Mwalimu Nyerere, legacy yake kamwe haitafutika. Legacy ya Mwalimu Nyerere ni kuwaongoza Watanganyika kupambania uhuru wao mpaka ulipopatikana.
Legacy haiwezi kuwa kujenga daraja, barabara, shule au hospitali, maana huko mbeleni, hivyo vitu vitakuja kujengwa vilivyo bora na vingi maradufu.
Samia alipoyachukua madaraka, watu walihisi huenda atakuwa Licoln wa Tanzania, lakini siku zilivyoenda matumaini yakazidi kutoweka!
Marekani mpaka leo ina watu 46 ambao wamewahi kuwa marais tokea uhuru wao. Lakini marais pekee wenye legacy ya kudumu ni wawili tu, George Washington na Abraham Lincoln. George Washington aliongoza harakati za kupata uhuru kutoka kwa Mwingereza. Na Lincoln ndiye iliyeanzisha na kujenga mifumo ya kidemokrasia nchini Marekani. Baada ya hapo, hawa marais wengine, wanakuja na kuondoka, na majina yao kusahaulika. Lakini George Washington na Abraham Lincoln, majina yao yameendelea kuishi.
Tanzania tuna George Wahington wetu, Mwalimu Nyerere, LAKINI tumeshindwa kumpata Abraham Lincoln wetu. Wote wanaochukua uongozi, wanaingia na kutoka bila ya kuacha legacy yoyote ya kudumu.
KIkwete alielekea kuacha legacy ya katiba mpya, akafeli. Samia akajaribu kuonesha dhamira ya kukamilisha upatikanaji wa katiba mpya na kutaka kutengeneza mifumo ya haki, lakini hakwenda mbali, akafeli kabisa kabla hajaanza, na sioni akionesha dalili za kuacha legacy yoyote.
Tunaendelea kujiuliza, ni nani kiongozi katika nchi yetu atakuja kuacha legacy kwenye nchi yetu? Baadhi wameishia kuacha legacy ya manung'uniko!! Mkapa kwenye kitabu chake ameacha manung'uniko kuwa anasikitika utawala wake uliua Wazanzibari waliokuwa wakidai haki kwenye uchaguzi, na kuwa aliwezesha CCM kuiba hela ya Serikali. Huenda na Rais Samia, naye anafikiria kuacha manung'uniko badala ya legacy halisi.
Kama Samia angefanya mabadiliko ya msingi ya kisheria kuwezesha demokrasia na haki kutamalaki, hakika angekuwa ameacha legacy kwa vizazi vyote. Lakini hakuna dalili. Kununua magoli, kugawa mitungi ya gas, kusafiri na wasanii, kumalizia miradi iliyoanzishwa na marehemu, n.k. kamwe haviwezi kutengeneza legacy. Hivyo ni vitu unapigiwa makofi, imeishia hapo.
Kuna legacy mbaya ya upande mwingine kwa kiongozi, kama utawala wako utasababisha maafa. Kwa kiongozi, bila ya kujali nani ameanzisha, maafa ya wananchi yakitokea wakati wa uongozi wako, ni uthibitisho wa wewe kushindwa kuongoza nchi.
Rais Samia ana machaguo matatu: Kuacha legacy njema ya kukumbukwa, legacy mbaya ya kulaaniwa vizazi vyote, au kupita kama vile hakuwahi kuwepo.
Ifahamike kuwa:
legacy in a broad sensse refers to a lasting impact and the way you will be remembered for generations to come.