Ukiwa pia ni Mkatoliki mwenzangu na Mcha Mungu mzuri nakukubali sana CDF Mstaafu. Jenerali Mabeyo na hapa umemaliza kila kitu hongera mno

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
60,025
119,543
DAR ES SALAAM - Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo amesema vijana wengi kwa sasa wanahangaika kupata ajira licha ya kuwa ni wasomi wazuri akishauri wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma kusaidia katika usimamizi wa mashirika hayo ili yatengeneze ajira kwa vijana.

Jen. Mabeyo amesema vijana hao kwa sasa wamekosa mwelekeo na wanajenga hofu kwa taifa la kesho akisisitiza ni wajibu wa waliopewa dhamana kufanya kazi kwa ari kubwa na kwa nia njema kuonesha njia katika kusimamia menejimenti kuleta matokeo makubwa.

Chanzo: HabariLeo

Utendaji wako haujawahi kuwa na Shaka lakini pia na hata Ubobezi wako Kijeshi nao pia ni wa Kiwango cha Kutukuka.

PIA SOMA
- MABEYO (CDF MSTAAFU): Vijana wanakosa mwelekeo, tunajenga hofu kwa taifa la kesho (Juni 11, 2024)
 
Vijana wa kiume wananyanyasika mno, ukijumlisha na haya mambo ya 50% 50% ndo wanapotea kabisa. Unakuta kijana kachoka kachoka kachakaa na ana degree huku akiulizwa utaoa lini?
kwani kuoa ni lazima?
 
Ameongea kwa uchungu sana... neno tunatengeneza " TAIFA LA HOFU" hapa mwenye akili atakuwa amemuelewa...jiulize nini maana ya Taifa la hofu?
 
DAR ES SALAAM - Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo amesema vijana wengi kwa sasa wanahangaika kupata ajira licha ya kuwa ni wasomi wazuri akishauri wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma kusaidia katika usimamizi wa mashirika hayo ili yatengeneze ajira kwa vijana.

Jen. Mabeyo amesema vijana hao kwa sasa wamekosa mwelekeo na wanajenga hofu kwa taifa la kesho akisisitiza ni wajibu wa waliopewa dhamana kufanya kazi kwa ari kubwa na kwa nia njema kuonesha njia katika kusimamia menejimenti kuleta matokeo makubwa.

Chanzo: HabariLeo

Utendaji wako haujawahi kuwa na Shaka lakini pia na hata Ubobezi wako Kijeshi nao pia ni wa Kiwango cha Kutukuka.

PIA SOMA
- MABEYO (CDF MSTAAFU): Vijana wanakosa mwelekeo, tunajenga hofu kwa taifa la kesho (Juni 11, 2024)
Aliongea Kama mtanzania na siyo mkatoliki
 
Itabdi na yeye aondoke hapo kama Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) ili vijana wapewe hiyo nafasi maana yeye kisha staafu tayari. Ajihuzuru hiyo nafasi kwanza kwa vitendo
 
Sasa hivi tunakumbwa na hili wimbi la wasomi wengi na ajira rasmi na zisizo rasmi ni za kugombania vibaya mno, Bado sijaona kama taifa tumejipanga vipi na hili. Sasa basi kama tunaliangalia Kwa macho tu basi Nina uhakika tutakuja kutafutana uchawi nchini.
 
Back
Top Bottom