Ukiona Dalili hizi jua uzee ndio huo unabisha mlangoni

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
27,225
65,645
Wakuu mpo Salama!

Kuna Watu hawajui kuwa namna uzee unavyoingia. Sio ajabu wameshaingia uzee lakini hajui au hawana uhakika.

Sasa hizi ni moja ya dalili kuu zinazoashiria kuwa unaingia katika uzee.

1. Kufananisha Watu au Mahali au matukio

Kuna ile ukimuona mtu unafikiri ulimuona wapi hata kama hujawahi kumwona kabisa. Hali hiyo ukianza kuiona jua huo ndio mwanzo kabisa wa uzee. Mara nyingi hali hiyo huanza mtu akiwa na miaka 25.

Kadirii unavyokua ndio hali hiyo inazidi.

Hiyo ni kupoteza kumbukumbu.

Kuna ile upo sehemu ambayo ndio siku ya kwanza umefika lakini unajiona kama uliwahi kufika eneo hilo. Huo ndio uzee wenyewe 😃.

Au unafanya tukio lakini unaona uliwahi kulifanya lakini haukumbuki vizuri.

Huo ndio uzee wenyewe umegonga mlango.

Hali hizo husababishwa na wingi wa majukumu na akili kuwa na mambo mengi.

2. Kupoteza Interest na Ishu za Muziki na waigizaji.
Yaani ukiwaona wanamuziki unaona kama wanafanya mambo ya kitoto. Kwa upande wangu hali hiyo ilinipata tangu nikiwa ninamiaka 22. Yaani nikiona mwanamuziki au muigizaji namchukulia kama mtoto. Sipo interest naye na sanaa yake.

Kikawaida wazee hawapendi Entertainment, kuintateiniwa, kuchezewa drama au vitu vyote vya akili nyepesi na uzee haviendi.

Ukiona unapunguza kukaa kwenye Luninga hata wakati ukiwa na muda labda ni weekend au umetoka kazini lakini huwezi kuangalià muziki au maigizo jua uzee unakunyemelea.

Ishu za Entertainment ni za vijana hasa vijana ambao bado hawana majukumu.

3. Majibu mafupi na hutaki Fujofujo au Ligi
Kikawaida maisha yalivyo yapo kwaajili ya kukutuliza, kuku- Neutralise. Yaani kukufanya uwe mpole. Utaanza kwa mbwembwe kutokana ni damu changa na bado maisha hayakupiga katafunua Ambakati moja matata.
Lakini ukishaona unamajibu mafupi na hautaki ligi na upo tayari kushindwa kama haidhuru. Ujue uzee ndio huo sasa.

Itafikia hatua mpaka Nzi utamuacha akufanye vile atakavyo😊.

4. Kuwa Jeshi la mtu Mmoja
Uzee unakuja na mikwaju mikali itakayokufanya ujikute upo pekeako.

Ujana utakuwa ni mtu wa marafiki wengi lakini ukishaona mara kwa mara unakuwa pekeako na unafanya mambo mwenyewe mwenyewe. Yàani jeshi la mtu mmoja basi elewa uzee ndio huo unakuta.

Kwa sisi ambao tumekaa na wazee tumeona maisha yao tunajua pale ambapo mtu uzee unamuanza.

Uzee huanza ukiwa na miaka 25. Siku utakayoanza kujiona upo mpweke, basi elewa kuwa upo kwenye hatua za awali za uzee. Hivyo utajaribu kuudhibiti kwa Kuoa na kuwa na familia. Lakini utakuwa haujaudhibiti zaidi ya kuuzuga tuu.

5. Kutaka Umoja ambao hauwezekaniki.
Uzee na utoto umetenganishwa na Ujana. Hivyo uzee na utoto kwa kiasi kikubwa kuna sifa zinaingiliana.
Watoto hupenda umoja, kufanya vitu kwa pamoja. Lakini kwenye ujana vitu vya pamoja na umoja hakuna kwani kila mtú anajiona ananguvu na anauwezo wa kufanya mwenyewe.

Ukishaona kwenye ukoo wenu wewe unataka na kutamani familia yenu muwe na umoja, mpendane na mshirikiane. Basi elewa huo ndio uzee wenyewe

Acha Nipumzike kwanza.
Maana uzee umeniingia.
 
Kitambo uko nilikua napenda sana gari iwe na sound kubwa hadi walioko nje wakereke,lakini sasa sipendi hata kusikiliza redio nikiwa kwenye gari,juzi kati nikiwa peke yangu nilisafiri umbali wa zaidi km 150 sikuwasha redio safari yote,uzee huu hapa aisee 🤔
 
Back
Top Bottom