Napata Elimu Kwangu Furaha.Nguvu ya msamaha ni kubwa sana ikiwakilisha Nuru na nguvu ya kisasi pia ni kubwa ikiwakilisha utawala wa giza...binadamu wengi wana roho ya Kimungu ndani yao ndio maana hukinzana sana na nafsi zao linapokuja suala la kisasi au msamaha
Kuna wakati huwa nakaribia kabisa kulipiza lkn narudi nyuma najua kama hayajawahi kukutokea ni ngumu kuelewa lkn yapo na maadamu nimeshaamua na nimeishi miaka yote hiyo nitavumilia tu.Usiishi na maumivu wala usijiweke njiapanda bila sababu fanya moja kati ya mawili,
Ushauri mbaya; lipa kisasi kupunguza maumivu kisha tubu
mkuu kuna mambo ukiangalia impact iliyokuletea maishani na unaishi ndani ya hiyo hali aisee unashindwa kusahau kabisa .. a
sawa mkuuMtani lipa kisasi ili hiyo roho ife
ngoja nifanye mchakato wa kulimalizaNakuelewa vizuri sana miss chagga , lakini nimejifunza kuachilia vinginevyo unweza kupata maradhi yasiyotibika na kukuletea matatizo makubwa bila sababu.
ngoja nifanye mchakato wa kulimaliza
Tukiweka Imani zetu za dini pembeni, hapo upo sawa.
Mkuu, Imani yako itakuponya, ukijua kusamehe inakubidi ujue pia na kusahau.Mimi huwa nasamehe mara zote ila kusahau ndo nilishashindwa kabisaa. Hivi inawezekana kabisa kusahau baya alilokutendea mtu??
asante mkuu kwa ushauriUbarikiwe sana.
Naomba nikutolee mfano mmoja, huenda ikawa watu tayari wapo kwenye ndoa na wanamaisha mazuri tu. Inakuja kutokea moja wa wanandoa anamfahamu mmoja wa watu waliowahi kuwa na mahusiano na mmoja wao kabla hawajaingia kwenye ndoa. Hali huenda ikabadilika hata kama tukio lilitokea zamani sana. Sasa nnachojiuliza kama hiyo hali ilikua ni hatari na inashida mbona waliishi vizuri tu hadi hapo hilo jambo lilipogundulika hata kama haliendelei kwa sasa? Tatizo linakua kwenye mtazamo na fikra tu lakini ki uhalisia hakua shida hapo.
Ndio maana tunashauriwa kuwa makini sana na mambo tunayofikiri na kutafakari, usikaribishe sana mawazo ya vitu vilivyokuumiza utajikuta unakosa amani bila sababu. kama jambo lilisha pita na haliendelei, endelea na maisha mapya!
hii ya leo ni tofauti kidogo na mada zetu zile , hii inahusika na kulipa kisasi
Katika maisha bila kujali unaamini nini hakuna jambo jema kama kusamehe!msamaha hukusaidia mengi mpaka kifo na maisha yanayofuata baada ya kifo iwe reincarnation au rebirth nk !msamaha hukufanya uwe mwema mwenye furaha ya kweli usiye na makunyanzi rohoni na usoni
Mwenye msamaha ana nuru usoni , msamaha ni tiba, msamaha ni mafanikio msamaha ni amani na ni upendo
Lakini je kama huamini katika msamaha? Kama unayemsamehe hasameheki? Na je kama ni mbabe mjuaji na dhulumati mkubwa?je kama anakuletea dharau kwa hali yoyote ile hata uwe msamehevu kiasi gani? Usiishi na maumivu! lipa au lipiza..!
Msamaha wako usikushushe msamaha wako usikufanye kiumbe dhaifu na mnyonge, utu wako ni muhimu heshima na dhima yako ni vitu vya kulinda na kuzingatia mno...ukishindwa kabisa kusamehe ukizidiwa na viwango vya uvumilivu wa kibinadamu usiumize roho yako andaa kisasi
Kama ilivyo kwa msamaha ile nafuu unayoipata kwenye kusamehe basi ndivyo ilivyo hata kwenye kisasi! Kisasi humpa mtu faraja na amani ya moyo huridhika kuona amefanya jambo baya kwa mtu mbaya
Tunaishi na wajuaji wengi kwenye jamii tunaishi na watu wanaojiona wao ni bora kuliko wengine wao ni zaidi kuliko wewe...wao ndio wanaijua pesa kuliko wewe. . . . usimpe nafasi mtu wa namna hii atambe...ni lazima umfundishe ajue kuwa maisha yana pande nyingi...kisha mfundishe kwa maumivu makubwa maumivu atakayodumu nayo mpaka kifo
LAKINI maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua...Fanya kile kitakachokupa nafuu ya rohoni na afya ya akilini kwakuwa uamuzi ni wako na mwisho utabaki wewe kama wewe ....visasi misamaha na malipizi vitabaki kuwa uamuzi binafsi kutokana na imani yako hofu yako na huruma yako
Mwanadamu yeyote aliyeumbwa na MUNGU anasameheka, ispokuwa iikingia roho ya shetani ndiyo shida. Ongeza maarifa juu ya mapenzi na upenda wa Mungu kwa wanadamu, itakuwa rahisi kwako kusamehe na kusahau.Kuna watu hawasameheki!
Ukimsamehe anakuona mjinga yeye mjanja sana yeye ndio ana akili za kutosha yeye ndio mtoto wa mjini.... Pipo kama hizi ni kulipiza tu kisasi kwenda nao sambamba tofauti na hapo utakufa umekunja sura
Hongera upo hatua nzuri sana, na unasogea kwenye ukamilifu wa uaanadamu, soma sana upendo wa MUngu kwa wanadamu, mtu asiyekosa kufa kwa ajili ya wengine wenye makosa. Omba MUNGU akupe nguvu ya kuujua upendo wake halisi. Itafika mahali utaomba msamaha mwingine akikosa na unajua yeye hajui amekosa.mimi naweza kusamehe ila huwa nakumbuka na kuumia sana hadi kulia .. kisasi naogopa na kusamehe nashindwa kusahahu
asante mkuu hope nitafikia kwenye huo ukamilifuHongera upo hatua nzuri sana, na unasogea kwenye ukamilifu wa uaanadamu, soma sana upendo wa MUngu kwa wanadamu, mtu asiyekosa kufa kwa ajili ya wengine wenye makosa. Omba MUNGU akupe nguvu ya kuujua upendo wake halisi. Itafika mahali utaomba msamaha mwingine akikosa na unajua yeye hajui amekosa.
haimainishi hutasikia hasira ukikosewa, lahasha ila hasira yako haitadumu masaa 12, amani ya moyo itakujia kabla jua halijazama, ukiona inazidi hapo omba MUNGU msamaha na rehema ili amani arudi kwako.
KWASABABU KUSAMEHE SI RAHISI NDO MAANA SITAK KUSEMA NENO LOLOTEUmependa hivyo unaenda wapi?
Mwanadamu yeyote aliyeumbwa na MUNGU anasameheka, ispokuwa iikingia roho ya shetani ndiyo shida. Ongeza maarifa juu ya mapenzi na upenda wa Mungu kwa wanadamu, itakuwa rahisi kwako kusamehe na kusahau.
Moja ya kigezo cha juu cha ukamilifu wa mwanadamu ni kusamehe na kusahau refer Nelson Mandela na mateso aliyopata.