Najua watu wanataka kuona vyeti vya Makonda, na wengine wangependa aondolowe Mkoa wa Dar na aletwe mtu mwingine mwenye vyeti vinavyoweza kuthibitisha kuwa alisoma shule ya vidudu a.k.a chekechea wapi, shule ya msingi wapi (na kama hakuhama) na hata ijulikane majina yake ya utotoni au ya Kilugha. Na najua watu wengine wamekwazika na yaliyotokea kwenye Mkutano Mkuu wa CCM na wengine wanaendelea kufuatilia yanayotokea TLS na matukio mengine mengi.. habari ya Magu kufisiwa na Trump (ambayo nilisema ilipoletwa humu haina ukweli) na habari nyingine nyingi..
Ila kati ya mengi ambayo binafsi nilitaka kusikia ni kuwa suala la njaa limeishia wapi. Maana mwaka ulivyoanza tulitaka kuaminishwa kabisa kuwa kuna watu wanakufa hasa baada ya "mifugo 3000" ya watu wenye njaa ilipokufa! Nakumbuka hata Magufuli alipofika mahali fulani watu walimlilia na kusema "njaa, njaa" hadi akawajibu 'mbovu' (walikuwa wanacheka wale waliokuwa wanasema 'njaa njaa').
Mvua zimeanza kunyesha na mafuriko kila kona, na juzi nimemuona dadangu mmoja nyumbani akitembelea shamba lake la mahindi huko Songea; mahindi yakiwa ya kijani kitupu yamefika kiunoni sasa.. nikabakia kujiuliza ile njaa ilikuwa kweli njaa au vipi?
Njaa ile imeisha au ni njaa itakayokuja; ni njaa iliyokuwepo tayari au kulikuwa na tishio la njaa baadaye mwakani au mwaka huu? Ni njaa ambayo maeneo yale ambayo yalikuwa kame bado yana ukame na watu hawajaweza kupanda au sasa yamekuga ya kijani tangu mvua zianze na watu wameanza kupanda..
Kama njaa haikuwa njaa ya kutisha kama tulivyoambiwa; itakuwaje siku kama kutakuwa na tishio la njaa la kweli. Siyo kwamba ndugu zetu waliolia "njaa njaa" wakawa kama yule mtoto wa kwenye simulizi la Hisopo aliyelia "mbwa mwitu mbwa mwitu" kwa sababu tu alikuwa ameboreka wakati anachunga kumbe hakukuwa na mbwa mwitu? Siku moja mbwa mwitu kweli akatokea na alia "mbwa mwitu!" watu wakadhani "ndiyo alivyo huyo" wakapuuzia?
Najisikia kukorofisha watu tu ili wahoji mambo makubwa zaidi yanayotishia taifa letu na vijana wetu kuliko vyeti vya Paul Makonda a.k.a Bashite Original.. or they say.