Ukipata nafasi ya kumshauri ushauri mmoja tu Mh. Rais Utamshauri nini?

Nitamshauri amtunze huyu bi mkubwa wa Changanyikeni. Anateseka sana na watoto na wajukuu zake. Jamaa msimwone hapo alipo alioa mapema japo alimtelekeza aliyejifunzia kuwa baba. Hapo alipo ana wajukuu. Huyo aliyenaye ni bi mdogo.
 
Nitamshauli

(mimi ni mfanyakazi)

1. Aongeze mishahara ya wafanyakazi na apunguze kodi kwenye mishahala hiyo.
2. Afatilie na kuwachukulia hatua waajiri wanaokula michango ya wafanyakazi inayopelekwa katika mifuko ya jamii kama NSSF.
3.Wafanyakazi wanaostaafu kazi walipwe haki zao haraka
4. Arudishe michezo ya wafanyakazi SHIMIWI
5.Ahakikishe pesa ya matumizi mengineyo ( OC ) ya kila mwezi inapelekwa kwenye, Halmashauri, Wizara na taasisi zake ili kukidhi mahitaji ya ofisi hizo.
5. Ahudhurie sherehe za kila mwaka za Meimosi na azungumze na wafanyakazi hasa kuhusu mikakati ya kuboresha maslahi yao
6.Apitishe hitaji la kuongeza kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi kiwe Shilingi Laki Tano
7. Aboreshe mkakati wa kukuza ajira katika taasisi za uma na binafsi.
8.Aimarishe ukaguzi wa mahesabu katika taasisi za uma na awatumbue viwavi wa pesa za uma. (wakamatwe na washtakiwe)
9.Aimarishe huduma za bima ya afya hasa upatikanaji wa dawa kwa wagonjwa wanaotumia kadi za bima.
10.Asikilize na kutatua kero mbalimbali za wafanyakazi, hasa wa sekta binafsi.

Nawasilisha.
 
Nitamshauri aachane na kutenga fedha za uchaguzi,mwaka 2020. Angoje mpaka 2025,
ndio aitishe uchaguzi,
Hiyo fedha ya uchaguzi2020awajengee chadema ofisi,na zingine tuanzishie mradi wa kuchimba chuma Liganga!"
 
Nitamshauri amtunze huyu bi mkubwa wa Changanyikeni. Anateseka sana na watoto na wajukuu zake. Jamaa msimwone hapo alipo alioa mapema japo alimtelekeza aliyejifunzia kuwa baba. Hapo alipo ana wajukuu. Huyo aliyenaye ni bi mdogo.
Kumbe??
 
Wakuu najua nchi haijengwi na mtu mmoja, tunahitaji mawazo ya watu mbali mbali ili tuijenge nchi yetu.

Ikitokea Leo umepata nafasi ya kusikilizwa na Mh. Rais utatoa ushauri gani? Kumbuka nafasi utakayo pewa ni moja tu, utamshauri nini?

Binafsi nitamshauri aunde tume huru ya uchaguzi.

Wewe je?
  • Nitamshauli kwenye awamu yake ya pili (2020-2025) aipeleke nchi kwenye muundo wa serikari moja
    • muundo wa sasa wa serikari mbili ni "imperfect union"- yani upo kama haupo
    • pia muundo wa sasa wa serikari mbili unapoteza sana hela za walipa kodi (wa bara na visiwani), mfano:
      • umepelekea kuwa na utitili wa taasisi na ofisi ambazo zilistahili kuwa moja, nataja kwa uchache tu; NEC Vs ZEC, NBS Vs Office of Chief of Government Statics of Zanzibar, TRA Vs Zanzibar Revenue Board, HELSB Vs Zanzibar Higher Education Loan Board
      • umepelekea kuwa na utitili wa viongozi hasa kwenye vyama, mfano katibu wa bara na katibu wa zanzibar
      • muundo wa sasa ndio uliopelekea Zanzibar kuwa na utitili wa wabunge kwenye bunge la Jamuhuri ya Muungano
      • nk.
 
ajitahidi kuwa unganisha wananchi wa tanzania bila kujali itikadi za vyama vyao ilitusonge na kuishi pamoja kama taifa.
 
NITAMSHAURI ANUNUE MATREKTA MENGI NA AAMRISHE KUWA NA MASHAMBA YA SERIKALI KILA KIJIJI,WILAYA BA MKOA ILI KUTIMIZA USEMI "KILOMO NI UTI WA MGONGO"
 
Ushauri ni muhimu hata kama anayeshauriwa hataupenda...Mimi nitamshauru awaache wapinzani waendelee na shughuli zao za kisiasa
 
Mkeo alikuwa sawa alipogoma kukufanyia kampeni. Huna uwezo wa kuongoza Tanzania hata chembe. Umejaa chuki za kutisha na unadhani vitisho vyako vya kila kukicha ndiyo kuongoza nchi. Hutaki ushauri wa yeyote ule kwa kujiona wewe ni mjuaji wa kila kitu. Unadharau katiba na sheria mbali mbali za nchi. Jiuzulu haraka sana ili uinusuru nchi yetu na majanga makubwa ya kuwa na mtu dhalimu aliyejaa chuki za kutisha kama wewe eti ndiye kiongozi wa Watanzania.
 
Namshauri abadilishe TANROAD muundo wake uwe kama TANESCO.
Mainjinia wa Tanroad hawana hata machepeo shimo likitokea barabarani wanatangaza tenda ya kuziba hawana hata concrete mixer mbona TBA wanajenga majengo.
Museveni aliagiza vifaa vya ujenzi akapeleka wilayani serikali ifanyie kazi. Zamani ilikuwepo PEHACO sababu za kutokuwa na usimamizi ikafa hii irudi kwa usawa wa Mukulu haitakufa .
Meneja wa TANROAD awe na ka unit ka maintanance kafanye kazi ushauri wangu huo kwa Mheshimiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom