya vidudu a.k.a chekechea wapi, shule ya msingi wapi (na kama hakuhama) na hata ijulikane majina yake ya utotoni au ya Kilugha. Na najua watu wengine wamekwazika na yaliyotokea kwenye Mkutano Mkuu wa CCM na wengine wanaendelea kufuatilia yanayotokea TLS na matukio mengine mengi.. habari ya Magu kufisiwa na Trump (ambayo nilisema ilipoletwa humu haina ukweli) na habari nyingine nyingi..

Ila kati ya mengi ambayo binafsi nilitaka kusikia ni kuwa suala la njaa limeishia wapi. Maana mwaka ulivyoanza tulitaka kuaminishwa kabisa kuwa kuna watu wanakufa hasa baada ya "mifugo 3000" ya watu wenye njaa ilipokufa! Nakumbuka hata Magufuli alipofika mahali fulani watu walimlilia na kusema "njaa, njaa" hadi akawajibu 'mbovu' (walikuwa wanacheka wale waliokuwa wanasema 'njaa njaa').

Mvua zimeanza kunyesha na mafuriko kila kona, na juzi nimemuona dadangu mmoja nyumbani akitembelea shamba lake la mahindi huko Songea; mahindi yakiwa ya kijani kitupu yamefika kiunoni sasa.. nikabakia kujiuliza ile njaa ilikuwa kweli njaa au vipi?

Njaa ile imeisha au ni njaa itakayokuja; ni njaa iliyokuwepo tayari au kulikuwa na tishio la njaa baadaye mwakani au mwaka huu? Ni njaa ambayo maeneo yale ambayo yalikuwa kame bado yana ukame na watu hawajaweza kupanda au sasa yamekuga ya kijani tangu mvua zianze na watu wameanza kupanda..

Kama njaa haikuwa njaa ya kutisha kama tulivyoambiwa; itakuwaje siku kama kutakuwa na tishio la njaa la kweli. Siyo kwamba ndugu zetu waliolia "njaa njaa" wakawa kama yule mtoto wa kwenye simulizi la Hisopo aliyelia "mbwa mwitu mbwa mwitu" kwa sababu tu alikuwa ameboreka wakati anachunga kumbe hakukuwa na mbwa mwitu? Siku moja mbwa mwitu kweli akatokea na alia "mbwa mwitu!" watu wakadhani "ndiyo alivyo huyo" wakapuuzia?

Najisikia kukorofisha watu tu ili wahoji mambo makubwa zaidi yanayotishia taifa letu na vijana wetu kuliko vyeti vya Paul Makonda a.k.a Bashite Original.. or they say.

MMM acha dhihaka. Afadhali uchochezi kuliko dhihaka hizo.

Je hujui Serikali yako ilipiga marufuku hilo neno kujadiliwa wala kuripotiwa na vyombo vya habari? Hujui baadhi ya ma RPC waliweka bayana kuwa hilo ni kosa na kuwa "wakorofi" watakaoripoti watakiona cha moto?

Lakini twende kwenye suala lenyewe, je unajua bei ya mahindi? Je unajua bei ya kilo moja ya unga wa mahindi? Je unajua bei ya nafaka nyinginezo? Ni kipato gani cha mwananchi wa kawaida kinaweza kuendana na kupanda huko kwa bei hizo? je unajua kaya nyingi zimeshindwa kumudu milo mitatu kwa siku?

Msimu wa kilimo kwa baadhi ya mikoa umewadia, baada ya ukame wa muda mrefu, je unajua wadudu waharibifu kama viwavi jeshi na magonjwa kama ukungu vinaharibu mazao yaliyoko shambani......Serikali makini ingefanya bidii kutoa taarifa na msaada ili kunusuru mazao yasiharibike na hivyo kuongeza uhaba wa chakula nchini. Badala ya wewe kuja hapa na bla bla nyepesi kama hii afadhali ungetumia nafasi na wino huo kuandika namna gani tunaweza kuepuka balaa lililo mbele yetu. Jamani muwe na utu na huruma wakati mwingine, tukiendekeza hizi siasa mfu tutadaiwa damu za watu siku moja.

Angalia wenzetu:-
Fall armyworm identified in South African crops
African Armyworm hits 22 states in Nigeria - AgroNigeria
Uunaweza kuona nchi nyingine pia zinavyokabiliana
 
Duh naanza kuwa na mashaka sasa na wewe.

kwa hiyo ni ruhusa kwa kiongozi yoyote na mtanzania yeyote kufoji vyeti na asihojiwe eti kwa sababu tuna matatizo mengine makubwa ndio tudeal nayo. Sasa kama hata vyeti vinafojiwa na ni dhambi kwa kiongozi wa umma kutoka hadharani na kueleza ukweli wa elimu na mali zake tutawezaje kutatua matatizo hayo unayoyaita makubwa.??

jitafakari mkuu.
 
Uko marekani...unasoma tuu kwenye mitandao ya kijamii...hali halisi ya chakula njoo utembelee vijijini huku sio kwenye keyboard.
 
Huku njaa Ipo,debe la mahindi 25000,Hii ni Mbeya.Huwezi kuelewa lakini,UPO MAREKANI.

Unataka debe la mahindi liuzwe shilingi ngapi? Sisi wakulima wazazi wetu wamekuwa masikini kwa miaka yote si kwa sababu hawafanyi kazi ila kwa sababu mazao ya shambani hayana bei kabisa. Ni wakati muafaka sasa kwa bei za mazao ya shambani kupanda bei ili asilimia 80 ya WTZ waanze kufaidika pia. Kwangu mimi nataka bei hii ya vyakula ipande zaidi na zaidi kwakuwa wakulima watanufaika na kuwa na maisha bora. Wewe unafahamu gharama na ugumu wa kilimo, unafahamu tabu anazopata mkulima wa mpungu tokea kwenye kufyeka shamba, kuchimbua kwa mkono, kupanda, kung'olea majani kwa mkono, kulinda ndege, kuvuna, kupiga, kupeta, kusafirisha nyumbani (kijijini), kukoboa na kupeleka sokoni, kisha unataka auze shilingi 500, are you real okay, sisi tulioishi maisha hayo ya kilimo na kukulia huko tunataka sana bei ipande na ipande ili mradi mkulima anufaike. Maisha ni ku plan, si wote lakini kuna watu wanaishi mijini na kulima huko kwao japo hekari mbili tatu kwaajili ya chakula cha familia, wewe huwezi hilo then acha ufe tu.
 
Hiyo ndiyo njaa kwa maoni ya baadhi ya watu mitaani na watafiti uchwara. Kabla hatujarudi studio kwa matokeo mengine zaidi kwa njia ya mtandao, naomba kutoa maoni yangu. Yaonekana bei ya mazao ya vyakula ikipanda, hiyo ni njaa. Sukari ilipopanda bei, hiyo haikuwa njaa. Kilo ya samaki ilipopanda bei kwa sababu ya rift valley fever, haikuwa njaa.

Maoni ya undani hebu tujadiliane. Mazao ya chakula kama Mpunga/mchele na mahindi hayaangaliwi sana na mpaka sasa hakuna anayeweza kunieleza bei halisi ya mazao hayo ni ipi, ili mkulima asipate hasara na mlaji asiumie. Kila mwaka wakati wa mavuno, mkulima ni kama anagawa bure mazao yake. November 2014 bei ya gunia la mahindi Sumbawanga liliuzwa TZS 8000 - 12000! Bei ya kishenzi kabisa! Walaji hawakusikiliza kilio cha mkulima, walikenua na wengine kusanga na kulisha nguruwe. Leo hii bei ya debe inapofikia 25000 watu walalama eti hiyo ndiyo njaa!

Serikali iliyopita iliwahi ruhusu uingizaji wa mchele wa nje kwa sababu tu kilo moja Dar ilifikia 2500. Mchele ukaingia na wafanyabiashara walionunua kwa mkulima na baadhi ya wakulima wakapigwa hasara.
Mkuu...bahati mbaya, lkn ni ukweli usiofurahisha ambao inabidi, tuuseme....wenzetu wengine wengi, kadri wanavyojitahidi jenga hoja ya njaa ktk tanzania, ndio wanavyozidi thibitisha namna walivyo na ubongo wa kiwango sawia na panya......
 
We we panya ni bonge LA genius, panya tulize sisi watu wa sayansi bwana. Nyie Si hampendi challenge? Mnaamini ndio MZEE je ni akili ujinga huko?
 
Kama hujaelewa kitu, omba ueleweshwe na sio kuleta ad hominem attacks. Hopeless!
Hamna lolote. Huu ni ulimbukeni uliokubuhu. Ningekuona wa maana kama ungeandika mada nzima kwa aidha Kiingereza au Kiswahili. Kuchanganya lugha ni sawa na kunajisi. Ninakuhakikishia huwezi kunisogelea kwa Kiingereza; ninakijua fika. Lakini huu ulimbukeni wa kuchanganya lugha siko huko.
 
Njaa? Njaa gani wakati mi hapa nimetoka kupata kitimoto....

IMG-20170215-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom