Ukitaka usipoteze muda na uhudumiwe haraka kwenye ofisi za umma ni muhimu kujua unahudumiwa na mtu wa aina gani

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
15,392
21,181
Kama hupendi mambo yako yaharibike unapokwenda kwenye ofisi za serikali kuomba huduma flani basi uwe na akili ya haraka ya kutambua yule afisa ni mtu wa aina gani. Mara nyingi kama yeye ni mjinga basi fanya kila uwezalo ujifanye mjinga zaidi yake, wakati mwingine hata zuzu kabisa (hii ni ngumu lakini).

Ukiona kabla hata hujamaliza kutaja jina lako anaingilia na kusema kwani wewe huna baba au ukoo na anaanza kung'aka hapo na kukuuliza maswali ya mtego na kuingilia kabla hata hujamaliza; basi ujue unadili na mjinga, kilaza, akina zero hao.

Hawa watu wana low self esteem na wanatafuta wapi wapige kiki ili angalau wajisikie watu kidogo. Watu hawa hupenda kudhalilisha wengine (hupenda ku-harass) kwasababu hawana wanachokijua na hawajiamini, kila mara watataka wakuweke chini ya miguu yao.

Hiyo inaitwa self defense na inafanywa na watu wale tunaita incompetent. Hawa ndio waliojaza maofisi ya serikali kwa bahati mbaya!
 
siku zote mjinga ndio ana jiamini sana
432299648_711342261213944_8509604648052012376_n.jpg
 
Hapa ndipo ninapowaelewa wale ndugu zangu wa "unanijua mimi nani" wallahi kuna mazingira mengine wasipokujua wewe nani hupati haki yako, yani mtu anafuata haki yake unaanza kumletea dharau halafu akikuonesha yeye nani unaanza kulalamika watu wana uonevu, hii nchi usipokuwa na pesa au cheo utadharauliwa na kuonewa sana hata pale ambapo unaona kabisa hapa unastahili kupata haki yako
 
Inawezekana pia ameshakusoma na ameshaelewa unachotaka kusema.

Inawezekana pia akawa,mbele yako kifikra kuhusiana na hilo lililokuleta.

Inawezekana pia japo sio kwa kiasi kikubwa kwa hicho unachokisema kwamba kipo.

So stay calm subiri maelekezo yake,ukijifanya mjuaji unaweza usikamilishe kilichokuleta na ukaishia kulaumu laumu tu.
 
Nawewe yawezekana pia una katabia kama ka hao watu.
Inawezekana pia ameshakusoma na ameshaelewa unachotaka kusema.

Inawezekana pia akawa,mbele yako kifikra kuhusiana na hilo lililokuleta.

Inawezekana pia japo sio kwa kiasi kikubwa kwa hicho unachokisema kwamba kipo.

So stay calm subiri maelekezo yake,ukijifanya mjuaji unaweza usikamilishe kilichokuleta na ukaishia kulaumu laumu tu.
 
Back
Top Bottom