Ukiona umefika miaka ya thelathini haujaoa/kuolewa, jifanyie assesment mwenyewe

live-your-life-impressing-yourself.jpg
 
Mke/ Mme mwema hutoka kwa Bwana. Na kamwe huwezi kumpangia Bwana akupe mtu huyo kwa wakati gani!

Kaa subir uona km bwana atakushushia mume. Kuna ule mfano wa kwenye bible, kuna mtu mmoja aliandaa karam akamwalika Yesu ahudhurie. Basi akaja mtummoja kachoka yupo yupo, wakadhani chokoraa, wakampa makombo wakamwamuru aondoke. Baadaye jamaa akamuuliza yesu, mbona hukuja? akasema nlikuja mbona mkanipa yale makombo af mkaniambia tambaa? Ndo walivyo dada zetu, ukitaka kumuoa lazma uwe unafanya kaz Bank n.k. Saiz mnamsingizia bwana Yesu, mtakeni lazi Yesu wetu wala hausiki, mlipokuwa mnawavulia nguo wenye pesa mlimshirikisha yesu? Saiz mnachina ndo mnajifanya mnamjua eee?
 
  • Thanks
Reactions: J C
ivi mtu humlishi wala akuombi chochote kuna aja ya kukeleketwa juu yako? pilipili usokula yakuwashia nn??
Mkuu hapa si swala la pili pili wala nini,kama umeangalia taarifa ya habari kile
kitoto kilichoopolewa chooni baada ya kutupwa na mdada aliyejifungua
ni mojawapo ya matokeo ya watu wanaosema bado wanajipanga.
kama mtu maisha ya mjini yamekushinda rudi kijijini.
Ni mara chache kuwakuta watu wa kijijini over 30 hawajaoa kwa kisingizio cha maisha.
Ktk hili binafsi nawatoa wadada kwani wao hawawezi kulazimisha kuolewa,
lakini kwa wanaume,huu uzi umepiga ikulu.Kubadilika ni muhimu.
 
Mkuu Tyta nakukubali sana,lakini kwa hili
lazima binadamu aonyeshe tofauti kati yake na mbuzi.
Huwezi kumwuliza mbuzi ana umri gani,ana mke au watoto akakujibu
Naongelea hasa hiyo ya ''marriage is not about age...''
Issue hapa ni unatafuta mpaka lini?
Kama mhusika anaowaona wote wana kasoro,basi naye ana kasoro
hivyo achukue mmojawapo kati ya wenye kasoro aoe.
 
Last edited by a moderator:
habari za jion wadau.

wadau kama heading inavyosema. hii inawahusu watu wazima wanaojitambua. mashoga, vicheche, wasagaji, unsound mind, haiwahusu.

ukiona umefika 30 na hujaoa wala kuolewa. na una mpango wa kuoa au kuolewa siku moja anza kujiangalia mara mbili.. usiku mwema wote

jiwe limerushwa gizani hilo ukisikia yalaaah ujue limempata mtu.

Usiwalazimishe watu wafuate staili zako za maisha. Mfano kama wewe unalala saa 12 kama jogoo usitake kila mtu ikifika saa 11:59 awe ameshapanda kitandani. Haiwezekani watu wote wakafanya mambo kwa wakati mmoja ndio maana hata vidole vya binadamu havilingani mfano dole gumba linasubiri sana kwa kidole cha kati.
 
Hawa waKantalamba wa rejareja wanavamia mitandao kwa pupa.
 
Mkuu hapa si swala la pili pili wala nini,kama umeangalia taarifa ya habari kile
kitoto kilichoopolewa chooni baada ya kutupwa na mdada aliyejifungua
ni mojawapo ya matokeo ya watu wanaosema bado wanajipanga.
kama mtu maisha ya mjini yamekushinda rudi kijijini.
Ni mara chache kuwakuta watu wa kijijini over 30 hawajaoa kwa kisingizio cha maisha.
Ktk hili binafsi nawatoa wadada kwani wao hawawezi kulazimisha kuolewa,
lakini kwa wanaume,huu uzi umepiga ikulu.Kubadilika ni muhimu.

Kwani kuoa/kuolewa lazima?
 
"Kama una mpango wa kuoa/kuolewa"..ni kweli kwa mawszo yangu pia. Kama huna mpango huo, hili halikuhusu..!!
 
ivi mtu humlishi wala akuombi chochote kuna aja ya kukeleketwa juu yako? pilipili usokula yakuwashia nn??

Wabongo wengine utawaweza kwa kuvunja faragha maisha ya wenzao wakati dunia hii inaelekea kwenye individualism sasa hivi.

Mtu kaamua kuishi kivyake, unamlazimisha aoe/ aolewe.

Kama hataki kuoa/ kuolewa kwa sababu ana matatizo ya akili na hataki kumsumbua mkewe/ mumewe na kuzaa watoto watakaorithi matatizo ya akili?
 
"Kama una mpango wa kuoa/kuolewa"..ni kweli kwa mawszo yangu pia. Kama huna mpango huo, hili halikuhusu..!!

Hivyo sivyo alivyosema mleta mada.

Kama una mada tofauti anzisha thread yako.
 
Mkuu Tyta nakukubali sana,lakini kwa hili
lazima binadamu aonyeshe tofauti kati yake na mbuzi.
Huwezi kumwuliza mbuzi ana umri gani,ana mke au watoto akakujibu
Naongelea hasa hiyo ya ''marriage is not about age...''
Issue hapa ni unatafuta mpaka lini?
Kama mhusika anaowaona wote wana kasoro,basi naye ana kasoro
hivyo achukue mmojawapo kati ya wenye kasoro aoe.

.......hapo ndipo unapokosea....kwanza si kila ambaye hajaoa bado anatafuta.....kuoa kama fasheni au kwa kuwa ni utamaduni ndio kunakoponza wengi.....labda unipe sababu za msingi usawa uliopo kwa mtu wa miaka 18-29 kuoa na utofauti wao na mtu wa miaka 30+
 
Back
Top Bottom